SE6EP8 - Salama Na PATRICIA HILLARY | MWAIMU MAME Salama Na

    • Entertainment News

Listen on Apple Podcasts
Requires subscription and macOS 11.4 or higher

Mtu kama Mama, Mama Patricia Hillary ni TUNU ya Taifa, ambayo pengine tunaichukulia tu poa, hatujui anaishije, analala wapi? Kama ana mahitaji yote ya kibinadamu ambayo anatakiwa kuwa nayo na pengina hata kujua kama ana furaha katika maisha yake? Sidhani kama hicho kinaweza kikawa kitu kigumu kwa yoyote kati yetu kuweza kufanya, au pengine Wizara husika? Ambayo inamhusu moja kwa moja? Kujua kama haki zake zote za ki uandishi na kisanii anazipata?

Kuanzia Mwaka 1980, pengine ulikua hata hujazaliwa basi Mame Patricia ndo alikua anaanza safari yake ya muziki RASMI kabisa. Mzaliwa wa Tanga, mjini Dar es Salaam alikuja baada ya kupita kwenye mchujo wa kutafuta vipaji uliokua ukifanywa mkoa kwa mkoa na Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi lilikua linazunguka nchi nzima kwaajili ya kutafuta vipaji kwa waimbaji wa muziki wa Dansi, Taarab na hata bendi yao ile ya brass. Kama ulikua una kipaji hiyo ilikua ni moja ya njia za kuingia pia jeshini na kupata ajira ya moja kwa moja.

Kwa miaka 40 Patricia amekua akilitumikia jeshi kwa moyo wake wote. Huku akiwa anaendeleza kipaji chake cha kuimba na kuandika, wakati huo huo alikua anafanya mafunzo ya kijeshi ambayo yamemsaidia sana kumuweka sawa na kumpa discipline ya kazi na kujiheshimu na kuheshimu kipaji chake pia. Pengine asingekua mwanajeshi basi heshima ya kuweza kukaa kwenye chati kwa muda mrefu na kujijali yeye pamoja na familia yake visingewezekana.

Muandishi, muimbaji, Mama, mke na icon ya muziki wa Taarab. Alinipa khadithi ya jinsi ambavyo aliandika wimbo ya Njiwa ambao wengi wetu ndo tunamfahamu nao, na nani alimsaidia kuweka mashairi yake sawa, na kupata melody nzuri ambayo ndo imefanya nyimbo hizo kuishi, kumbuka kuna njiwa namba moja na mbili, ulijua hilo? Well… Mie nilikua sina uhakika ila kwenye maongezi yetu haya niliupata vizuri.

Mimi na yeye pia tulizungumzia utenzi wa sasa ambao umekua na ushairi wa matusi ya waziwazi na maoni yake juu ya hilo, hakusita kunipa pia elimu ya uandishi na baadhi ya nyimbo za zamani ambazo kwa mujibu wake pia zilikua zimeandikwa kwa mashairi ya kuficha sana kiasi kwamba mimi ndo nilijua wakati wa mazungumzo haya kwamba maana yake si hiyo ambayo mimi nilikua naidhania, hiyo ndo ‘sanaa’ na hivyo ndivyo ambavyo utunzi unatakiwa KUWA.

Pia tuliongelea mapenzi yake na social media, jinsi ambavyo yuko active sana na kama huwa anafanya yeye mwenyewe hizo likes na comments. Tuliongelea mahusiano yake na Marehemu Ruge Mutahaba. Urafiki wake la Lady JD, watoto wake wawili ambao Mungu ndo alimbariki nao na kifo cha mtoto wake mmoja. Usimamizi wa kazi zake ambazo mwanae ndo anafanya sasa na pia Marehemu Mumewe tulimzungumzia kwa kiasi.

Sasa Mama amestaafu jeshini baada ya kulitumikia kwa miaka AROBAINI. Maisha baada ya hapo yakoje? Mipango yake? Ana miss? Bado ana mapenzi na muziki kama zamani?
Majibu ya maswali haya yote yako katika maongezi haya na yangu matumaini uta enjoy. Mpaka wakati mwengine, take care.

Love,
Salama.