Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.

若要收听包含儿童不宜内容的单集,请登录。

关注此节目的最新内容

登录或注册,以关注节目、存储单集,并获取最新更新。

选择国家或地区

非洲、中东和印度

亚太地区

欧洲

拉丁美洲和加勒比海地区

美国和加拿大