100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..

    • 2 min
    29 MEI 2024

    29 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.
    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Makala inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Na mashinani tutaelekea Gambella nchini Ethiopia  kusikia ni kwa jinsi gani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF linahakikisha kuwa wasichana hawakosi masomo yao kwa kukosa sodo au taulo za kike wakati wa hedhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

    • 9 min
    Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa

    Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa

    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. 
    Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya 76,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanadumisha lengo bora zaidi la ubinadamu, amani. Siku baada ya siku, wakihatarisha Maisha yao, wanawake na wanaume hawa wanafanya kazi kwa ujasiri katika baadhi ya maeneo hatari na yasiyo na utulivu duniani ili kulinda raia, kudumisha haki za binadamu, kumsaidia masuala ya uchaguzi na kuimarisha taasisi. Zaidi ya walinda amani 4,300 wamelipa gharama ya Maisha yao wakati wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Hatutawasahau kamwe.”
    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maudhui ya siku ya mwaka huu yanaashiria kwamba wakati ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umethibitika kuwa sehemu ya suluhu kwa zaidi ya miaka 75 ukizisaidia nchi mwenyeji kuvuka mapito kutoka kwenye migogoro hadi amani muhtasari wa Sera wa Katibu Mkuu wa Ajenda mpya ya amani unaweka njia ya operesheni za kimataifa za amani na usalama mbele ili kusalia kuwa zana zinazofaa kushughulikia vita na migogoro ijayo.
    Naye mkuu wa operesheni za Umoja wa Mataifa za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix,akiongeza sauti yake katika siku hii amesema "Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unasalia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa, huku walinda amani kutoka zaidi ya nchi 120 wakifanya mabadiliko yenye tija kila siku kwa mamilioni ya watu katika baadhi ya maeneo magumu zaidi duniani. Tunapokabiliana na changamoto za kesho, ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unaendelea kubadilika, na kuhimiza ushirikiano kuwa mahiri, msikivu na unaofaa kwa madhumuni yaliyokusudiwa, kukuza utulivu, kulinda walio hatarini na kusaidia kujenga amani ya kudumu."
    Siku ya Kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kila mwaka Mei 29 na ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2002 ili kuwaenzi wanaume na wanawake wote katika operesheni za ulinzi wa amani na kuenzi kumbukumbu ya wale wote waliopoteza Maisha yao kwa lengo la kuleta amani.

    • 2 min
    Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo

    Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo

    Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.
    Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop ambaye anatamatisha jukumu lake anasema angalau kwa sasa kuna jawabu la ulinzi wa amani ambalo licha ya changamoto zake linaleta nuru.
    “Na ulinzi wa amani umethibitisha kuwa unaweza kutatua baadhi ya mizozo. Ninaweza kukupatia mfano wa Timor-Letse [TIMORLETSI]. Ninaweza kukupa mifano ya Côte d'Ivoire, ya Sierra Leone, ya Liberia, ambako ulinzi wa amani umesaidia kurejesha amani na utulivu. Na sasa nchi hizi hata zinashiriki kwenye ulinzi wa amani.”
    Ingawa ulinzi wa amani unazaa matunda, kwa Jenerali Diop ambaye anatoka Senegal, jambo muhimu ni kuzidi kuboresha huduma hiyo kwani itaendelea kuwa muhimu huku Umoja wa Mataifa ukihakikisha ujumbe wa ulinzi wa amani unapatiwa mamlaka na majukumu sahihi ili kukidhi mantiki ya uwepo wake. Na zaidi ya yote.
    “Tunatakiwa pia leo hii kuambatanisha ujumbe wa ulinzi wa amani na mfumo wa kimkakati wa mawasiliano ili kuzuia habari potofu na habari za uongo zinazoharibu kila kitu tunachofanya. Ulinzi wa amani hautafanikiwa iwapo nchi mwenyeji haiungi mkono ujumbe wa ulinzi wa amani.”

    • 1 min
    28 MEI 2024

    28 MEI 2024

    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
    -Watu zaidi ya 2000 wahofiwa kufunikwa na maporomoko ya udongo Papua New Guinea , Umoja wa Mataifa wasaidia
    -Ripoti ya UNRWA inasema wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na dharura ya kiafya isiyokuwa na mfano wake iliyosababishwa na vita mbaya zaidi katika historia ya Gaza
    - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  ameuambia Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS4) Antigua na Barbuda kwamba ulimwengu unahitaji kuchukua hatua ili kusaidia vyema na kuhamasisha ufadhili kwa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS) 
    -Katika kuelekea siku ya walindamani hapo kesho leo kikosi cha Tanzania TANZBAT11 nchini DRC chashikamana na wananchi katika miradi mbalimbali
    -Na mashinani utamsikia mlindamani kutoka Italia anayehudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL

    • 10 min
    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza

    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza

    Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.
    Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:
    1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo yake ya tarehe 26 Januari 202 na 28 Machi 2024, ambayo yanapaswa kutekelezwa mara moja na kwa ufanisi
    2. Imeainisha hatua zifuatazo za muda kwamba : Taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la Rafah
    Isitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi, na hatua nyingine yoyote katika jimbo la Rafah ambayo yanaweza kusababishia kundi la Wapalestina Gaza hali hiyo ya maisha inayoweza kuleta uharibifu wa kimwili kwa ujumla au sehemu;Iendeleel kukiacha wazi kivuko cha Rafah  kwa utoaji usiozuiliwa kwa kiwango cha haraka cha huduma za msingi zinahitajika na msaada wa kibinadamu;Kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa Ukanda wa Gaza kwa tume yoyote ya uchunguzi, ujumbe wa kutafuta ukweli au chombo kingine cha uchunguzi kilichoagizwa na vyombo vyenye uwezo wa Umoja wa Mataifa kuchunguza tuhuma za mauaji ya kimbari;3. Mahakama imeamua kwamba Israeli itawasilisha ripoti kwa Mahakama juu ya hatua zote kuchukuliwa ili kutekeleza agizo hili, ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya agizo hili.

    • 1 min

Top Podcasts In News

Global News Podcast
BBC World Service
China voorbij de muur
VRT NWS
FT News Briefing
Financial Times
Stay Free with Russell Brand
Russell Brand
The Economics Show with Soumaya Keynes
Financial Times
Reuters World News
Reuters

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations