100 episodios

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • Noticias

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya

    UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya

    Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.
    Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu.
    "Wanafunzi wetu mara nyingi hupata ujifunzaji wao kupitia hisia ya kuona, kwa sababu usikivu wao hauwafai sana. Kwa hivyo, UNICEF kuunganisha shule kwenye intaneti kumesaidia sana hasa katika kuboresha ufundishaji wetu. Watoto wetu wanaweza kujifunza na hasa kujifunza kupitia njia ya kuona wanaweza kupata maarifa kwa njia bora zaidi.”
    Mwalimu Terika Gevera anafafanua zaidi akisema,
    "Intaneti ni sehemu muhimu sana katika kujifunza. Tuliamunganishwa katika nyenzo za E-Kitabu. E-Kitabu wamejaribu kuandika hadithi zao kwa lugha ya ishara, hivyo wanafunzi hutazama picha, huangalia ishara na mwisho wa kila hadithi, wanafunzi huulizwa maswali kuhusu hadithi ambayo imesimuliwa kwa ishara. Kupitia hilo wanafunzi wamefahamu kuwa wanaweza kusoma hadithi, kuelewa na kujibu maswali.”

    • 1m
    31 MEI 2024

    31 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?
    Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai ya kuwajibika na mauaji hayo kutoka pande zote, makundi yenye silaha na serikali. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Makala inaturejesha Bahrain kufuatilia usimamizi wa Akili Mnemba wakati huu ambapo huko Geneva, wabobezi wa Akili Mnemba na wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi wakibonga bongo kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia hiyo, Assumpta Massoi amezungumza na mwanazuoni kutoka Malaysia kandoni mwa jukwaa la Umoja wa Mataifa la Uwekezaji kwa wajasiriamali lililomalizika hivi karibuni huko Manama.Na katika mashinani tutasalia nchini Kenya kaunti ya Garissa ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM linaendelea kutoa msaada kwa maelfu ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    • 9 min
    Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome

    Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome

    Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. 
    Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemba 2023 na Aprili mwaka huu 2024 imepokea madai ya ukiukwaji wa haki na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu ukiwaathiri takriban watu 2732 hili likiwa ni ongezeko la asilimia 71 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.
    Taarifa inasema watu 1794 ay asilimia 65 miongoni mwa watu hao ni waathirika wa mauaji ya kinyume cha sheria.
    Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema Makundi yenye silaha, kama vile Jamāʿat nuṣrat al-islām wal-muslimīn, Kundi kubwa la Kiislamu katika Jangwa la Sahara na makundi mengine yanayofanana na hayo, yamezidisha mashambulizi yao dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na dhidi ya wakimbizi wa ndani. 
    Kwa mujibu wa Bwana Türk "Wakati makundi yenye silaha yanadaiwa kuhusika na idadi kubwa ya matukio na waathirika, na yanapaswa kuwajibika, pia ninasikitishwa sana kwamba vikosi vya usalama na ulinzi na wasaidizi wao ambao ni watu waliojitolea kwa ulinzi wan chi yao wanadaiwa kutekeleza mauaji ya kiholela, ikiwa ni pamoja na kunyongwa,”
    Awali mkuu huyo wa haki za binadamu alizungumzia masuala haya na Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso, wakati wa ziara yake nchini humo Machi mwaka huu.
    Türk ameongeza kuwa "Ninatambua kikamilifu vitisho tata vya usalama ambavyo Burkina Faso inakabiliana nayo. Jawabu dhidi ya vitisho hivi litafaulu tu ikiwa sheria za kimataifa zitaheshimiwa kikamilifu kote nchini. Kwa hivyo narudia wito wangu kwa mamlaka nchini Burkina Faso kuchukua hatua zote zinazowezekana ili kuhakikisha ulinzi wa raia,” 
    Kamishna Mkuu ametoa wito kwa Serikali ya Burkina Faso kuunga mkono uchunguzi wa kina, huru na wa uwazi kuhusu tuhuma zote za ukiukaji wa haki na ukiukwaji wa sheria za kimataifa, na kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa mahakamani, katika kesi zinazokidhi viwango vya kimataifa, ili kuhakikisha haki ya kweli kwa waathirika na fidia.
    Amesisitiza kwamba ni “Lazima kuweka na haki na uwajibikaji endapo mamlaka inataka kweli kuihakikishia jamii inarejesha mshikamano wa kijamii na kujenga upya uaminifu kati ya raia na vikosi vya usalama." 

    • 1m
    Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili  leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI” 

    30 MEI 2024

    30 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.
    Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kwamba dalili zote zinaonesha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe kwa watoto na wanawake katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita. Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika hayo matatu la Kuhudumia Watoto (UNICEF), la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la afya ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa wito wa usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kwasababu hali inazidi kuwa tete kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema hakuna mengi ambayo linaweza kufanya kwa sasa huko Rafah kwani akiba ya chakula ni ndogo na kuna vikwazo vingi kuwafikia watu.Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa Akili Mnemba umeanza leo Mei 30 mjini Geneva, Uswisi kujadili matumizi bora ya Akili Mnemba (AI) ili kuharakisha kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na unaunganisha wabunifu wa Akili Mnemba na watoa uamuzi wa sekta ya umma na binafsi ili kusaidia kuongeza ufumbuzi unaotokana na akili Mnemba kote duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 11 min
    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan

    Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..

    • 2 min

Top podcasts en Noticias

El Faro Audio
El Faro
La Tribu FM
Pencho Duque
CNN 5 Cosas
CNN en Español
mixx.io
Álex Barredo
Las noticias en Onda Cero
OndaCero
El hilo
Radio Ambulante Estudios

Más de United Nations

Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations