100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

    WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi

    Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.
    Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.
    Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.
    Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”
    Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwango cha mwaka 2012. 
    Ripoti hiyo ya 2024 pia imeainisha ni jinsi gani athari hizo zimehisiwa tofauti na hazilingani kote duniani.
    Maeneo ya WHO yaliyoathirika Zaidi ripoti inasema ni Ukanda wa Amerika na Kusini-Mashariki mwa Asia, ambako umri wa kuishi ukishuka kwa takriban miaka 3 na matarajio ya maisha yenye afya yakishuka kwa miaka 2.5 kati ya mwaka 2019 na 2021.
    Kinyume chake, Kanda za Pasifiki Magharibi zimeathiriwa kidogo wakati wa miaka miwili ya kwanza ya janga hla COVID-19 na kupata hasara ya chini ya miaka 0.1 katika umri wa kuishi na miaka 0.2 katika matarajio ya maisha yenye afya.

    • 2 min
    Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7

    Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7

    Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA)

    • 3 min
    FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania

    FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania

    Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu Mviwata FM ya Mkoani Morogoro amehudhuria Kikao hicho na kuandaa taaarifa hii. 

    • 3 min
    24 MEI 2024

    24 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na  mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? 
    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo. Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.Katika makaala zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika  Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA).Na mashina Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM inaendelea kutoa vifaa muhimu vya nyumbani na usafi pamoja na usaidizi wa pesa kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini Kenya, Mahmood Abdirahman, kuongozi wa jamii katika kaunti ya Garissa anasimulia changamoto zilizowakumba jamii hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 10 min
    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”

    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”

    • 1 min
    23 MEI 2024

    23 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”  
    Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba maelfu ya familia zinazokimbia Rafah zinajikuta zikiwa na uhaba wa chakula na maji safi.Mvua nyingi zaidi kuliko kawaida inatabiriwa katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika kuanzia mwezi Juni hadi Septemba mwaka huu. Maeneo yatakayotarajiwa kuwa na hali hiyo ni Djibouti, Eritrea, kaskazini na katikati mwa Ethiopia, magharibi na pwani ya Kenya, sehemu kubwa ya Uganda, Sudan Kusini, na Sudan.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 10 min

Top Podcasts In News

COCKTAILS AND TAKEAWAYS
cocktails and takeaways
Focus on Africa
BBC World Service
Global News Podcast
BBC World Service
AlhajiRadio
Alhaji Jadama
Newshour
BBC World Service
Africa Daily
BBC World Service

More by United Nations

The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations