Jua Haki Zako RFI Kiswahili
-
- Government
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
-
Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii
Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica.
Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au wale huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi. -
DRC : Makundi ya waasi yatuhumiwa kwa ukatili wa kijinsia dhidi ya raia mbilimo
Nchini DRC ; familia ya jamii ya mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu.
-
Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?
Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume.
-
Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023
Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi.
-
Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu
Unamkumbuka kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.
-
Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi.