100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko

    Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko

    Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa  kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii

    • 3 min
    UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka

    UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka

    Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.
    Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.
    Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha.
    "Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaji wa watu wengi, milipuko hatari, na kuongezeka kwa utapiamlo kumeupinda mfumo wa afya wa Haiti, lakini kunyongwa kwa minyororo ya usambazaji kunaweza kuwa ndio kunauvunja."
    Makontena yaliyojazwa vifaa muhimu yamezuiliwa, au kuporwa, kama ilivyokuwa kwa maghala na maduka mengi ya dawa. Wakati huo huo, mamia ya makontena yaliyosheheni vifaa vya kibinadamu yamekwama huko Port-Au-Prince ikiwa ni pamoja na kontena za UNICEF zilizo na vifaa vya watoto wachanga, wajawazito na vya matibabu.
    Port-Au-Prince, kitovu kikuu cha Haiti, kwa kawaida hupokea na kutuma mizigo ya uagizaji wa vifaa tiba vya Haiti. Sasa jiji hilo limelemazwa na vurugu, na wakazi wake zaidi ya 160,000 wameyakimbia makazi yao, jiji hilo haliwezi kutosheleza mahitaji ya watu ambao kwa wakati mmoja wanapambana na majeraha ya kimwili na hatari ya magonjwa, inafafanua taarifa ya UNICEF.
    Mawimbi ya familia zilizofurushwa zinazotafuta usalama, hasa katika sehemu ya kusini mwa nchi, yanaleta shinikizo la ziada kwa huduma za afya za wanakokimbilia, ambazo hata kabla ya kuongezeka kwa mzozo hazikuweza kuhimili mahitaji. Uhaba wa wafanyakazi umeenea, na takriban asilimia 40 ya wafanyakazi wote wa matibabu wameondoka nchini Haiti kutokana na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama.
    Kati ya Oktoba 2022 na Aprili 2024, Haiti iliripoti jumla ya visa 82,000 vinavyoshukiwa kuwa na kipindupindu. Takriban watu milioni 4.4 nchini Haiti wanahitaji msaada wa haraka wa chakula, na watu milioni 1.6 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya uhaba wa chakula, jambo ambalo linaongeza hatari ya kupata tatizo la uzito mdogo kwa watoto na utapiamlo. Kuwasili kwa msimu wa mvua kunatazamiwa kuzidisha hali kuwa mbaya zaidi, hivyo kusababisha ongezeko la visa vya magonjwa yatokanayo na maji pamoja na magonjwa yanayoenezwa na mbu, kama vile malaria.
    Ili kukabiliana na hali hiyo, UNICEF na wadau wanatafuta njia mbadala za kuagiza na kusambaza mizigo. Kupitia njia za pili za uingizaji na utoaji, pamoja na Wizara ya Afya, wafadhili wa kimataifa na washirika, UNICEF imeweza kuendelea kupeleka chanjo, dawa na vifaa vya matibabu kwa watoto nchini Haiti ambao wanahitaji zaidi.
    Tarehe 18, 20 na 21 Mei 2024, UNICEF iliwezesha kuwasilisha tani 38 za vifaa vya kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya na kipindupindu, na bidhaa nyingine muhimu za matibabu nchini Haiti kupitia njia ya anga kwa kuungwa mkono na Muungano wa Ulaya na WFP kutoka Panama hadi mji mkuu wa Haiti, ambapo UNICEF na Umoja wa Mataifa wameanzisha kituo kipya cha kufanya kazi. Lakini msaada zaidi unahitajika.
    "Hatuwezi kuruhusu vifaa muhimu ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya watoto kubaki vikiwa vimezuiliwa kwenye maghala na makontena. Lazima viwasilishwe sasa,” amesisitiza Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti.

    • 1 min
    22 MEI 2024

    22 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? 
    Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Makala inatupeleka Kaunti ya Garisa nchini Kenya ambako waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo ya hivi karibuni walio katika makambi za muda za wakimbizi wa ndani wanapokea msaada wa fecha na vocha kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake ikiwaweze kujikimu.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

    • 10 min
    Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha - Nika Alexander

    Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha - Nika Alexander

    Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”
    Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza tofauti ya kwanza anayoona sasa akiwa amerejea kutoka Gaza ambapo wakati angali kule siku baada ya siku wakisikia mlio wa ndege basi bomu linaweza kuanguka dakika yoyote, wakati sasa ukiwa sehemu ambayo si ya vita akisikia mlio wa ndege pengine ni watu wanaendea likizo ni kama watu wa Gaza wanaishi kinyume na ulimwengu. 
    Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kurejea Gaza Bi.Nika anasimulia hali ya kule. 
    “Nilichoondoka nacho ni mawazo ya jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu wa Gaza, jinsi hali ilivyo ngumu kwa watu wanaojaribu kuwasaidia watu wa Gaza na jinsi kulivyo hatari.” 
    Amesema hospitali zinazofanya kazi ni chache na hazifanyi kazi kamili.
    “Kimsingi, kote Gaza, ni theluthi moja ya hospitali ndio zinafanya kazi. Kwa hivyo takriban hospitali 12 kati ya 36 bado zinaweza kufanya kazi kwa namna fulani. Hawawezi kutoa huduma kamili. Baadhi yao wanafanya kama sehemu ya kutoa huduma ya kwanza na kusaidia wenye kiwewe, ambapo wanajaribu tu kutibu wake wanakuwa wanavuja damu na vyovyote vile wawezavyo ilimradi watu wasife kutokana na majeraha.”
    Afisa huyu wa mawasiliano ya dharura anasema pamoja na yote hayo lakini lipo lililompa matumaini licha ya kutokuwepo kwa eneo lolote salama katika Ukanda wa Gaza. 
    “Kilichonivutia sana ni kwa jinsi kila mtu anavyofanya kazi kwa bidii licha ya hali mbaya ambapo kila kelele inaweza kuwa ni mlipuko karibu yako, au unaweza kuwa unakulipukia wewe. Nilipoondoka Rafah wiki moja iliyopita, tulikuwa wafanyakazi 19 wanaondoka na wengine 20 wa Umoja wa Mataifa wanaingia Rafah. Ninawaona wenzangu hao kuwa wajasiri sana, na sio kwamba wanakuja kujifanyia kazi wenyewe bali wanakuja kushirikiana na wafanyakazi wa Gaza wa sekta ya afya.” 

    • 2 min
    21 MEI 2024

    21 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni? 
    Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameeleza wasiwasi mkubwa walio nao juu ya usalama wa wagonjwa na wafanyakazi waliokwama katika hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Ukraine, limeeleza kuhusu wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayozidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa Waukraine na kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi mapya ya ardhini ya Jeshi la Urusi katika eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv.Na katika mashinani leo tunakupeleka katika eneo Bunge la Ngong lililoko katika kaunti ya Kajiado  nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa utunzaji wa chemichemi ya maji.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 10 min
    Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer

    Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer

    Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto katika kikosi na jamii ya wenyeji. Msimulizi ni Anold Kayanda

    • 3 min

Top Podcasts In News

Global News Podcast
BBC World Service
The Denny J Show
Denny J
What If... We think differently?
Tendai Murisa
Black Land Podcast
iHeartPodcasts
FT News Briefing
Financial Times
Al Jazeera News Updates
Al Jazeera

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
The Lid is On
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations