100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

    UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inaanzia Bujumbura Burundi kisha inakupeleka Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kama inavyosimuliwa na Evarist Mapesa.

    • 3 min
    UNICEF: Watoto walioko Rafah wasihamishwe kwani tayari wako taabani

    UNICEF: Watoto walioko Rafah wasihamishwe kwani tayari wako taabani

    Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo. 
    Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini New York, Marekani inakumbusha kuwa amri ya kuhamia Rafah, kusini mwa Gaza iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Israel imefanya eneo hilo sasa kuhifadhi watu wapatao milioi 1.2, nusu yao wakiwa ni watoto wakiishi kwenye mahema au nyumba zisizo kamilifu.
    Kwa kuzingatia mlundikano wa watoto, wakiwemo wengi walio hatarini wakihaha kuishi, pamoja na ukubwa wa ghasia zinazoendelea na njia za kutumia kukimbia zikiwa na vilipuzi au hakuna njia kabisa , UNICEF inaonya madhila zaidi kwa watoto na operesheni za kijeshi vitaongeza vifo zaidi vya raia na miundombinu ya huduma za msingi iliyosalia kusambaratishwa.
    Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell amesema zaidi ya siku 200 za vita zimekuwa ‘mwiba’ kwa watoto na Rafah hivi sasa ni mji wa watoto wasio na pahala salama pa kukimbilia Gaza. Iwapo operesheni kubwa za kijeshi zikianza, watoto sio tu watakuwa hatarini na ghasia, bali pia vurugu na kiwewe wakati ambapo hali zao kimwili na kiakili zimeshadhoofishwa.
    Hivyo UNICEF inasisitiza wito wa Kamati ya Mashirika ya UN kwa Israel ya kuzingatia wajibu wake kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu ya kupatia chakula na matibabu watoto na kuwezesha operesheni za kugawa misaada na kwa viongozi wa dunia kuzuia janga zaidi kwa watoto Gaza sambamba na sitisho la mapigano.

    • 1 min
    06 MEI 2024

    06 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza, na mafuriko nchini Kenya huku mashirika wakihaha kusaidia waathirika. Makala tunasalia na mada hiyo ya mafuriko Afrika mashariki na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? 
    Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo..Wingu kubwa la mvua likiwa limetanda kwenye mji wa Garsen, ulioko kaunti ya Mto Tana nchini Kenya, Eva Ghamaharo, mama wa watoto watatu anarejea nyumbani akitembea na watoto wake wawili mapacha wenye umri wa miaka mitatu baada ya kununua matumizi ya nyumbani kutoka kioski cha jirani. Watoto hawa wawili mapacha wa kike ni Grace na Jane na wanaonekana na furaha kwani angalau leo mama yao ameweza kuwanunulia kila mmoja pakiti ya maziwa na wanakunywa kwa furaha..Makala inaangazia madhila ya mafuriko kwa wakimbizi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katuka ukanda wa Afrika Mashariki.Na mashinani tutaelekea Darfur nchini Sudan kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa umerejesha matumaini kwa waathirika wa vita.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    • 9 min
    Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu

    Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu

    Mvua za El-nino zikiendelea kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo taifa la Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza limepatia msaada wa hali na mali wakazi wa kaunti ya mto Tana walioathiriwa na mafuriko hayo.  Cecily Kariuki na taarifa zaidi.
    Video ya UNICEF Kenya inaanza ikimuonesha mkazi huyu wa hapa mji wa Garseni katika kaunti ya mto Tana akiwa amebeba kikapu huku akiwa na watoto wake wawili wakirejea nyumbani.
    Huyu si mwingine bali Eva Ghahamaro akisimulia yaliyowasibu na msaada ulivyowafikia. Anasema, “Maisha yalikuwa magumu kwa sababu mafuriko yaliharibu nyumba na mashamba. Vyakula vilisombwa. Watu wengi waliteseka sana. Maafisa wa kaunti waliona tunateseka, walitembea nyumba kwa nyumba wakisajili majina watu wenye watoto na wajauzito. Nilikuwa nikipata shilingi 2,750.”
    Shilingi 2750 ni sawa na dola 20 za kimarekani, na wanapatiwa kila mwezi. Rachael Wamoto ni afisa kutoka UNICEF Kenya na anafafanua kuhusu usaidizi huo ambao haukulenga tu waathiriwa wa mafuriko bali pia kaya zenye watoto walio na utapiamlo.
    “Kwa programu hii tuko katika kaunti sita. Kwa kaunti ya Mto Tana tumeweza kufikia kaya 1,800 (Elfu Moja Mia Nane) katika miji ya Galole na Garsen. Vikundi kazi vya Kaunti ndio vilihusika kwenye kuchagua kaya zenye uhitaji. Hivyo tuliweza kutambua watu walioathiriwa na mafuriko na waliokimbia makwao. Tunashirikiana na serikali na mamlaka ya taifa ya udhibiti wa ukame. Tuliweza kutumia orodha yao na hivyo kufikia haraka wahitaji.”
    Msaada wa fedha taslimu uliofadhiliwa na serikali ya Uingereza, umekuwa na manufaa kwa Eva. Akisema twins, anamaanisha watoto mapacha.
    “Nilitumia hizo fedha kununulia wanangu chakula, uji, mkaa na pia mahindi na mchele kwa familia yangu. Halikadhalika, watoto wangu hawa mapacha niliwaandikisha shule nikawanunulia sare na mabegi ya shule. Nimeshukuru sana UNICEF kwa msaada wao kwa sababu mmetusaidia.

    • 2 min
    Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

    Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

    Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira. 

    • 3 min
    Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

    Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

    Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.
    Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Matal Amin iliyoko Baidoa nchini Somalia zaidi ya wananchi 1500 wanahaha huku na kule kurekebisha maturubai yao ambayo hasa ndio makazi yao ikiwa ni maandalizi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza muda wowote. 
    Hali ni hivyo hivyo pia katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rama cade kama anavyotueleza Kiongozi wa kambi hiyo Abdulkadir Adinur Aden anasema “Tunajiandaa na msimu wa mvua ili kupunguza athari za mafuriko, tunatumia maturubai ya plastiki kufunika makazi yetu na pia tunatumia viroba vilivyojazwa michanga ili kuzuia mnomonyoko mafuriko yatakapo tukumba.”
    Wadau mbalimbali wa misaada ya kibinadamu ikiwemo OCHA wamepeleka katika kambi hizo misaada kama vile chakula na lishe, viroba vilivyojazwa michanga, maji safi na salama pamoja na dawa mbalimbali ikiwemo za kipindupindu hata hivyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa OCHA nchini Somalia Erich Ogoso anasema mengi ya makazi hayataweza kuhimili mvua kubwa na hivyo yataharibiwa.
    “Wananchi wanaoishi katika kambi hii ya Matal Amin walifika hapa mwaka 2017 wakitokea katika mkoa wa Bay ambako walikimbia ukame, mzozo, na mambo mengine. Wamekuwa wakiishi hapa tangu kipindi hicho, mafuriko yanapokuja wamekuwa wakiondoka eneo hili na kukikauka wanarejea na sasa wanajiandaa tena na mafuriko na kuna uwezekano wakutakiwa kuondoka eneo hili.” 
    OCHA wanasema taarifa walizopokea kutoka kwa wadau wao walioko mashinani mpaka kufikia tarehe 28 mwezi Aprili mwaka huu, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Somalia zimewaathiri zaidi ya watu 124,155 na kuwaacha zaidi ya 5,130 bila makazi huku vifo vya watoto saba vikiripotiwa. 

    • 2 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Serial
Serial Productions & The New York Times
Up First
NPR
The Ben Shapiro Show
The Daily Wire
The Charlie Kirk Show
Charlie Kirk
The Tucker Carlson Podcast
Tucker Carlson Network

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations