100 épisodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • Actualités

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    04 JUNI 2024

    04 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako UNICEF na wadau wake imefanikisha utengenezaji wa sodo za kufuliwa. Piatunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, wahamiaji kutoka bara la Afrika na watoto katika migogoro. Mashinani inatupeleka nchini DR Congo, kulikoni?
    Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) imeripoti ubomoaji wa makazi leo kwenye eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu katika miji ya Shuqba, Al Jwaya na Mantiqat Shi'b al Butum, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imeangazia hatari zinazowakabili wakimbizi na wahamiaji wanapokuwa njiani kutoka Afrika kwenda Ulaya. UNHCR imeweka wazi kuwa wengi wao hufariki dunia wakivuka jangwa au karibu na mipaka, hufanyiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Shirika hilo limetoa wito kwa wafadhili kuangazia usaidizi na watu kuelezwa njia mbadala halali za kuhama nchi.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kukumbuka watoto walio kwenye maeneo yenye mizozo ikihusisha ukatili na unyanyasaji, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Denise Brown ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kukataa kuhalalisha vita na athari zake kwa watoto. Akitathimini hali ya watoto nchini Ukraine kutokana na uvamizi wa Urusi amesema zaidi ya watoto 600 wameshauawa na 1,420 wamejeruhiwa tangu Februari mwaka 2022.Katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka watoto wasio na hatia waathiriwa wa uvamizi na ukatili tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya msichana ambaye alitumikishwa na makamanda wa kundi la waasi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 13 min
    Watumiaji wa baiskeli wasema manufaa ni zaidi ya afya

    Watumiaji wa baiskeli wasema manufaa ni zaidi ya afya

    Baiskeli! Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wake tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi. Huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, taifa lililo Afrika Mashariki, utamaduni wa kutumia baiskeli kama njia ya usafiri unazidi kushamiri na miongoni mwa watumiaji hao wanaelezea kwenye makala hii msingi wa matumizi, changamoto na nini kifanyike ili matumizi ya baiskeli yawe salama.

    • 3 min
    UNRWA: Gaza hali si hali tena huku watu milioni 1 wakikimbia Rafah

    UNRWA: Gaza hali si hali tena huku watu milioni 1 wakikimbia Rafah

    Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. 
    Katika tarifa yake iliyotolewa leo kupitia mtandao wa kijamii wa X UNRWA imesema mji wa Rafah kwenye mpaka wa kusini wa Gaza na Misri ulikuwa nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao kwa karibu miezi minane ya mashambulizi ya kila siku ya jeshi la Israel, kujibu shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana.
    "Maelfu ya familia sasa wanaishi katika vituo vilivyoharibiwa na kusambaratishwa huko Khan Younis ambapo UNRWA inaendelea kutoa huduma muhimu, licha ya changamoto zinazoongezeka. Masharti hayaelezeki,” 
    Haya yanajiri siku tatu tangu Rais wa Marekani Joe Biden kuzindua pendekezo la usitishaji mapigano kwa kuzingatia usitishaji wa hatua kwa hatua kwa vita hiyo, pendekezo likiripotiwa kujumuisha kuondolewa kwa majeshi ya Israel kutoka maeneo wyalikorundikana, kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina, pamoja na mpango wa ujenzi mpya wa Gaza.
    Kulingana na UNRWA, maelfu ya familia zimelazimika kutafuta makazi katika majengo yaliyoharibiwa vibaya huko Khan Younis jiji ambalo liko kaskazini mwa Rafah, na linakadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 1.7. 
    Imeripotiwa kwamba makao yote 36 ya UNRWA huko Rafah sasa yamesalia matupu.
    Shirika hilo limeongeza kuwa Takriban wanawake na wasichana 690,000 wanaaminika kukosa vifaa vya msingi vya usafi wakati wa hedhi, faragha na maji ya kunywa.
    Ikiangazia mapambano ya kila siku yanayowakabili watu walio hatarini sana huko Gaza, UNRWA imelinukuu Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uzazi UNFPA ambalo linakadiria kwamba karibu wanawake 18,500 wajawazito wamelazimika kukimbia Rafah. 
    "Takriban 10,000 zaidi wamesalia huko katika hali mbaya na upatikanaji wa huduma za afya na vifaa vya uzazi ni mdogo. Afya ya mama na mtoto iko hatarini.”
    Likirejea wasiwasi huo mkubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP  kupitia Matthew Hollingworth, Mkurugenzi wa WFP katika eneo linalokaliwa la Palestina lisema sasa hakuna "kikubwa tunachoweza kuwafanyia watu ambao bado wako Rafah, ambako barabara si salama, hazifikiki vizuri, na washirika wetu wengi na mashirika mengine ya kibinadamu yametawanywa”.
    Ameonya kwamba hofu ya afya ya umma sasa imevuka viwango vya janga, wakati sauti, harufu, na maisha ya kila siku, ni ya kutisha na ya kuzimu. Watu "wamekimbilia maeneo ambayo maji safi, vifaa vya matibabu na usaidizi havitoshi, usambazaji wa chakula ni mdogo, na mawasiliano ya simu yamesitishwa."

