Mjadala wa Wiki RFI Kiswahili
-
- Noticias
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
-
Rais wa DRC Felix Tshisekedi athibitisha kuwa uchaguzi utafanyika mwaka 2023
Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi amewaambia viongozi wa dunia kuwa uchaguzi mkuu utafanyika nchini mwake mwaka 2023 kama ilivyopangwa kikatiba.Kauli hii pia imeungwa mkono na spika wa Bunge la kitaifa huko DRC Chistophe Mboso Nkodia wakati wa Mkutano wake na Raia kwenye mji wa Kinshasa Siku ya Jumapili iliyopita.Hata hivyo Tume ya Uchaguzi inayotakiwa kuandaa uchaguzi huo, haijawekwa wazi.
-
Joto la kisiasa kuelekea uchaguzi nchini Kenya 2022
Makala haya mJadala wa wiki tunajadili siasa za Kenya kuelekea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa rais wa hapo mwakani.
-
Mapinduzi nchini Guinea na hali ya kisiasa kwa watawala barani Afrika
Kwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Guinea na nini sababu za kutokea mapinduzi ya serikali barani Afrika. Swala ni kwa nini imejengeka dhana kwamba kiongozi anayeng'ang'ania madaraka mwisho wake siku zote ni mapinduzi ya kijeshi, nini kifanyike ili ifike mahali demokrasia na watawala waheshimu katiba za nchi zao?
Mjadala wa wiki na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka -
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amtaka naibu wake ajiuzulu
Kwenye Mjadala wa wiki, tunaangazia hali ya kisiasa nchini Kenya. Wiki hii, rais Uhuru Kenyatta amemwambia naibu wake William Ruto ajiuzulu iwapo anaona hafurahishwi na ajenda ya serikali ambayo yeye ni mdau mkubwa.
-
Siku 100 za Waziri Mkuu wa DRC Sama Lukonde
Tunajadili siku 100 za serikali ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Sama Lukonde.
-
Siasa za vyama nchini Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu
Kenya inajiandaa kuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2022. Vyama vya siasa vimeanza maandalizi kujiweka tayari kwa uchaguzi huo. Lakini je, vyama hivi vimejiandaa vya kutosha ? Tunajadili.