24 épisodes

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii RFI Kiswahili

  • Actualités

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Maombolezo ya kitaifa nchini Kenya baada ya kifo cha rais wa zamani Arap Moi, kaimu waziri mkuu wa ubelgiji azuru DRC, China yaahidi kupambana na Corona

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Maombolezo ya kitaifa nchini Kenya baada ya kifo cha rais wa zamani Arap Moi, kaimu waziri mkuu wa ubelgiji azuru DRC, China yaahidi kupambana na Corona

  Maombolezo ya kitaifa yaliendelea nchini Kenya baada ya kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Arap Moi. Nchini Malawi, mahakama ya katiba ilibatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu uliompa ushindi rais Peter Mutharika na huko DRC sakata la mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili, Moise Mbiye lazua sintofahamu jijini Kinshasa kufuatia tuhuma za ubakaji, tume ya uchaguzi Burundi yatangaza idadi ya wapigakura, nchini Marekani baraza la seneta lamuondolea makosa rais wa Marekani, Donald Trump

  • 21 min
  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Rais wa zamani wa Kenya azikwa nyumbani kwake, mauaji yaendelea wilayani Beni, virusi vya Corona vyaangamiza zaidi

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Rais wa zamani wa Kenya azikwa nyumbani kwake, mauaji yaendelea wilayani Beni, virusi vya Corona vyaangamiza zaidi

  Viongozi mbalimbali wa Afrika mashariki na kwingineko duniani walijiunga na Maelfu ya wakenya kushiriki mazishi ya aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Daniel Arap Moi, katika eneo la Kabarak katika kaunti ya Nakuru, na huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wasiwasi kuongezeka kuhusu maambukizi ya virusi hatari vya ebola, kutokana na maelfu ya wakaazi wa Mangina kutoroka makwao, mawaziri wa nchi za nje kutoka Uganda na Rwanda walikutana jijini Kigali, na kimataifa virusi vya Corona kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha nchini China.

  • 20 min
  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Maambukizi ya virusi vya Corona yaongezeka China, mauaji ya Beni yatisha, Uingereza yajiondoa rasmi EU

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Maambukizi ya virusi vya Corona yaongezeka China, mauaji ya Beni yatisha, Uingereza yajiondoa rasmi EU

  Katika makala hii, tumeangazia maambukizi ya virusi vya Corona nchini China kuendelea kuzua hofu kubwa huku ulimwengu ukihamasika katika kupambana navyo, huko DR Congo mauaji yaliendelea huku maafisa wa serikali wakiahidi kuimarisha usalama kuzuia mauaji yanayotekelezwa na waasi wa ADF. Kimataifa, Uingereza yajivua uanachama wake rasmi katika umoja wa ulaya, pia mchakato wa kumwondoa rais wa Marekani Donald Trump kushika kasi.

  • 21 min
  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Rais wa DRC Felix Tshisekedi aadhimisha mwaka mmoja madarakani, viongozi wa sudan kusini washindwa kuafikiana, virusi vya Corona vyaripotiwa China

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Rais wa DRC Felix Tshisekedi aadhimisha mwaka mmoja madarakani, viongozi wa sudan kusini washindwa kuafikiana, virusi vya Corona vyaripotiwa China

  Katika makala hii tumeangazia mwaka mmoja wa rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi madarakani lakini pia kauli yake ya kulivunja bunge la kitaifa, nchini Burundi wabunge waidhinisha muswada wa sheria unaopanga marupurupu ya rais atakayestaafu lakini pia faida zingine, suala la ulanguzi wa binadamu nchini Kenya, waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania ajiuzulu na mengine mengi katika uga wa kimataifa.

  • 20 min
  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Jeshi la Congo labomoa ngome ya ADF mashariki mwa DRC, waalimu wa Kenya kuondoka maeneo ya Garisa, Iran yatuhumu nchi za magharibi

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Jeshi la Congo labomoa ngome ya ADF mashariki mwa DRC, waalimu wa Kenya kuondoka maeneo ya Garisa, Iran yatuhumu nchi za magharibi

  Jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, juma hili lilifahamisha kuwa limedhibiti ngome muhimu ya Madina baada ya kuwatimua waasi wa ADF, huko Kenya waalimu watishia kuondoka katika eneo la Garissa kwa sababu za kiusalama, viongozi wa mataifa ya Sahel walikubaliana kuhusu kuimarisha mapambano dhidi ya magaidi, na huko Marekani mchakato wa kumuondoa madarakani rais Donald Trump washika kasi

  • 20 min
  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Shambulio la kambi ya kijeshi Lamu laua darzeni Kenya, DRC yafunga chuo kikuu Kinshasa, mvutano wa Iran na Marekani washika kasi

  Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii - Shambulio la kambi ya kijeshi Lamu laua darzeni Kenya, DRC yafunga chuo kikuu Kinshasa, mvutano wa Iran na Marekani washika kasi

  Katika makala ya wiki hii tumeangazia kuhusu shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa al-Shabaab dhidi ya kambi ya simba huko Lamu pwani ya Kenya, wiki hii serikali ya DR Congo kukifunga chuo kikuu cha Kinshasa kufwatia vurugu zilizojitokeza ambapo askari polisi mmoja aliuawa na mahusiano kati ya Rwanda na Uganda yaanza kuboreka, kimataifa mvutano kati ya Iran na Marekani washika kasi mpya

  • 20 min

Classement des podcasts dans Actualités

Plus par RFI Kiswahili