24 épisodes

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.  

Jukwaa la Michezo RFI Kiswahili

  • Sports

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.  

  Jukwaa la Michezo - Tuhuma za ukosefu wa maadili zalikumba shirikisho la soka Afrika, CAF

  Jukwaa la Michezo - Tuhuma za ukosefu wa maadili zalikumba shirikisho la soka Afrika, CAF

  Karibui miaka mitatu tangu Ahmad Ahmad kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, shirikisho hilo linakabiliwa na mshororo wa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya fedha. Tunajadili katika makala ya Jukwaa la Michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Juma Mudimi na Bonface Osano

  • 24 min
  Jukwaa la Michezo - Changamoto za marefarii barani Afrika

  Jukwaa la Michezo - Changamoto za marefarii barani Afrika

  Soka la bara la Afrika, limeendelea kushuhudia changamoto mbalimbali za waamuzi au marefarii, huku baadhi wakikosa maadili kwa kujihusisha na upangaji wa matokeo na kutofuata ipasavyo sheria 17 za mchezo huu unaopendwa duniani, kama ilivyoshuhudiwa nchini Tanzania na uongozi wa nchi hiyo kuchukua hatua.

  • 23 min
  Jukwaa la Michezo - Rais wa Fifa apendekeza fainali za Afrika kuchezwa baada ya miaka minne

  Jukwaa la Michezo - Rais wa Fifa apendekeza fainali za Afrika kuchezwa baada ya miaka minne

  Rais wa shirikisho la kandanda duniani Fifa Gian Infantino amependekeza fainali za mataifa ya Afrika kuchezw akila baada ya miaka minne badala ya miaka miwili ya sasa. Tunajadili kwa kina katika jukwaa la michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Mustapha Mtupa, Samwel John na Bonface Osano

  • 16 min
  Jukwaa la Michezo - TP Mazembe, Mamelody Sundowns zafuzu robo fainali ya klabu bingwa Afrika

  Jukwaa la Michezo - TP Mazembe, Mamelody Sundowns zafuzu robo fainali ya klabu bingwa Afrika

  Michuano ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi imeendelea kurindima ambapo klabu za TP Mazembe, Mamelody Sundowns, Zamalek ni miongoni mwa klabu zilizofuzu hatua ya robo fainali. Je msisimko wa michuano hiyo umepungua msimu huu? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi wa soka Mohammed Simbaulanga na Aloyce Mchunga kutathimini kwa kina.

  • 15 min
  Jukwaa la Michezo - Fainali za Afrika 2021 kuchezwa mwezi Januari hadi Februari

  Jukwaa la Michezo - Fainali za Afrika 2021 kuchezwa mwezi Januari hadi Februari

  Shirikisho la kandanda Afrika CAF wiki hii lilitangaza kubadili ratiba ya fainali za Afrika za mwaka 2021 zitakazochezwa nchini cameroon kutoka Juni hadi Januari. Uamuzi huu una tija? Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Bonface Osano na Samwel John kutathimini kwa kina.

  • 24 min
  Jukwaa la Michezo - Changamoto na mafanikio ya soka nchini Rwanda

  Jukwaa la Michezo - Changamoto na mafanikio ya soka nchini Rwanda

  Mchezo wa soka unapendwa na kufuatiliwa kwa kariubu nchini Rwanda hata hivyo taifa hilo la Afrika mashariki bado halijapiga hatua kubwa katika mchezo huo. Tunaangazia mafanikio na changamoto za soka nchini Rwanda. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na Christopher Karenzi, mchambuzi na mwandishi wa habari za spoti kutoka Rwanda

  • 21 min

Classement des podcasts dans Sports

Plus par RFI Kiswahili