100 集

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • 新聞

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka

    Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka

    Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali  ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki ambao walikuja katika jukwaaa hilo na azimio maalum linalohimiza mama kuvaa kofia yake ili kusaidia kutatua migogoro kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi kimataifa. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili akianza kwa kufafanua kuhusu azimio hilo 

    • 8 分鐘
    30 APRIL 2024

    30 APRIL 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.
    Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4.  Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii  hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,"Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linashirikisha wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira kupitia upandaji miti na kupitia video iliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus FM nampisha mwanaharakati wa mazingira ambaye alitembelea eneo Bunge la Ngong katika kaunti ya Kajiado  jijini Nairobi ili kushirikiana na wanafunzi katika kutimiza wito wa UNEP wa upanzi wa miti.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 12 分鐘
    Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund

    Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund

    Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.

    • 3 分鐘
    29 APRILI 2024

    29 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni? 
    Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi.  Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.Mashinani ikiwa ni wiki ya chanjo, kniniki tembezi inayofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imekuwa uti wa mgongo wa mfumo wa afya nchini Somalia na tunakutana na Jamila Moham, Mhudumu wa afya ya jamii katika kijiji cha Dhusamareeb.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 11 分鐘
    UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza

    UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza

    Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni. 
    Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.
    Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.
    UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.
    Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhimu kama maji ya kunywa ambapo wakimbizi wa ndani wanapokea chini ya lita moja ya maji kwa mtu kwa ajili ya kunywa, kufua na kuonga ikiwa ni tofauto kubwa na lita 151 ambacho ni kiwango cha chini wanachostahili kupata.
    Na jana Jumapili UNRWA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada w uteguzi wa mabomu UNMAS walianza operesheni muhimu ya kutathimini uharibifu katika vituo vya UNRWA kuweka alama kwa makombora yoyote na vifaa vyovyote ambavyo hvijalipuka.
    Mitambo 165 ya UNRWA huko Ukanda wa Gaza imeathiriwa wakati wa vita hii inayoendelea. 
    Na UNMAS inasema ili kuifanya Gaza kuwa salama dhidi ya vifaa vya milipuko ambayo haijalipuka inaweza kuchukua miaka 14.

    • 1 分鐘
    Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji

    Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji

    Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi 
    Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii. 
    Mbinu hii inayoendeshwa na wana jumuiya wenyewe inaweka kiwango kipya cha usaidizi wa kibinadamu nchini humo, kama anavyoeleza Mola Suleiman ambaye ni Mshiriki wa Msaada wa WFP anasema, "Wanaotambua wenye uhitaji zaidi sio viongozi, bali watu wasioegemea upande wowote waliochaguliwa na jamii. Tunaweza kwenda kwenye madawati ya usaidizi yaliyoanzishwa huko wilayani Kebeles na viunga vyake na kupeleka malalamiko yetu. Kwa kufuata utaratibu wa uwazi, tunakagua na kuthibitisha wale waliochaguliwa na jumuiya pana, kwakweli huu mfumo ni bora kuliko ule wa awali”
    Selam Ambachew ni mwanakamati aliyechaguliwa na jamii.
    "Kama jumuiya, tulichagua kamati, kisha kamati ikaanza tathmini yake, tunapokea orodha ya watu wote wanaoishi katika eneo hili, na tunachunguza orodha ili kuona ni nani anayefaa kwa vigezo vya usaidizi katika jamii"
    Tadel Gebeyehu ni mmoja wa wananchi walionufaika na mfumo huu mpya wa jamii yenyewe kuchagua wenye uhitaji zaidi wa Msaada wa kibinadamu, anasema "Tulipewa kadi za mgao na lazima tuzioneshe tunapokwenda kupokea chakula. Kadi hizi za mgawo ni muhimu kwa sababu zinazuia watu masikini kunyanyaswa"
    Ama hakika mwitikio wa kibinadamu nchini Ethiopia unazingatia uwazi, unaendeshwa kwa kuzingatia takwimu na kufikia wale wenye uhitaji zaidi, na hili linathibitishwa Haftom Gebretsadik mmoja wa wagawaji wa msaada.
    “Mchakato wa kugawa Msaada ni mzuri sana, kila nyanja ni nzuri sana, kinachofanya uwe ya kipekee ni heshima ya utu na ubinadamu. Mfumo ni wa uwazi, hakuna mkanganyiko wala wizi, kwa ujumla mchakato huo ni wa kupongezwa”. 

    • 2 分鐘

關於新聞的熱門 Podcast

Global News Podcast
BBC World Service
端聞 | 端傳媒新聞播客
端传媒音頻 | Initium Audio
Hong Kong Today
RTHK.HK
The Daily
The New York Times
晨早新聞天地
RTHK.HK
聚焦背後
集誌社 The Collective HK

United Nations的更多節目

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Interviews
United Nations
UN News - Global perspective Human stories
United Nations
The Lid is On
United Nations
ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations