1 min

TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    • Daily News

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon. 
Shughuli ya makabidhiano ya wakimbizi kutoka upande mmoja kwenda mwingine yamefanyika katika Wilaya ya Gamboula iliyoko mpakani mwa nchi hizo mbili mkoani Mambéré-Kadéï magharibi mwa CAR na yameshuhudiwa na wawakilishi wa masharika mbalimbali ya Umoja wa mataifa, vikosi vinavyohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini CAR, MINUSCA wakiwemo TANBAT 7 pamoja na majeshi ya Cameroon na CAR.
Kwa niaba ya ujumbe wa UNHCR kutoka kambi ya Batuli ya nchini Cameroon Mkuu wa kitengo cha Usalama wa wakimbizi wa Kambi hiyo Samwel Forterbel amesema kundi hili ni la wakimbizi ni wale walioamua kurudi nyumbani kwao kwa hiari yao wenyewe "baada ya hali ya Usalama kuimalika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na tukio hili lina maana kwamba wakivuka mpaka sio wakimbizi tena na hayo ni mafanikio makubwa."
Kwa upande wa Mkuu wa Msafara huo kutoka kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7, Kapteni Cosmas Mnyasenga amesema wamekamilisha kuwasafirisha salama waliokuwa wakimbizi hao na kuwafikisha salama nchini mwao, "katika makazi ya muda mjini Berberati." 
Mwaka 2013 nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na mya ndani ambapo makundi ya 3R, Anti Balaka na Seleka yalihitirafiana na kusababisha watu zaidi ya laki nne kuikimbia nchi hiyo na kwenda kuishi uhamishoni katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Chad na Cameroon na sasa baadhi wameanza kurejea nchini mwao na kuanza kulijenga taifa lao mara baada ya amani kuendelea kuimarika siku baada ya siku. 

More by United Nations

UN Interviews
United Nations
UN News - Global perspective Human stories
United Nations
The Lid is On
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations