100 episodios

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • Noticias

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao

    UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao

    Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha.
    Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea mjini Yerusalemu, Bi. Guimond amesema unapoingia tu kwenye kivuko cha Shalom na lango linafungwa, unahisi umefungiwa kwenye dunia ya uharibifu. Kuanzia shule, hospitali, makazi yaliyolundikana watu na uhaba wa vitu, watu wakihaha kusaka usalama, wanawake wakimuuliza vita itakoma lini? Na zaidi ya yote. 
    “Wakazi wa Gaza wanataka hii vita ikome. Kila siku ambayo mzozo huu unaendelea, inazidi kuleta uharibifu na mauaji. Lazima hii ikome. Wavulana na wasichana walikuwa wananiuliza ni lini vita hii itaisha? Nami sikuwa na jibu la kuwapatia.” 
    Akaendelea kusema.. 
    “Gaza ni zaidi ya simulizi zaidi ya milioni mbili za kupoteza. Kila mwanamke niliyekutana naye ana simulizi ya kupoteza mtu. Zaidi ya wanawake 10,000 wamepoteza wapendwa wao. Zaidi ya familia 6,000 zimepoteza mama zao. Wanawake na wasichana milioni 1 wamepoteza utu wao, makazi yao, familia zao na kumbukumbu zao.” 
    Bi. Guimond akasema kwa sasa..
    "Swali si kwamba ni nini wanawake wanahitaji: Swali linapaswa kuwa ni nini wanawake hawahitaji. Wanawake hawataki kufa, hawataki kuzika wapendwa wao, hawataki kubakia wenyewe kupata machungu.”

    • 2 min
    UNHCR: Utoaji wa vitambulisho kwa wakimbizi nchini Ethiopia waboresha maisha yao

    UNHCR: Utoaji wa vitambulisho kwa wakimbizi nchini Ethiopia waboresha maisha yao

    Wakati dunia hapo jana Juni 20 ikiwa imeadhimisha siku ya wakimbizi duniani na wito kutolewa kila kona wa kuhakikisha wakimbizi wanajumuishwa katika masuala yote ya kuweza kuwasaidia kustawi katika nchi wanayopatiwa hifadhi hii leo tunaelekea nchini Ethiopia kujionea namna mradi wa kutoa vitambulisho vya kitaifa ambao unajumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi ulivyobadiliasha maisha ya wakimbizi. 
    Makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inathibitisha namna mradi huo wa vitambulisho vya kitaifa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia umeleta matumaini pamoja na upatikanaji wa ajira kwa wakimbizi na hivyo kuwaondoa katika kundi la watu tegemezi kwani sasa wanaweza kufanya shughuli za kuwaingizia kipato. Leah Mushi anatujuza zaidi. 

    • 3 min
    Jengo la uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko mpakani Mutukula lakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania

    Jengo la uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko mpakani Mutukula lakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini. 
    Hatua hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapema dhidi ya milipuko ya magonjwa imekuja ukiwa umetimia mwaka mmoja kamili tangu  mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya virusi vya Marburg ulipotangazwa kuisha kabisa nchini Tanzania baada ya kuwa umetokea mwanzoni mwa mwaka jana 2023  katika mkoa wa Kagera kaskazini magharibi mwa nchi.
    Dkt. Janeth Masuma, Afisa wa Kitengo cha WHO Tanzania cha kuzuia na kudhibiti maambukizi anasema, “kwa hiyo kwa kuwa na mafanikio haya makubwa ya jengo la utambuzi wa wagonjwa katika mpaka wa Mutukula kutasaidia uchunguzi wa haraka na kuwatenganisha wote wanaohisiwa kuwa na maambukizi ili kuhakikisha mipaka yote imelindwa, kulinda nchi nyingine na kuhakikisha kwamba hakuna wasafiri wowote watapeleka ugonjwa nje ya Tanzania kwa mujibu wa mapendekezo na wajibu wa afya kimataifa.”
    Salum Rajab Kimbau, Mratibu wa Chanjo wa Mkoa wa Kagera anaeleza ilivyo faida kubwa kuwa na jengo la namna hii mpakani akisema, “huu mradi kiujumla una faida kwenye mkoa. Tumeupokea na kufurahi na pia furaha hii iko upande wa halmashauri ya mkoa n anchi kwa ujumla. Mradi una sehemu mbili za matibabu na kinga. Awali tulikuwa tunatumia hema moja ambalo lilikuwa linakusanya wahisiwa wote wa kike na wa kiume lakini hata mazingira yenyewe siyo rafiki kwa maana ya joto kali lakini pia akiingia mgonjwa badala ya kupona kwa haraka au badala ya kukaa kustahimili vizuri inakuwa kazi.”
    Kituo hiki ni moja ya afua nyingi zinazoendelea ili kuhakikisha uimarishaji wa mifumo ya afya nchini Tanzania ili kuongeza kasi ya ajenda ya afya kwa wote.

    • 1m
    21 JUNI 2024

    21 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake huko Gaza, na masuala ya afya nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Ethiopia na mashinani tunasalia nchini Tanzania, kulikoni? 
    Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini.Makala inatupeleka nchini Ethiopia ambako nchi hiyo kwasasa inatekeleza mpango wa kihistoria wa utoaji wa vitambulisho vya kitaifa unaojumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi.Na mashinani tutakepeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe wa watoto kuhusu elimu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 9 min
    Methali: “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”

    Methali: “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”

    • 1m
    20 JUNI 2024

    20 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Japan kufuatilia harakati za kusongesha teknolojia rafiki na nafuu ili dunia iwe mahali salama kwa miti na binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo, na uchambuzi wa methali.
    Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi, Umoja wa Mataifa umeitumia siku hii kutoa wito wa mshikamano na wakimbizi kote duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema, "wanapopewa fursa, wakimbizi hutoa mchango mkubwa kwa jamii zinazowahifadhi."Mashambulizi ya Israel kwa kutumia mabomu kutoka angani, nchi kavu na baharini yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo zaidi vya raia, kuhama makazi yao, na uharibifu wa nyumba na miundombinu mingine ya raia, imeeleza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limeipongeza Chad kwa kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa malale. Chad ni nchi ya kwanza kwa mwaka huu kutambuliwa kwa kutokomeza ugonjwa huo ulio katika kundi la magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs) na inakuwa nchi ya 51 kufikia lengo kama hilo ulimwenguni. Ugonjwa huu husambaa kutokana na binadamu kung’atwa na mdudu Mbung’o mwenye maambukizi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 9 min

Top podcasts en Noticias

公視每日新聞 Daily News
Taiwan Public Television Service
Global News Podcast
BBC World Service
Aristegui
CNN en Español
Unlimited Hangout with Whitney Webb
Whitney Webb
Winaukee Chatter
Camp Winaukee
The TMZ Podcast
TMZ

Más de United Nations

Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
The Lid is On
United Nations
UN Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations