In Her Shoes With Getrude Shussa Getrude Shussa
-
- Education
Ninawasaidia #singlemomtz kutambua thamani yao, malezi, mahusiano na upambanaji kwa ajili ya maisha yao bila kujisikia upweke kwa kuwa wao ni single mom
-
Unawezaje Kumsahau Baba wa mtoto wako?
Jamaniii kuzaa naye haimaniishi mpaka kifo kiwatenganishe, haimaniishi ni lazima muishi pamoja kitu unachotakiwa kujua ni kuwa "Mapenzi huisha" lakini mtoto ataendelea kuwepo na atawaunganisha kwa namna moja ama nyingine.
Unamuona hafai kwako kwasababu mapenzi yameisha kati yenu lakini anaweza kuwa baba bora sana kwa mwanao.
Tatizo linakuja pale ambapo hutaki kukubali kuwa wewe na yeye hamuwezi tena kuwa pamoja unazidi kuumia siku hadi siku na unashindwa kumove on na maisha yako mengine. Kwenye episode hii utapata kujua dondoo chache ambazo zitakusaidia wewe kumove on na maisha yako. -
Ijue nguvu ya msamaha
Wewe ni miongoni mwa wale watu ambao hawawezi kusamehe hata iwejeđbasi uko sehemu sahihi kwani kupitia podcast hii utaweza kuijua nguvu ya msamaha na utaona ni kwa namna gani msamaha ni muhimu kwako kiasi gani. Najua sio kazi rahisi kusamehe na kusahau au kusamehe lakini ukiamua kutoka moyoni mwako hakuna kitakachoshindikana. Ungana nami mwanzo mpaka mwisho usisahau na kuwashirikisha watu wengine.