100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa neno "Kotokoto"

    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa neno "Kotokoto"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO.”

    13 JUNI 2024

    13 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uvuvi endelevu kwa kutumia kanuni za uvuvi na tunafuatilia mtazamo wa wakazi wa eneo la ziwa Taganyika kuhusu kufungwa zia hilo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za watoto katika migogoro, Ualbino na COSP17. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “Kotokoto.”
    Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu viwango vya ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo ya mizozo yenye matumizi ya silaha inaonesha kuwa mwaka 2023 kulikuwa na ukatili wa kupindukia. Ripoti hiyo inayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kila mwaka inasema “Mwaka wa 2023 watoto waliandikishwa na kutumika vitani ikiwa ni pamoja na kwenye mstari wa mbele, kushambuliwa majumbani mwao, kutekwa nyara wakielekea shuleni, shule zao zikitumiwa kijeshi, madaktari wao wakilengwa, na orodha ya kutisha inaendelea. Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu kufurahia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, Muluka-Anne Miti-Drummond amepongeza maendeleo ya pamoja yaliyopatikana katika kufuatilia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipotambua rasmi tarehe 13 Juni kuwa Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino miaka kumi iliyopita. Hata hivyo, amesema wanatambua kwamba safari ya kuelekea katika  ulimwengu wa haki sawa kwa watu wenye ualbino bado inakumbwa na changamoto na ugumu mkubwa.Na leo ndio ndio tamati ya Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, COSP17 uliodumu kwa siku tatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Sarah Muthoni Kamau, Mwenyekiti wa Jukwaa la Watu wenye ulemavu la Jumuiya ya Madola ni mmoja wa waliohudhuria mkutano huu uliodumu kwa siku tatu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 9 min
    Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia

    Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia

    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Hebu tutekeleze ahadi zetu kukomesha ajira ya watoto” tunaelekea nchini Argentina kukutana na muathirika wa ajira ya watoto ambaye sasa  ameamua kulivalia njuga suala hilo na anafanya juu chini kuitokomeza ajira kwa watoto ambayo imekita mizizi nchinihumo kwa miaka nenda miaka rudi.  Kwa mujibu wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO ajira kwa watoto ni ukiukwaji mkubwa wa haki zao n ani uhalifu unaokwenda kinyume na sheria na mikataba ya kimataifa ya kazi lakini pia ni kosa la jinai.  Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii.

    • 3 min
    Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu: Simulizi kutoka Sudan 

    Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu: Simulizi kutoka Sudan 

    Nchi ya Sudan inakabiliwa na hatari inayoongezeka ya njaa inayosababishwa na migogoro ambayo itakuwa na matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha, haswa kwa watoto wadogo. Hata pale wananchi wanapojaribu kukimbia vita ili kwenda kusaka msaada maeneo mengine wanakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kuporwa mizigo yao na makundi ya wapiganaji. Leah Mushi na maelezo zaidi.
    Kiujumla hali ni mbaya nchini Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya makundi mawili ambayo ni vikosi vya kijeshi vya serikali na vikosi vya msaada wa haraka. Wananchi maisha yao yamebadilika kabisa maana sasa hawawezi kuendelea na shughuli zao za kawaida kama vile kilimo. 
    Mmoja wa waathirika wa vita nchini Sudan ni Bi. Thuraya mwenye umri wa miaka 37 aliyekimbia eneo la El Fasher Kaskazini mwa Darfur na watoto wake kwenda kusaka hifadhi katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam anasema maisha yamekuwa magumu hawana hata chakula cha kuwapikia watoto. “Tumekuja kutokea Tawila, tulilazimika kuondoka usiku, hatukuweza kuondoka mchana sababu tulikuwa tunaogopa mapigano na silaha nzito. Walitukagua na kututishia, mnaenda wapi? mmebeba nini kwenye mabegi yenu?. Walichukua vitu vyetu na kutuacha na vitu vichache, na hela kidogo tulizokuwa nazo tuliweza kufika katika kambi hii ya wakimbizi.”
    Masikini Bi.Thuraya anatamani maisha yake kabla ya vita. “Kabla ya vita maisha yetu yalikuwa ya furaha, tulikuwa tunaenda shambani, hatukuwa tunanunua mkate wala chochote sokoni. Tulikuwa tukienda huko tunanunua nguo. Tulikula nyama kutoka kwenye mifugo yetu majumbani lakini wameiiba yote. Tulivyofika hapa kambini walitupa vitu vichache lakini vimeisha vyote. …… Ujumbe wangu kwa dunia ni watusaidie tupate amani. Hilo ndilo jambo letu Pekee.”
    Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, ikijumuisha lile la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Mpango wa Chakula (WFP) na la Afya Duniani (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto.
     

    • 1 min
    Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

    Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

    • 2 min
    12 JUNI 2024

    12 JUNI 2024

    Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.
    Simulizi kutoka Sudan: Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu.
    Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia.
    Mashinani: Kutokana na kuzuka upya kwa mizozo katika jimbo la Equotoria Magharibi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umeimarisha uwepo wa askari wake wa kulinda amani ili kuwalinda na kuwapatia msaada wa kibinadamu mamia ya watu katika kambi za wakimbizi wa ndani za eneo la Tambura.
     
     

    • 10 min

Top Podcasts In News

Mark Levin Podcast
Cumulus Podcast Network
Bad Faith
Briahna Joy Gray
Amanpour
CNN
پرگار
BBC Persian Radio
កម្មវិធីវិទ្យុពេលព្រឹក - វីអូអេ
វីអូអេ
2 Old 4 TikTok
2 Old 4 TikTok

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations