100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

    Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

    Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania.
     

    • 5 min
    Jifunze Kiswahili: Tofauti ya “Adili na Idili.”

    Jifunze Kiswahili: Tofauti ya “Adili na Idili.”

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”

    09 MEI 2024

    09 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika kazi za Zahra Salehe na timu yake ya ICCAO nchini Tanzania katika kusongesha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza na asasi za kiraia Nairobi Kenya, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki. 
    Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga mjini Nairobi Kenya ukiwaleta pamoja washiriki takriban 1500 kutoka kila kona ya dunia wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Sepemba mwaka huu. Umoja wa Mataifa Kenya ndio mwenyeji wa mkutano huo ambapo Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini humo Dkt. Stephen Jackson amesema taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa mstari wa mbele kwenye kusongesha ushirikiano wa kimataifa tangu uhuru wake.Huko Gaza takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah tangu Jumatatu wiki hii wakati mashambulizi ya Israel yakishika kasi usiku kucha kuamkia leo ndani na katika viunga vya vya mji huo a Kusini mwa Gaza kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Na kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 9 min
    Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

    Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 anajibu swali aliloulizwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwamba Je, Lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu linalohamasisha usawa wa kijinsia litafikiwa huko Zanzibar kufikia mwaka 2030?

    • 3 min
    Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

    Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

    Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao. 
    Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa takwimu hizo likinukuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, huku ikisema kuwa idadi inazidi kuongezeka kila uchao.
    IOM kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na Nairobi, Kenya inasema mvua hizo za masika zimesababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya udongo na kuharibu miundombinu muihmu kama vile barabara, madaraja na mabwawa ya maji.
    Mkurugenzi wa IOM Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika Rana Jaber anasema mafuriko hayo ya kipekee na yaliyosababisha uharibifu yameibua ukweli mchungu wa mabadiliko ya tabianchi, kwa kusababisha vifo na kufurusha watu makwao, watu ambao sasa wanakabiliwa na kazi kubwa ya kujijenga upya huku hali zao zikizidi kuwa taabani.
    Ni kwa mantiki hiyo anaesema katika nyakati hizi muhimu, wito wa IOM unasalia kuchukuliwa kwa hatua endelevu na za dharura za kutatua ukimbizi wa binadamu unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi.
    Pamoja na kushirikiana na serikali na wadau kusambaza misaada ya hali na mali ya kuokoa maisha ikiwemo fedha taslimu kwa walioathiriwa huko Burundi, Kenya, Somalia, Ethiopia na Tanzania, IOM inasema mjadala ujao huko Ujerumani kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC ni dhahiri shairi kuwa mazungumzo kuhusu tabianchi lazima yazingatie ukimbizi utokanao na janga hilo.
    Afrika inaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi licha ya kuchangia asilimia 4 pekee ya hewa chafuzi duniani.

    • 1 min
    08 MEI 2024

    08 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, na wakimbizi wanaorejea nchini Sudan Kusini kutoka Sudan. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?
    Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.Katika makala Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, alipata nafasi kuzungungumza na Anold Kayanda.Na mashinani inatupeleka katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri wa Kidemkrasia ya Congo DRC, ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku kadhaa sasa zimesababisha maafa, ikiwemo maelfu ya familia kuathirika. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 10 min

Top Podcasts In News

Path to Power
Matt Cooper & Ivan Yates
The Rest Is Politics
Goalhanger Podcasts
The Indo Daily
Irish Independent
The Stardust Tragedy
The Irish Sun
The David McWilliams Podcast
David McWilliams & John Davis
The Rest Is Politics: US
Goalhanger

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
UNcomplicated
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain
United Nations
The Lid is On
United Nations
Interviews
United Nations