100 episodios

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • Noticias

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa

    Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.

    • 3 min
    Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa

    Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa

    Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. 
    Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis. 
    Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili. 
    Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili.
    Mwenyekiti wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusuu watu wa asili Bi. Hindou Oumarou Ibrahim akizungumza katika jukwaa hilo amesema “Kuondolewa vikwazo kwenye upatikanaji wa fedha ni muhimu ili kuhakikisha watu wa asili wanatekeleza kwa vitendo mipango yao na kuwa na njia ya kudumisha kujitawala,” 
    Kwa upande wake Bwana Li Junhua, ambaye ni msaidizi waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) amesema “unahitaji ufadhili wa muda mrefu, unaotabirika, na wa moja kwa moja kwa Watu wa Asili, ikijumuisha kupitia mifumo ya ufadhili ya umma, ya kibinafsi, na inayoongozwa na Wenyeji ambayo inashirikisha kikamilifu Wanawake na vijana wa kiasili.”
    Unaweza kufuatilia moja kwa moja matangazo ya jukwaa hili yanayorushwa mubashara na Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake wa UN Web TV,matangazo yanarushwa kwa lugha rasmi sita za umoja wa Mataifa ambazo ni Kingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.

    • 1 min
    15 APRILI 2024

    15 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia utekwaji nyara wa watoto wa kike 275 huko Chibok nchini Nigeria, na uwezeshaji kiuchumi wa watu wa asili. Makala inamulika masuala ya mazingira ikiangazia watut wa asili na mchango wao, na mashinani tunakupeleka nchini Chad kusikia simuliza ya mkimbizi kutoka Sudan.  
    Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Makala Stella Vuzo, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, anatuletea mazungumzo kati yake na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhudhuria wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika mwezi uliopita jijini Nairobi, Kenya. Kwa kuwa jamii zinazoishi kiasili wakati mwingine zimekuwa zikilaumiwa kuwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.Na mashinani tunamulika vita nchini Sudan ambayo inaendelea kuwalazimisha mamilioni ya watu kukimbia kuokoa maisha yao. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mkimbizi ambaye alikimbia machafuko nchini humo kuelekea Chad anasimulia changamoto alizozipitia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 11 min
    UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi

    UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi

    Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.  
    Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa. 
    Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiingereza, inaonesha ukweli mchungu wa kufanikisha safari hiyo kwa mtoto nchini Nigeria kuweko shuleni bila uoga. 
    Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Cristian Munduate amesema tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok ni kengela ya kutuamsha juu ya hatari kubwa watoto wetu wanakabiliwa nayo wanaposaka elimu. 
    Anasema leo tunapotafakari janga hili na mengine ya hivi karibuni ni dhahiri kuwa juhudi zetu za kulinda mustakabali wa watoto wetu lazima ziimarishwe. 
    Mwakilishi huyo anasema kwa kuzingatia takwimu zilizotolewa na ambazo zinatia hofu kubwa, ni lazima kupata majawabu ya sio tu dalili bali pia chanzo cha janga hilo la utekaji nyara watoto. 
    Bi. Munduate amekumbusha kuwa elimu ni haki ya msingi na ni njia muhimu ya kuelekea kuondokana na umaskini. Lakini kwa watoto wengi nchini Nigeria inasalia kuwa ndoto isiyotimizika. 
    Ripoti ilimulika maeneo 6 ikiwemo mifumo thabiti ya shule, ukatili dhidi ya watoto, majanga ya asili,mizozo ya kila siku na miunmdombinu ya shule na kubaini utofauti mkubwa wa vigezo hivyo katika majimbo yote 36. 
    Jimbo la Borno liko thabiti kwani limekidhi viwango kwa asilimia 70 ilhali majimbo ya Kaduna na Sokoto bado yako nyuma. 
    Uchambuzi huu unakuja wakati kuna ripoti za ongezeko la ghasia dhidi ya shule ambapo katika miaka 10 iliyopita, matukio ya mashambulizi yamesababisha watoto zaidi ya 1,680 kutekwa nyara wakiwa shuleni au kwinigneko. 
    UNICEF inataka Nigeria pamoja na mambo mengine ihakikishe shule kwenye majimbo yote zina rasilimali za kutekeleza MSSS. 
    Pia itatue pengo la uwiano wa usawa katika hatua za kuimarisha usalama shuleni. Nigeria pia iimarishe usimamizi wa sheria na mikakati ya usalama ya kulinda taasisi za elimu na jamii dhidi ya utekwaji. 
    Kwa sasa UNICEF inashirikiana na serikali kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mazingira salama ya kusomea. 
    Soma ripoti nzima hapa.

