SE6EP10 - Salama Na Madam Rita | SOMETHING SPECIAL Salama Na

    • Entertainment News

Listen on Apple Podcasts
Requires subscription and macOS 11.4 or higher

Ms Rita Sundi Paulsen Hans ni mtu muhimu kwangu na kwa mamia kama pengine si maelfu ya wenzangu hapa nyumbani Tanzania. Yeye ni Mama kwanza, Dada kwa wengine, Aunt poa sana kwa kina Malik na Jamal, Bosi ya Mboka kwa Salama na wenzie lakini kubwa kabisa ni MJASIRIAMALI, jambo ambalo amekua akilisimamia lile analo liamini kwa miaka zaidi ya 30 sasa. Rita au Madam Rita alianza kufanya kazi toka alipokua na miaka yake ya mwanzo kabisa ya 20.

Mtoto kutoka kwenye familia ya kitajiri maana Marehemu Mzee Paulsen hakua mnyonge. Baba Mjerumani na Mama Mwenye asili ya kisukuma, kirudi na mchanganyiko wa makabila mengine kadhaa ambayo atatuambia humu ndani. Amekulia kwenye mitihani mingi mara baada ya Baba yake kufariki wakati yeye ana miaka 12 tu. Kutoka kwenye mazoea ya maisha ya kishua mpaka kupata mimba akiwa na umri mdogo na hilo kumlazimisha yeye kuondoka nyumbani akiwa na umri mdogo ndo mi naamini lililomfanya awe CHUMA mpaka leo. Naamini vile wanavyosema kila mtu na njia zake. Kila kitu kinachotokea kwenye maisha yetu kina sababu yake. Yeye kufariki kwa Baba yake ndo kulipelekea kupita KOTE alipopita. Shida na mitihani wakati mwengine huja kwa baraka tele, BARAKA ambazo mpaka leo hii ambayo mimi naandika waraka huu kwa majivuno mengi juu yake. Kweli kila kitu hutokea kwa sababu ili kitu kengine kizuri zaidi kiweze kukufuata ulipo.

Mimi na yeye tulifahamiana kwaajili ya kazi, nadhani wengi wanaijua hiyo khadhithi, ila kama hufahamu mimi na yeye makutano yetu ya kwanza yalikua ya kunipa kazi ya ku host Kili Music Awards ila hiyo kazi ilikuja baada ya pinduapindua nyingi alizo zifanya pale EATV baada ya siku moja mimi kuisema vibaya moja ya video ambazo kampuni yake ya Benchmark ilizitengeneza. Ilikua mtihani haswa baada ya kuskia naitwa tena ofisini kwake? Haya jengine lipi tena? Kumbe round hii ilikua kwa Neema sana, ila Bahati mbaya hiyo kazi wala sikuipata maana na watu wa Kili nao walinikataa kwasababu huko nyuma pia niliwasemea tuzo zao ambazo ki ukweli zilikua za kiwango CHA CHINI MNO considering hela ambazo wanazo wao kama KAMPUNI, kwa kweli lile halikua linapaswa kunyamaziwa.

Basi, peleka mbele mwaka mmoja au miwili baada ya hiyo incident akaniita tena kwaajili ya kazi ya Bongo Star Search sasa, na hii nyengine skia, nilipoitwa sikujua kama yeye ananitaka mimi kama Judge, mawazo yangu yalidhani anataka MTANGAZAJI wa shindano hilo, kumbe yeye alikua na BETTER idea, kama wazungu wanavyosema, the rest is history.

Rita ameniona mimi nakua mbele ya macho yake, nami pia nimeona transformation ya maisha yake kama Mama na Dada. Mengi amepitia ya hadharani na kwas siri, ninayo yajua na nisiyo yajua, ila ambalo nina uhakika nalo ni JINSI AMBAVYO MIMI NAJIVUNIA YEYE, kwa mishale yote ALOIKWEPA na kuendelea KUSIMAMA IMARA, Rita Paulsen Hans ni SHUJAA NA NUSU.

Mengi ameyaongea humu, ambayo ningependa uyaskie MWENYEWE bila ya mimi kudokoa lolote, hakuna chumvi wala sukari ilozidishwa humu ili ‘picha ipendeze’, badala yake ni simulizi nyundo ambazo kama kawaida zitakufanya ujifunze mambo mengi na pia kuangalia baadhi ya vitu kwa jicho jengine.
Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.