    • 1m
    03 JUNI 2024

    03 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na afya ya uzazi nchini Randa. Mashinani tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?
    Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto.Katika makala Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wa baiskeli tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi.Na mashinani tutaelekea Mwanza nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mikakati ya kudhibiti uhalifu katika mipaka Afrika mashariki.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    • 9 min
    UNICEF yafanikisha mradi wa Lishe Bora kwa Wanawake Wajawazito nchini Rwanda

    UNICEF yafanikisha mradi wa Lishe Bora kwa Wanawake Wajawazito nchini Rwanda

    Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto. 
    Nshimiyimana Clementine, ni Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kabaya, Wilayani Ngororero katika Jimbo la Magharibi nchini Rwanda anasema, “Wajawazito wanapata taarifa kutoka kwa Wahudumu Afya Jamii ambao wanawaelekeza kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya vipimo muhimu na kupata vidonge vya lishe.”
    “Tunawashauri kumeza kidonge kimoja kila siku angalau kwa miezi sita. Na sasa kwa kuwa tumeanza kusambaza vidonge lishe hivi tunaamini vitakuwa na manufaa kwa kuzingatia lishe zilizomo. Wajawazito hawatakosa virutubisho kutoka kwenye matunda na mbogamboga kwa kuwa hivi vidonge vinavyo. Japo bado tunawahimiza wajawazito kula matunda na mbogamboga, lakini wale wasiomudu hawataathirika na upungufu wa virutubisho. ”
    Umugwaneza Yvette ni mmoja wa wajawazito wanufaika wa programu hii iliyowezeshwa kwa ukarimu wa KIRK Humanitarian shirika lisilo la kiserikali linalojitolea kuhakikisha Virutubisho lishe kupitia Umoja wa Mataifa vinawafikia wajawazito kokote waliko duniani.
    “Wakati usambazaji wa vidonge vya MMS ulipoanza, nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kupokea. Mwili wangu umevipokea vizuri. Sijapata changamoto yoyote. Ninameza mara kwa mara na ninajisikia mwenye afya.”

    • 1m
    Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay

    Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay

    Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italeta manufaa. Suala hilo hilo pia lilikuwa miongoni mwa mijadala ya jukwaa la 4 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali huko Manama, Bahrain ambapo mmoja wa wanajopo alikuwa Profesa Dokta Selvaraj Oyyan Pillay kutoka Malaysia ambaye katika makala hii Assumpta Massoi alizungumza naye na kuumuliza iwapo ana shaka na shuku kuhusu mustakabali wa akili mnemba na nini kifanyika.

    • 3 min

Classement des podcasts dans Actualités

L’Heure du Monde
Le Monde
Les actus du jour - Hugo Décrypte
Hugo Décrypte
Journal Afrique
RFI
Journal Monde
RFI
Today in Focus
The Guardian
Les Enjeux internationaux
France Culture

Plus par United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Interviews
United Nations
ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
The Lid is On
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations