100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    UNICEF inasisitiza umuhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto

    UNICEF inasisitiza umuhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto

    Shirika la Umoja wa Mataifa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF inasisitiza mchango muhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto na afya yao ya akili. Makala hii inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.

    • 4 min
    Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika

    Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika

    Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika.
    Amesema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi huyu wa WHO kanda ya Afrika katika ukurasa wake wa X, kwenye ujumbe wake wa siku ya leo ya uchangiaji damu duniani, maudhui yakiwa Miaka 20 ya kuchangia: Asanteni Wachangiaji wa damu.
    Anashukuru wachangiaji wote wa damu barani Afrika. Akisema wanaokoa maisha. Na zaidi ya yote anapenda kuwahamasisha wawe wachangiaji wa damu mara kwa mara.
    “Nimekutana na mabingwa kadhaa ambao wamekuwa wakichangia damu kwa muongo mmoja au zaidi. Hili ni jambo ambalo tunafanya mara moja kwa mwaka pindi tunaposherehekea siku hii kama leo, lakini kwa kawaida mara tatu au mara nne kwa mwaka.”
    Lakini ni nini kinahitajika?
    “Tunahitaji kuhamasisha watu kujitolea zaidi kuchangia damu barani Afrika. Hali inazidi kuimarika lakini bado safari ni ndefu.”
    Kulikoni safari ni ndefu?
    Kwa sababu tunahitaji kuongeza maradufu uchangiaji wa damu angalau Afrika. Kwa sasa kiwango chetu ni Uniti 5 za damu kwa watu 100. Tunahitaji angalau uniti 10 kwa watu 1000. Kwa hiyo jitokezeni mara kwa mara.”
    Akaelekeza wito kwa kundi mahsusi..
    “Njooni kila mwaka. Hebu tuwahusishe vijana na tuweze kuimarisha hali ya afya kwa wakazi wa Afrika.”
    WHO inasema damu salama inaokoa maisha na uchangiaji wa damu mara kwa mara kutoka kwa watu wenye afya kunahitajika ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote pale inapohitajika. 

    • 1 min
    14 JUNI 2024

    14 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Utoaji Damu Duniani na umuhimu wake, na wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ufilipino, kulikoni?
    Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.Mashinani tunasalia kwa hii ya Utoaji Damu Duniani, na tutaelekea jijini manila ufilipino amabapo wafanya kazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani wanaongoza mstari wa mbele kwa kutoa damu wakitueleza umuhimu shughuli hii”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 10 min
    TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR

    TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon. 
    Shughuli ya makabidhiano ya wakimbizi kutoka upande mmoja kwenda mwingine yamefanyika katika Wilaya ya Gamboula iliyoko mpakani mwa nchi hizo mbili mkoani Mambéré-Kadéï magharibi mwa CAR na yameshuhudiwa na wawakilishi wa masharika mbalimbali ya Umoja wa mataifa, vikosi vinavyohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini CAR, MINUSCA wakiwemo TANBAT 7 pamoja na majeshi ya Cameroon na CAR.
    Kwa niaba ya ujumbe wa UNHCR kutoka kambi ya Batuli ya nchini Cameroon Mkuu wa kitengo cha Usalama wa wakimbizi wa Kambi hiyo Samwel Forterbel amesema kundi hili ni la wakimbizi ni wale walioamua kurudi nyumbani kwao kwa hiari yao wenyewe "baada ya hali ya Usalama kuimalika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na tukio hili lina maana kwamba wakivuka mpaka sio wakimbizi tena na hayo ni mafanikio makubwa."
    Kwa upande wa Mkuu wa Msafara huo kutoka kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7, Kapteni Cosmas Mnyasenga amesema wamekamilisha kuwasafirisha salama waliokuwa wakimbizi hao na kuwafikisha salama nchini mwao, "katika makazi ya muda mjini Berberati." 
    Mwaka 2013 nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na mya ndani ambapo makundi ya 3R, Anti Balaka na Seleka yalihitirafiana na kusababisha watu zaidi ya laki nne kuikimbia nchi hiyo na kwenda kuishi uhamishoni katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Chad na Cameroon na sasa baadhi wameanza kurejea nchini mwao na kuanza kulijenga taifa lao mara baada ya amani kuendelea kuimarika siku baada ya siku. 

    • 1 min
    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa neno "Kotokoto"

    Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa neno "Kotokoto"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO.”

    13 JUNI 2024

    13 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uvuvi endelevu kwa kutumia kanuni za uvuvi na tunafuatilia mtazamo wa wakazi wa eneo la ziwa Taganyika kuhusu kufungwa zia hilo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za watoto katika migogoro, Ualbino na COSP17. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “Kotokoto.”
    Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu viwango vya ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo ya mizozo yenye matumizi ya silaha inaonesha kuwa mwaka 2023 kulikuwa na ukatili wa kupindukia. Ripoti hiyo inayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kila mwaka inasema “Mwaka wa 2023 watoto waliandikishwa na kutumika vitani ikiwa ni pamoja na kwenye mstari wa mbele, kushambuliwa majumbani mwao, kutekwa nyara wakielekea shuleni, shule zao zikitumiwa kijeshi, madaktari wao wakilengwa, na orodha ya kutisha inaendelea. Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu kufurahia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, Muluka-Anne Miti-Drummond amepongeza maendeleo ya pamoja yaliyopatikana katika kufuatilia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipotambua rasmi tarehe 13 Juni kuwa Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino miaka kumi iliyopita. Hata hivyo, amesema wanatambua kwamba safari ya kuelekea katika  ulimwengu wa haki sawa kwa watu wenye ualbino bado inakumbwa na changamoto na ugumu mkubwa.Na leo ndio ndio tamati ya Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, COSP17 uliodumu kwa siku tatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Sarah Muthoni Kamau, Mwenyekiti wa Jukwaa la Watu wenye ulemavu la Jumuiya ya Madola ni mmoja wa waliohudhuria mkutano huu uliodumu kwa siku tatu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 9 min

Top Podcasts In News

Global News Podcast
BBC World Service
Focus on Africa
BBC World Service
Candace
Candace Owens
The Daily
The New York Times
Economist Podcasts
The Economist
COCKTAILS AND TAKEAWAYS
cocktails and takeaways

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Interviews
United Nations
The Lid is On
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations