100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mfumo wa kutoa tahadhari mapema warejesha imani kwa wakazi wa Ituri, DRC

    Mfumo wa kutoa tahadhari mapema warejesha imani kwa wakazi wa Ituri, DRC

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari mapema kuhusu mashambulizi dhidi ya raia yanayoendeshwa na waasi kwenye mji wa Bunia jimboni Ituri. Mfumo huu unaweza jamii, jeshi la serikali na MONUSCO kubadilishana taarifa na hivyo wananchi wanakuwa na hakikisho la usalama wao kwani pindi taarifa inapotolewa, hatua sahihi zinachukuliwa kama anavyosimulia Assumpta Masso kwenye makala hii iliyofanikishwa na MONUSCO.

    • 3 min
    WHO: Takribani watu milioni 1.6 huugua kila siku kutokana na chakula kisicho salama

    WHO: Takribani watu milioni 1.6 huugua kila siku kutokana na chakula kisicho salama

    Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. 
    Hii leo kupitia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi uliowahusisha Dkt. Francesco Branca, Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula wa FAO imeelezwa kuwa madhara yatokanayo na chakula kisicho salama hayaangalii mipaka na yametapakaa katika nchi nyingi duniani.  
    Dkt. Francesco Branca aliyekuwa katika ukumbi huo wa mikutano ametoa taarifa kwamba "kutokana na kuugua kwa takribani watu milioni 1.6 kila siku kunakosababishwa na vyakula visivyo salama, watu 420,000 hufariki dunia kutokana na sababu hiyo."
    Mwaka huu, kaulimbiu ya kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, ni Jiandae kwa Yasiyotarajiwa, ambayo sio tu inasisitiza umuhimu wa kuwa tayari kudhibiti matukio ya usalama wa chakula ili yasiwe ya dharura, lakini pia umuhimu wa kuchukua muda kupanga, kuandaa na kuwa tayari kuchukua hatua katika mazingira ya dharura.
    Kwa upande wake Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula katika Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), kwa njia ya video akizungumza kutoka Roma, Italia ameeleza namna FAO inavyohusisha chakula salama na utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu…anasema, “Chakula kinapozalishwa na kuuzwa katika mfumo wa kilimo salama na endelevu, kinachangia maisha yenye afya na kuboresha uendelevu kwa kuwezesha upatikanaji wa soko na tija, ambavyo vinasukuma maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umaskini, hasa katika maeneo ya vijijini.”

    • 1 min
    07 JUNI 2024

    07 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa chakula, na ripoti ya ILO kuhusu suala la ajira Gaza wakati huu wa machafuko. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?
    Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Tukimulika suala la ajira Gaza ambapo ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda huo wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5..Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa anatupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mashambulizi ya mara kwa mara kutoka makundi ya waasi waliojihami dhidi ya raia, yamesababisha Umoja wa Mataifa na kuja na mfumo wa kutoa tahadhari mapema ili kuimarisha ulinzi wa wa raia.Mashinani leo ikikiwa ni siku ya usalama wa chakula duniani tunakwenda nchini Sudan kumulika masuala ya lishe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 10 min
    Vita katika ukanda wa Gaza yasababisha ukosefu wa ajira kufikia asilimia 80 – ILO

    Vita katika ukanda wa Gaza yasababisha ukosefu wa ajira kufikia asilimia 80 – ILO

    Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5. 
    Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kati ya kila watu 10 Ukanda wa Gaza wenye uwezo wa kufanya kazi, ni watu wawili tu wenye ajira, imesema ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa ushirikiano na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina kuonesha ni kwa vipi vita imeathiri soko la ajira na njia za kujipatia kipato kwenye eneo hilo la Palestina linalokaliwa na Israeli.
    Ripoti inasema miezi minane ya vita imesababisha watu kupoteza kwa kiwango kikubwa ajira na mbinu zao za kujipatia kipato Gaza.
    Ukingo wa Magharibi nako vita hiyo imeathiri vibaya kwani ukosefu wa ajira umefikia asilimia 32.
    Ripoti inaonya kuwa takwimu hazijumuishi wale waliolazimika kuacha kazi kwa sababu ya vita, na kwamba idadi halisi ya waliolazimika kuacha kazi ni kubwa kuliko kinachodokezwa kwenye ripoti.
    Biashara zikiwa zimefungwa, kipato cha kaya nacho kimepungua kwa asilimia 87 na zinatuma watoto wao kufanya kazi ili kupata kipato.
    Mkurugenzi wa ILO Kanda ya nchi za kiarabu Ruba Jadarat anasema vita Gaza imesababisha vifo, hali ngumu ya kibinadamu ikiambatana na kusambaratika kwa hali ya kiuchumi na kujipatia kipato Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hivyo kurejesha mbinu za watu kujipatia kipato na kuweka fursa za ajira zenye hadhi ni muhimu ili wapalestina waweze kukwamuka kutoka kwenye vitisho na ukatili ambao vita imewatumbukiza.
    Amesema kukwamuka huko kuende sambamba na harakati za sasa za usaidizi wa kibinadamu na kwamba ILO na wadau wake wanatekeleza kupitia Mpango wa Hatua wa Dharura kwa Palestina.

    • 2 min
    Jifunze Kiswahili - Pata ufafanuzi wa neno "Nyendea"

    Jifunze Kiswahili - Pata ufafanuzi wa neno "Nyendea"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya neno “NYENDEA”

    06 JUNI 2024

    06 JUNI 2024

    Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 
    -Gaza Nuiserat Israel imeshambulia shule moja iliyokuwa inahifadhi wakimbizi 6,000 wa kipalestina na kuua watu 35, na wengine wengi wamejeruhiwa,
    -Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika tukio la kukumbuka wafanyakazi 188 wa chombo hicho waliouawa mwaka 2023 pekee wakiwemo 135 watumishi wa UNRWA waliouawa ukanda wa Gaza
    -Duniani kote mtoto mmoja kati ya wanne anaishi katika mazingira ya umaskini wa chakula akila aina moja au mbili tu ya mlo kutokana na vita, mizozo, janga la tabianchi na ukosefu wa uwiano, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. 
    -Katika mada kwa kina utamsikia Erick Mukiza mmoja wa wanasheria waliothibitishwa kuwa wapatanishi au wasuluhishi wa migogoro nje ya mahakama nchini Tanzania na mipango yake ya kujumuisha wenye ulemavu ili wanufaike na mpango huo wa serikali ya Tanzania.
    -Na katika jifinze Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno Nyendea

    • 9 min

Top Podcasts In News

The Don Lemon Show
Lemon Media Network
Face à Michel Onfray
Goussard Thomas
Le Meilleur de l'info
CNEWS
Soir Info Week-End
CNEWS
Punchline
CNEWS
The Daily
The New York Times

More by United Nations

Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations