Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

  1. 16小时前

    Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka

    Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.  Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa  mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka. Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka. Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi. Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”. Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada. Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.

    2 分钟
  2. 16小时前

    22 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia majadiliano huko Baku Azerbaijan kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi, na kazi za walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT-11 huko DRC. Makala inaturejesha kataika mkutano wa COP29 na mashinani inatupeleka Namibia, kulikoni? Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala inakupeleka Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 kumsikia kijana kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, tunasikia kauli ya Willem Westhuizen, mkulima kutoka Namibia, akielezea changamoto zinazotokana na ukame unaoathiri maisha yao kila siku”.  Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!

    10 分钟
  3. 16小时前

    Mafunzo ya walinda amani kutoka Tanzania huko Beni yajengea uwezo walimu kusaidiana na watoto

    Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.  Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao. Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa wameathirika kisaikolojia. Zavadi Mbambu ni miongoni mwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto lukuki ikiwemo mapigano. Akisema stress, anamaanisha msongo. “Unakuwa na wanafunzi wanaokuwa na msongo wa mawazo kutokana na jambo ambalo wanaishi, na hata mauaji. Kuna wale ambao hata wameua wazazi wao , hata familia yao yote.  Na kwa hao wanafunzi wanapoingia shuleni , wanakuwa kama hawako ndani, fikra zao zinakuwa mbali .  Lakini kupitia mafunzo nimewaelewa , na tumejua namna gani ya kuishi nao. Na tayari mabadiliko yameanza kuonekana.” Pacifique Kyakimwa, mmoja wa wanafunzi anasimulia mkasa mmoja. “Kuna mwenzetu  aliyekuwa na tatizo, yaani tukiwa ndani ya shule, alikuwa anacheka, yaani anatusumbua hadi hatumwelewi mwalimu. Lakini tangu wameanza kufundisha hili somo, wameanza kuelewa . Ameanza kuwa na akili inayotumika vizuri. Mafunzo haya yamefika wakati tunahitaji , na imetusaidia sana.”

    2 分钟
  4. 1天前

    Jinsi usawa wa kijinsia na rika katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya

    Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi na umeimarisha usimamizi wa ardhi kwa ajili ya maisha bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kaunti zote zinazotekeleza. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Cecily Kariuki anaeleza matokeo yake. Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uuliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi na umeimarisha usimamizi wa ardhi kwa ajili ya maisha bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kaunti zote zinazotekeleza. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Selina Jerobon anaeleza matokeo yake katika makala hii..… Wazee wa jamii za kijiji cha Maiyanat iliyoko katika kaunti ya Turkana kaskazini-magharibi mwa Kenya wanafanya kikao cha pamoja hapa, wakiwa wamevalia mavazi yao ya kitamaduni, watoto wakiwa pembeni wakifuatilia kinachoendelea. Wanajadili matumizi mazuri ya mashamba ya jamii zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na marika yote. Je, awali umiliki wa ardhi ulizingatia usawa huu? Ratinui Macharia ni mwenyekiti wa ardhi ya jamii ya Maiyanat, anasema, “Awali, wanawake na vijana hawakuruhusiwa kushiriki au hata kuchaguliwa kwenye kamati ya ardhi lakini sasa imetuleta sote pamoja.” Lois Kimere ni mwanamke mwanachama wa kamati ya ardhi Maiyanat. “Kulingana na jamii za Maiyanat, wanawake hawakuwa wanaonekana kama watu wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya kijamii. Tulihamasisha wanawake kuhusu mambo ya ardhi, uongozi katika vijijini na katika ngazi za kitaifa hususani serikali, na katika bishara.” Kwa msingi wa dharura, awamu ya kwanza na ya majaribio ya mpango huu ilitekelezwa katika kaunti za Laikipia, Nandi, Pokot magharibi, Baringo, Vihiga, Marsabit, Kajiado, Samburu, Tana River na Turkana. Asha Lekudere ni mwanachama wa ardhi ya jamii ya sereolipi, anasema FAO imeimarisha mtazamo wao. “Zamani tulikuwa na shamba la kikundi. Kisha FAO ikatupeleka kwenye mafunzo kadhaa. Niliweza kujifunza maana ya umiliki wa ardhi kwa jamii yetu ya samburu, uwezo wetu na haki za wanawake.” Chini ya ajenda ya ardhi ya jamii, programu iliwezesha mila shirikishi na jumuishi katika usimamizi wa ardhi kwa njia ya usawa wa jinsia na rika zote. Na hatua gani zinaweza kuchukuliwa mizozo inapotokea? Mpango wa usimamizi wa ardhi umekuza mfumo mbadala wa mahakama, wa kupigania haki za kibinadamu unaojulikana kama AJS, njia bora ya kusuluhisha kesi mashinani na kuachilia ardhi itumike kwa ajili ya jamii zote haraka iwezekanavyo. Jonathan Osewu, Msajili wa ardhi  katika kaunti ya Kajiado anasema, “Katika utamaduni wetu wa kimasai tunazo njia nyingi sana za kutatua mizozo. Kwa hivyo AJS ilipoletwa, ilikuwa ni njia bora ya kuimarisha utaratibu wetu wa jadi wa kutatua kesi.” Na isitoshe, njia za teknolojia za kutoa ramani ya ardhi na rasilimali yote kwa muonekano wa anga, GIS ili kusaidia kufanya maamuzi ya kesi haraka, pia imechangia utangamano katika jamii husika. Vituo hivi vimetekelezwa katika sehemu nyingi ikiwemo kaunti ya Vihiga. Wilber Ottichilo, Gavana wa mkoa wa Vihiga anatoa shukrani kwa FAO. “Kama kaunti ya Vihiga,…

    5 分钟
  5. 1天前

    21 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kushuhudia jinsi mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa wa "kusaidia jamii kufikia Ajenda 2030” ambao FAO imetekeleza kwa kaunti kadhaa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno. Hague kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ICC ambayo leo imetoa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Galant  na kiongozi wa kundi la kipalestina la Hamas Mohamed Diab Ibrahim al-Masri alimaarufu kama  kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaifu wa vita ulitendeka wakati wa vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas.Mjini  Baku nchini Azerbaijan mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachanama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabainchi COP29 unaelekea ukingoni  na leo ukijikita na masuala ya kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa waliozungumzia changamoto ya tabianchi kwa wanawake ni  Jemimah Njuki, mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa kiuchumi katika shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women.“Raia  wanaoshtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Uganda hukosa dhamana sawa ya mchakato wa kisheria kama wale wanaoshtakiwa katika mahakama za kiraia,” amesema Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu hii leo kufuatia tukio la kutekwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye akiwa nchini Kenya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MHARABU”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 分钟
  6. 2天前

    COP29 Georgina Magesa: Watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama

    Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 unaoendelea huko Baku Azerbaijan umeleta pia watoto na vijana wanaharakati wa mazingiria kutoka kote ulimwenguni na kuwapatia fursa kuketi katika meza moja na viongozi ili kuhakikisha mustakabali wao umewekwa katika ajenda ya mkataba huo.  Jukumu lao kama wachechemuzi wa mabadiliko chanya na hitaji la mazungumzo na ushirikiano kati ya vizazi lilitambuliwa rasmi katika matokeo ya Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF mnamo Septemba 2024. Georgina Magesa, msichana mwenye umri wa miaka tisa na mwanaharakati wa mazingira, ambaye amewakilisha watoto wenzake kutoka Tanzania katika Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan. Anatoa ujumbe mahsusi akianza kwa kusistiza kuwa watoto pia wana mchango katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi. “Watoto wenzangu duniani kote, nyie pia mnaweza kuleta mabadiliko chanya. Anza na hatua ndogo pia muwe na ndoto kubwa. Panda miti. Hifadhi maji. Jifunze kuhusu mazingira yetu. Kwa Pamoja vitendo vyetu vidogo vitageuka mabadiliko makubwa” Katika mwaka huu wa 2024 ambao viwango vya joto duniani vimevunja rekodi duniani, watoto na vijana wanaendelea kupaza sauti zao wakihimiza viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka zinazohitajika ili kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Georgina anasema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF liko mstari wa mbele, lakini sasa ni wakati wa mshikamano kwa ajili ya mazingira bora kwa watoto wa leo, na wa zama zijazo.. “Kwa viongozi wa dunia walioko hapa leo, hii si kazi ya UNICEF pekee. UNICEF inafanya kazi nzuri na sisi watoto, lakini tunahitaji msaada wako ili kujenga ulimwengu wa kesho ambapo hakuna mtoto anayepaswa kuchagua kati ya afya na elimu yake; ambapo hakuna mtoto anayekunywa maji yasiyo salama; hakuna mtoto anayekosa shule kwa sababu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi; na ambapo kila mtoto ana nafasi ya kuwa na afya bora na elimu bora.” Georgina anatamatisha kwa kusisitiza kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi limenyima watoto haki zao hivyo kwa kila mtu... “Kumbuka unapolinda mazingira unalinda afya, elimu na ndoto za watoto. Mtoto mwenye afya bora na elimu bora anaweza kubadilisha ulimwengu.” Ama kweli watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama!

    4 分钟
  7. 2天前

    20 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti siku ya watoto duniani, na kwa kutambua siku hii tunamulika mikutano yote yanayoendelea kwa ajili ya haki za watoto na vijana, ambao wametoa ujumbe wao kutoka Baku nchini Azerbaijan na Denmark wakiwakilisha nchi zao. Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao.Kama ulivyosikia katika taarifa yetu ya kwanza leo ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani..Makala ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, tunakupeleka Baku Azerbaijan katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29,  ambako Selina Jerobon amefuatilia mkutano wa watoto na vijana inayomulika mchango wao katika kuhakikisha mazingira bora.Mashinani katika kuadhimisha siku ya watoto duniani tunabisha hodi msitu wa Amazoni nchini Peru kwa mtoto Susan akitoa wito kwa dunia kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kulinda msitu huo kunusuru kizazi cha watoto wa sasa na wa vizazi vijavyo katika taifa hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 分钟

评分及评论

5
共 5 分
4 个评分

关于

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

更多来自“United Nations”的内容

若要收听包含儿童不宜内容的单集,请登录。

关注此节目的最新内容

登录或注册,以关注节目、存储单集,并获取最新更新。

选择国家或地区

非洲、中东和印度

亚太地区

欧洲

拉丁美洲和加勒比海地区

美国和加拿大