SE6EP7 - Salama Na TID | NYOTA YAKO Salama Na

    • Entertainment News

Listen on Apple Podcasts
Requires subscription and macOS 11.4 or higher

Khalid Mouhamed Tidy aka TID ni familia kwangu, mimi na yeye tunafahamiana zamani sana na ukabila wa Mama zetu pengine ndo ulitufanya tuwe karibu kwa kiasi hicho. Tulikua na marafiki wanaofahamiana. Sote tulikua tunaanza kazi na utafutaji tukiwa pamoja na pengine kiu na ubora wa kazi zetu ulitufanya kipindi flani twende kwenye njia tofauti. Ila kina mmoja alikua anashinda mechi zake kwenye ligi yake na kutawazwa kuwa bingwa wa mashindano kadha wa kadha.

Nadhani yeye kuwa STAR mkubwa hapa Afrika ya Mashariki kulitokana na kujielewa kwake na kuwa mvumilivu wa mambo kwa kipindi kirefu. Usikuambie yoyote kwamba TID alikua star kwa usiku mmoja au, yaani alilala na kuamka then boom, hapana. Ilibidi afanye kazi nyingi, na watu wengi na kwenye hizo kazi ndo alikutana na Boss ambaye aliona kipaji chake na akamuunganisha na mtu sahihi. Baada ya hapo kazi ikafanyika na mengine yakafuata.

Alikua mkubwa kiasi gani lakini? Alipitia mitihani gani? Na kipi anajivunia sana kwenye fani yake? Yepi majuto yake? Lowest moment kwenye maisha yake ilikua ipi? Kama huwa anapata mawazo ya kutaka siku zirudi nyuma na pengine angefanya vitu kwa utofauti? Kina nani na nani wanamaanisha nini katika maisha yake? Muziki wa nyumbani umemfanyia nini kwenye maisha yake?

Wapi alisoma? Elimu yake ni ya kiwango gani? Ukaribu wake na Mama yake? Maisha ya sasa? Misukosuko aliyopitia miaka mitatu iliyopita ambayo ilimfanya aingie matatani na vyombo vya dola na mambo mengine mengi tuliyazungumzia humu. TID ana Kaka zake ambao wako naye karibu sana. Hilo nalo tuliligusia humu. Suala la yeye kuwa trend setter na mwisho wa siku hana faida anayopata kwa miaka mingi na nini hilo humfundisha pia hatukuliacha nyuma.

Haya yalikua maongezi ya mtu na rafiki yake wa siku nyingi, humu pia nilitaka kujua kuhusu well being yake na mipango ya sasa ikiwa ni pamoja na TV show yake ambayo inamfanya awe busy na kumpa yeye nafasi ya kuwa na mashabiki wake kwa karibu zaidi. Tidy ni mcheshi, na mwenye kujielewa. Hatukuacha pia kuongelea mahusiano yake na Marehemu Albert Mangwea na maswali yaliyokua yamegubika juu ya chanzo cha kifo chake na pia yeye kama Rafiki na star, nini alijifunza.

Yangu matumaini uta enjoy, utacheka na kuelewa baadhi ya mambo ambayo ulikua unajiuliza au pengine ulikua hujui kutoka kwa mmoja wa wasanii wa Bongo Flavour ambaye amesaidia kwa kiasi kikubwa kuutambulisha mziki wetu KIMATAIFA.

Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.