    • 2 min
    Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo

    Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo

    Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona. 
    Tukio lilianza kwa ukumbi kuwa giza na video ya dakika tano ikachezwa kueleza kuwa watu wengi wanaijua Rwanda kuanzia 1994, lakini ilikuweko hata kabla ya ukoloni, na kwamba wakoloni ndio waligawa watu kwa misingi ya makundi licha ya kwamba lugha yao ilikuwa moja. Manusura na watekelezaji wa mauaji walizungumza pia kwenye video hiyo!
    Video ikafuatiwa na kuwasha mishumaa kukumbuka waliouawa na kisha hotuba ambapo Katibu Mkuu Guterres akawa ana ujumbe mahsusi kwa vijana wa Rwanda walioshiriki kimtandao na pia ukumbini.
    Anasema rafiki zangu, katu hatutasahau vitisho vya siku 100. Lakini tunahitaji msaada wenu. Tunahitaij sauti na uchechemuzi wenu kusongesha kumbukizi za wale waliouawa. Na kukemea chuki kokote muisikiako au muionapo. Mijini kwenu, vitongojini, shuleni, mtandaoni, popote pale na kila mahali.
    Akaendelea kusema kuwa hebu na tuondoe chuki na ukosefu wa stahmala kokote tuvionapo. Kumbukumbu za waliouawa zichochee vitendo vyetu, na azma yetu ya kuhakikisha dunia bora na salama kwa watu wote. 
    Guterres amesema Umoja wa Mataifa kila wakati utashikamana na vijana katika juhudi hizo muhimu. 
    Mauaji ya kimbari Rwanda ya mwaka 1994 yalifanyika kwa siku 100 kuanzia tarehe 7 Aprili na zaidi ya watu milioni moja waliuawa, wengi wao Watutsi, halikadhalika wahutu wenye msimamo wa kati na watu wengine waliokuwa wanapinga mauaji hayo. 
    Katibu Mkuu amesema siku hizo 100 ziliakisi ubaya zaidi wa ubinadamu. Lakini kipindi baada ya mauaji kilidhihirisha ubora wa roho ya ubinadamu: mnepo, maridhiano, ujasiri na nguvu. 
    Amesema simulizi za manusura ni ushahidi wa nguvu ya matumaini na msamaha ambapo amemtaja manusura Laurence Niyonangira ambaye alipoteza jamaa zake 37 wakati wa mauaji hayo. 
    “Alichagua kusamehe mmoja wa wahusika wa mauaji ya familia yake baada ya mhusika kuungama na kutumikia muda jela kwa makosa aliyotenda. Kama manusura, Laurence alisema ‘tunaweza kuponya vidonda kwa kushirikiana wale waliovisababisha.” Amesema Guterres. 
    Hivyo Katibu Mkuu amesema mwaka huu ambapo kumbukizi inajikita kwenye mzizi wa mauaji ya kimbari ambao ni chuki, ambayo sasa inakolezwa na mitandao ya kijamii, “ni lazima tushikamane pamoja na kurejelea shinikizo la dunia la kuridhia na kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya kimbari, huku tukiimarisha mifumo ya kuzuia, kuelimisha vizazi vipya kuhusu mauaji ya kimbari yaliyopita na kukabili taarifa potofu na za uongo ambazo huchochea kauli za chuki na nia na vitendo ya mauaji ya kimbari.” 

    • 3 min
    Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC

    Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC

    Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu ni Kapteni Fadhila Nayopa, Afisa habari wa kikosi hicho. 

    • 3 min

Top podcasts de Noticias

Mañanas en Libertad
Radio Libertad
Bolsillo
La Vanguardia
Más de uno
OndaCero
Es la Mañana de Federico
esRadio
La Trinchera de Llamas
esRadio
La rosa de los vientos
OndaCero

Quizá también te guste

Más de United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations