100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Kauli za chuki zinasababisha mauaji ya kimbari - Alice Wairimu Nderitu

    Kauli za chuki zinasababisha mauaji ya kimbari - Alice Wairimu Nderitu

    Leo siku ya kimataifa ya kupinga kauli za chuki ikiadhimishwa ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Nguvu ya Vijana ya Kupinga na Kushughulikia Kauli za Chuki”, Dunia bado iko katika kumbukumbu za maombolezo ya siku 100 za mauaji ya Kimbari ya Rwanda yaliyofanyika miaka 30 iliyopita, ambapo kauli za chuki zimeelezwa kuwa moja ya chachu kubwa ya mauaji hayo. Flora Nducha wa Idhaa hii ameketi na Alice Wairimu Nderitu mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbali kujadili kuhusu mchango wa kauli za chuki katika zahma duniani, jukumu la vijana na nini kifanye kuzitokomeza. Na Bi. Nderitu anaanza kwa kufafanua je dunia inaelewa kuhusu mchango wa kauli hizo za chuki katika mauaji ya kimbari.

    • 7 min
    18 JUNI 2024

    18 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikimulika nguvu ya Vijana ya Kupinga na Kushughulikia Kauli za Chuki. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani inayoangazia michango mikubwa ya kiuchumi ya utumaji fedha kutoka ughaibuni.
    Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk hii leo katika Taarifa yake kupitia katika kikao cha 56 cha Baraza la Haki za Kibinadamu kilichoanza leo Juni 18 mjini Geneva, Uswisi,  ameelezea wasiwasi wake juu ya athari mbaya za migogoro ya kimataifa inayoendelea kwa raia, akibainisha ongezeko la asilimia 72 la vifo vya raia kwa mwaka jana 2023. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Kauli za Chuki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyaeleza mataifa ulimweguni kote kwamba yana wajibu chini ya sheria ya kimataifa kuzuia na kupambana na uchochezi wa chuki na badala yake kuhamasisha kutambua tofauti, kukuza maelewano na mshikamano.Utafiti mkubwa kuhusu mitazamo ya watu kwa wakimbizi kote Kaskazini na Kusini mwa Ulimwengu unaonesha kwamba ingawa uungaji mkono wa upokeaji wakimbizi umepungua katika baadhi ya nchi hasa baada ya uvamizi wa Urusi kwa Ukraine lakini robo tatu ya watu wazima ulimwenguni wanaendelea kuamini kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kutafuta usalama katika nchi nyingine.Na mashinani mashinani, hivi majuzi katika siku ya kimataifa ya utumaji fedha kutoka ughaibuni, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ulisisitiza nafasi ya fedha hizo katika kuokoa maisha kwa mamia ya mamilioni ya watu, nusu yao walioko  maeneo ya vijijini, kauli ambayo inapata pongezi na shukrani kutoka kwa Dkt. Shea Mochodo, Mkuu wa Muungano wa raia wa Kenya wanaoishi ughaibuni.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 12 min
    UNICEF inasisitiza umuhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto

    UNICEF inasisitiza umuhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto

    Shirika la Umoja wa Mataifa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF inasisitiza mchango muhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto na afya yao ya akili. Makala hii inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.

    • 4 min
    Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika

    Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika

    Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika.
    Amesema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi huyu wa WHO kanda ya Afrika katika ukurasa wake wa X, kwenye ujumbe wake wa siku ya leo ya uchangiaji damu duniani, maudhui yakiwa Miaka 20 ya kuchangia: Asanteni Wachangiaji wa damu.
    Anashukuru wachangiaji wote wa damu barani Afrika. Akisema wanaokoa maisha. Na zaidi ya yote anapenda kuwahamasisha wawe wachangiaji wa damu mara kwa mara.
    “Nimekutana na mabingwa kadhaa ambao wamekuwa wakichangia damu kwa muongo mmoja au zaidi. Hili ni jambo ambalo tunafanya mara moja kwa mwaka pindi tunaposherehekea siku hii kama leo, lakini kwa kawaida mara tatu au mara nne kwa mwaka.”
    Lakini ni nini kinahitajika?
    “Tunahitaji kuhamasisha watu kujitolea zaidi kuchangia damu barani Afrika. Hali inazidi kuimarika lakini bado safari ni ndefu.”
    Kulikoni safari ni ndefu?
    Kwa sababu tunahitaji kuongeza maradufu uchangiaji wa damu angalau Afrika. Kwa sasa kiwango chetu ni Uniti 5 za damu kwa watu 100. Tunahitaji angalau uniti 10 kwa watu 1000. Kwa hiyo jitokezeni mara kwa mara.”
    Akaelekeza wito kwa kundi mahsusi..
    “Njooni kila mwaka. Hebu tuwahusishe vijana na tuweze kuimarisha hali ya afya kwa wakazi wa Afrika.”
    WHO inasema damu salama inaokoa maisha na uchangiaji wa damu mara kwa mara kutoka kwa watu wenye afya kunahitajika ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote pale inapohitajika. 

    • 1 min
    14 JUNI 2024

    14 JUNI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Utoaji Damu Duniani na umuhimu wake, na wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ufilipino, kulikoni?
    Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.Mashinani tunasalia kwa hii ya Utoaji Damu Duniani, na tutaelekea jijini manila ufilipino amabapo wafanya kazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani wanaongoza mstari wa mbele kwa kutoa damu wakitueleza umuhimu shughuli hii”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 10 min
    TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR

    TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon. 
    Shughuli ya makabidhiano ya wakimbizi kutoka upande mmoja kwenda mwingine yamefanyika katika Wilaya ya Gamboula iliyoko mpakani mwa nchi hizo mbili mkoani Mambéré-Kadéï magharibi mwa CAR na yameshuhudiwa na wawakilishi wa masharika mbalimbali ya Umoja wa mataifa, vikosi vinavyohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini CAR, MINUSCA wakiwemo TANBAT 7 pamoja na majeshi ya Cameroon na CAR.
    Kwa niaba ya ujumbe wa UNHCR kutoka kambi ya Batuli ya nchini Cameroon Mkuu wa kitengo cha Usalama wa wakimbizi wa Kambi hiyo Samwel Forterbel amesema kundi hili ni la wakimbizi ni wale walioamua kurudi nyumbani kwao kwa hiari yao wenyewe "baada ya hali ya Usalama kuimalika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na tukio hili lina maana kwamba wakivuka mpaka sio wakimbizi tena na hayo ni mafanikio makubwa."
    Kwa upande wa Mkuu wa Msafara huo kutoka kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7, Kapteni Cosmas Mnyasenga amesema wamekamilisha kuwasafirisha salama waliokuwa wakimbizi hao na kuwafikisha salama nchini mwao, "katika makazi ya muda mjini Berberati." 
    Mwaka 2013 nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na mya ndani ambapo makundi ya 3R, Anti Balaka na Seleka yalihitirafiana na kusababisha watu zaidi ya laki nne kuikimbia nchi hiyo na kwenda kuishi uhamishoni katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Chad na Cameroon na sasa baadhi wameanza kurejea nchini mwao na kuanza kulijenga taifa lao mara baada ya amani kuendelea kuimarika siku baada ya siku. 

    • 1 min

Top Podcasts In News

ဘီဘီစီမြန်မာပိုင်း ညနေခင်းသတင်းအစီအစဉ်
BBC Burmese Radio
နံနက်ပိုင်း ၆း၀၀-၇း၀၀ - ဗွီအိုအေ
ဗွီအိုအေ
အာရ်အက်ဖ်အေ နေ့စဉ် အသံလွှင့် အစီအစဉ်
RFA
The Irrawaddy Newscast - Burmese Edition
The Irrawaddy
ညပိုင်း ၉း၀၀-၁၀း၀၀ - ဗွီအိုအေ
ဗွီအိုအေ
စိုပြေ မပြောချင်ဘူး
RFA

More by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations