Changu Chako, Chako Changu RFI Kiswahili
-
- 社会/文化
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
-
Historia na Utamaduni wa wanyakyusa na muziki wa Kidum pamoja na Esther Nish
Furaha ilioje kukutana nawe Jumapili ya leo katika Makala Changu chako Chako Changu, ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophpone na Muziki ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya makala kuhusu historia ya Wanyakyusa, na kwenye Miuziki nitakuletea mwanamuziki Esthernish pamoja ni Kidum. Mimi ni Ali Bilali bienvenue. Ama Karibu.
-
Sehemu ya makala kuhusu utamaduni wa waluo na waluhya hasa kwenye maswala ya ndoa
Karibu katika Makala haya changu chako chzako changu Jumapili ya leo ambapo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu tamaduni za wa Luhya na wa luo nchini Kenya ambapo sasa tutaangazia kuhusu tamadunbi za ndoa, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na kwenye muziki nitakuletea mwanamuziki Mbosso kutoka nchini Tanzania. Mimi ni Ali Bilali Karibu.
-
Utamaduni wa watu wa kabila la Waluo na Waluhya kutoka nchini Kenya
-
Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho
Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.
-
Sehemu ya tatu ya Makala kuhusu kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani
Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi
-
Kongamano la idhaa za kiswahili duniani, umuhimu wa kujifunza lugha ya Kiswahili
Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Msimamizi wa kituo cha radio China Kimataifa ambaye ni raia wa China kufahamu zaidi kwanini alivutiwa na swala la kujifunza lugha ya kiswahili, ni katika muktada wa kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania. Kwenye Muziki utasikiliza wimbo wa mwanamuziki Lupman mwenye asili ya Burundi anaefanya kazi yake huko Sweeden.