![](/assets/artwork/1x1-42817eea7ade52607a760cbee00d1495.gif)
128 episodes
![](/assets/artwork/1x1-42817eea7ade52607a760cbee00d1495.gif)
Sepetuko Standard Media
-
- News
Kurunzi ya falsafa inayoangazia bila woga masuala mazito yanayoiathiri jamii.
-
Maandamano ya Wakenya Dhidi ya Mswada wa Fedha
Maandamano ya Wakenya dhidi ya Mswada wa Fedha yahweh onyo kwa serikali. Onyo kuwa wananchi wamejifundisha kujitetea na kutetea haki yao wanapohisi kuhujumiwa. Kinyume na maandamano ya miaka ya nyuma, haya yanaongozwa na Wakenya wenyewe, na sio wanasiasa.
-
Udhaifu wa Maamuzi ya Bunge
Mwenendo wa Wabunge wetu wakati wa kufanya maamuzi muhimu yanayomhusu Mkenya wa kawaida ni dhihirisho tosha la maamuzi duni ambayo huwa tunafanya Bungeni. Haimhitaji mpigakura kumtumia arafa Mbunge ama kuandamana ili wafanye maamuzi bora ya kutuwakilisha. Tujifundishe kitu, inatupasa kufanya maamuzi bora debeni siku za usoni.
-
Junior Starlets Wafuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake Chini ya Miaka 17
Heko kwa Junior Starlets kwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa wanawake chipukizi chini ya miaka 17. Historia iliyoje! Junior Starlets inakuwa timu ya kwanza kabisa ya Kenya ya kandanda kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Maandalizi ya kushiriki kombe hilo yaanze sasa. -
Pengo Kubwa katika Bajeti ya 2024/2025
Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Kifedha wa 2024/2025 yalisomwa Bungeni na Waziri wa Fedha Njuguna Ndungu. Katika makadirio hayo ya jumla ya shilingi trilioni 3.99 lipo pengo la shilingi bilioni 600. Pengo hili lazima likutie wasiwasi. Unajua kwa nini?
-
Kuwajibika kwa Mafao ya Rais Mstaafu: Je, Jopo ni Lazima?
Suala la mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta halistahili jopo, ni suala ambalo sheria za nchi zinatosha katika kulitatua.
Kenyatta anauliza kipi kilifanyika kwa mgao wake wa bajeti kwa miaka miwili, kwa mfano, haihitaji jopo kujibu swali hilo. -
Heko Rais Ruto Kwa Kushughulikia Malalamishi ya Kenyatta
Suala la mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta halistahili jopo, ni suala ambalo sheria za nchi zinatosha katika kulitatua. Kenyatta anauliza kipi kilifanyika kwa mgao wake wa bajeti kwa miaka miwili, kwa mfano, haihitaji jopo kujibu swali hilo.