1m

UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    • Actus du jour

Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.
Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.
Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha.
"Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaji wa watu wengi, milipuko hatari, na kuongezeka kwa utapiamlo kumeupinda mfumo wa afya wa Haiti, lakini kunyongwa kwa minyororo ya usambazaji kunaweza kuwa ndio kunauvunja."
Makontena yaliyojazwa vifaa muhimu yamezuiliwa, au kuporwa, kama ilivyokuwa kwa maghala na maduka mengi ya dawa. Wakati huo huo, mamia ya makontena yaliyosheheni vifaa vya kibinadamu yamekwama huko Port-Au-Prince ikiwa ni pamoja na kontena za UNICEF zilizo na vifaa vya watoto wachanga, wajawazito na vya matibabu.
Port-Au-Prince, kitovu kikuu cha Haiti, kwa kawaida hupokea na kutuma mizigo ya uagizaji wa vifaa tiba vya Haiti. Sasa jiji hilo limelemazwa na vurugu, na wakazi wake zaidi ya 160,000 wameyakimbia makazi yao, jiji hilo haliwezi kutosheleza mahitaji ya watu ambao kwa wakati mmoja wanapambana na majeraha ya kimwili na hatari ya magonjwa, inafafanua taarifa ya UNICEF.
Mawimbi ya familia zilizofurushwa zinazotafuta usalama, hasa katika sehemu ya kusini mwa nchi, yanaleta shinikizo la ziada kwa huduma za afya za wanakokimbilia, ambazo hata kabla ya kuongezeka kwa mzozo hazikuweza kuhimili mahitaji. Uhaba wa wafanyakazi umeenea, na takriban asilimia 40 ya wafanyakazi wote wa matibabu wameondoka nchini Haiti kutokana na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama.
Kati ya Oktoba 2022 na Aprili 2024, Haiti iliripoti jumla ya visa 82,000 vinavyoshukiwa kuwa na kipindupindu. Takriban watu milioni 4.4 nchini Haiti wanahitaji msaada wa haraka wa chakula, na watu milioni 1.6 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya uhaba wa chakula, jambo ambalo linaongeza hatari ya kupata tatizo la uzito mdogo kwa watoto na utapiamlo. Kuwasili kwa msimu wa mvua kunatazamiwa kuzidisha hali kuwa mbaya zaidi, hivyo kusababisha ongezeko la visa vya magonjwa yatokanayo na maji pamoja na magonjwa yanayoenezwa na mbu, kama vile malaria.
Ili kukabiliana na hali hiyo, UNICEF na wadau wanatafuta njia mbadala za kuagiza na kusambaza mizigo. Kupitia njia za pili za uingizaji na utoaji, pamoja na Wizara ya Afya, wafadhili wa kimataifa na washirika, UNICEF imeweza kuendelea kupeleka chanjo, dawa na vifaa vya matibabu kwa watoto nchini Haiti ambao wanahitaji zaidi.
Tarehe 18, 20 na 21 Mei 2024, UNICEF iliwezesha kuwasilisha tani 38 za vifaa vya kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya na kipindupindu, na bidhaa nyingine muhimu za matibabu nchini Haiti kupitia njia ya anga kwa kuungwa mkono na Muungano wa Ulaya na WFP kutoka Panama hadi mji mkuu wa Haiti, ambapo UNICEF na Umoja wa Mataifa wameanzisha kituo kipya cha kufanya kazi. Lakini msaada zaidi unahitajika.
"Hatuwezi kuruhusu vifaa muhimu ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya watoto kubaki vikiwa vimezuiliwa kwenye maghala na makontena. Lazima viwasilishwe sasa,” amesisitiza Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti.

Plus par United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations