100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI” 

    30 MEI 2024

    30 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.
    Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kwamba dalili zote zinaonesha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe kwa watoto na wanawake katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita. Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika hayo matatu la Kuhudumia Watoto (UNICEF), la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la afya ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa wito wa usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kwasababu hali inazidi kuwa tete kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema hakuna mengi ambayo linaweza kufanya kwa sasa huko Rafah kwani akiba ya chakula ni ndogo na kuna vikwazo vingi kuwafikia watu.Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa Akili Mnemba umeanza leo Mei 30 mjini Geneva, Uswisi kujadili matumizi bora ya Akili Mnemba (AI) ili kuharakisha kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na unaunganisha wabunifu wa Akili Mnemba na watoa uamuzi wa sekta ya umma na binafsi ili kusaidia kuongeza ufumbuzi unaotokana na akili Mnemba kote duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 11 min
    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..

    • 2 min
    29 MEI 2024

    29 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.
    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Makala inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Na mashinani tutaelekea Gambella nchini Ethiopia  kusikia ni kwa jinsi gani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF linahakikisha kuwa wasichana hawakosi masomo yao kwa kukosa sodo au taulo za kike wakati wa hedhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

    • 9 min
    Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa

    Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa

    Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee  wa kimataifa. 
    Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya 76,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanadumisha lengo bora zaidi la ubinadamu, amani. Siku baada ya siku, wakihatarisha Maisha yao, wanawake na wanaume hawa wanafanya kazi kwa ujasiri katika baadhi ya maeneo hatari na yasiyo na utulivu duniani ili kulinda raia, kudumisha haki za binadamu, kumsaidia masuala ya uchaguzi na kuimarisha taasisi. Zaidi ya walinda amani 4,300 wamelipa gharama ya Maisha yao wakati wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Hatutawasahau kamwe.”
    Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maudhui ya siku ya mwaka huu yanaashiria kwamba wakati ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umethibitika kuwa sehemu ya suluhu kwa zaidi ya miaka 75 ukizisaidia nchi mwenyeji kuvuka mapito kutoka kwenye migogoro hadi amani muhtasari wa Sera wa Katibu Mkuu wa Ajenda mpya ya amani unaweka njia ya operesheni za kimataifa za amani na usalama mbele ili kusalia kuwa zana zinazofaa kushughulikia vita na migogoro ijayo.
    Naye mkuu wa operesheni za Umoja wa Mataifa za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix,akiongeza sauti yake katika siku hii amesema "Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unasalia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa, huku walinda amani kutoka zaidi ya nchi 120 wakifanya mabadiliko yenye tija kila siku kwa mamilioni ya watu katika baadhi ya maeneo magumu zaidi duniani. Tunapokabiliana na changamoto za kesho, ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unaendelea kubadilika, na kuhimiza ushirikiano kuwa mahiri, msikivu na unaofaa kwa madhumuni yaliyokusudiwa, kukuza utulivu, kulinda walio hatarini na kusaidia kujenga amani ya kudumu."
    Siku ya Kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kila mwaka Mei 29 na ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2002 ili kuwaenzi wanaume na wanawake wote katika operesheni za ulinzi wa amani na kuenzi kumbukumbu ya wale wote waliopoteza Maisha yao kwa lengo la kuleta amani.

    • 2 min
    Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo

    Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo

    Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.
    Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop ambaye anatamatisha jukumu lake anasema angalau kwa sasa kuna jawabu la ulinzi wa amani ambalo licha ya changamoto zake linaleta nuru.
    “Na ulinzi wa amani umethibitisha kuwa unaweza kutatua baadhi ya mizozo. Ninaweza kukupatia mfano wa Timor-Letse [TIMORLETSI]. Ninaweza kukupa mifano ya Côte d'Ivoire, ya Sierra Leone, ya Liberia, ambako ulinzi wa amani umesaidia kurejesha amani na utulivu. Na sasa nchi hizi hata zinashiriki kwenye ulinzi wa amani.”
    Ingawa ulinzi wa amani unazaa matunda, kwa Jenerali Diop ambaye anatoka Senegal, jambo muhimu ni kuzidi kuboresha huduma hiyo kwani itaendelea kuwa muhimu huku Umoja wa Mataifa ukihakikisha ujumbe wa ulinzi wa amani unapatiwa mamlaka na majukumu sahihi ili kukidhi mantiki ya uwepo wake. Na zaidi ya yote.
    “Tunatakiwa pia leo hii kuambatanisha ujumbe wa ulinzi wa amani na mfumo wa kimkakati wa mawasiliano ili kuzuia habari potofu na habari za uongo zinazoharibu kila kitu tunachofanya. Ulinzi wa amani hautafanikiwa iwapo nchi mwenyeji haiungi mkono ujumbe wa ulinzi wa amani.”

    • 1 min

Top Podcasts In News

COCKTAILS AND TAKEAWAYS
cocktails and takeaways
Global News Podcast
BBC World Service
The Global Story
BBC World Service
Al Jazeera News Updates
Al Jazeera
Law&Crime Sidebar
Law&Crime
1Twente Vandaag Uitgelicht
1Twente

More by United Nations

The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations