53 episodes

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.

Kisa Changu The Standard Group PLC

    • Society & Culture

Watu mbalimbali wanasimulia wanayopitia ama kushuhudia kwa namna ya kugusa moyo, kushtua na kuliza machozi, vilevile kauli za matumaini.

    Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast

    Eliot Berry, Mwingereza anayependelea kuishi Kenya| Kisa Changu Podcast

    Eliot Berry, Raia wa Uingereza alikuja Kenya akiwa na umri wa miaka 19 alipotumwa na mamaye kutembea. Anasema alikuwa msumbufu na mara nyingi alikuwa akitoroka shuleni lakini alipofika Kenya alihisi kuwa nyumbani na maisha yake yakabadilika.
    Alianza rasmi kuishi nchini Kenya mwaka 2011 na amejifunza Kiswahili na pia Sheng kwa lengo la kutangamana na watu wa matabaka yote.
    Aidha, kwenye mitandao ya kijamii anakojulikana kama Reverend Dad, amekuwa akiwafurahisha watu kwa video za ucheshi kutumia Kiswahili. Katika Kicha Changu Podcast wiki hii tunaangazia maisha ya Reverend Dad, katika mahojaino haya na Faith Kutere.

    • 15 min
    Familia zatafuta wapendwa wao, Mombasa | Kisa Changu Podcast

    Familia zatafuta wapendwa wao, Mombasa | Kisa Changu Podcast

    Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa familia mbili kwenye eneo la Likoni katika Kaunti ya Mombasa zinaendelea kuhangaika kuwatafuta wapendwa wao ambao wanaaminika kuchukuliwa kwa nguvu na maafisa wa Idara ya Usalama.
    Tumesema na familia ya Bakari Mwanyota mwenye umri wa miaka 38 wa Mtaa wa Consolata na familia ya Tunu Said mwenye umri wa miaka 55. Familia hizo mbili zinasema wapendwa wao walichukuliwa kwa nguvu mwezi Februari na Julai, 2021 na hadi sasa hawajui waliko.
    Robert Menza amezungumza na familia za wawili hao katika makala haya ya Kisa Changu Podcast.

    • 20 min
    Mlinzi wa Binafsi Aliyeponea Kifo | Kisa Changu Podcast

    Mlinzi wa Binafsi Aliyeponea Kifo | Kisa Changu Podcast

    Bernard Kibet amekuwa bawabu kwa zaidi ya miaka kumi. Japo kazi hii imemwezesha kuilisha familia yake na kuwasomesha watoto wake ni kazi ii hii ambayo imemsababishia machungu ambayo hatawahi kusahau kamwe.
    Kibet anasema wakati mmoja genge la majambazi lililokuwa kwenye eneo lake la kazi liliiba na kumpiga risasi kichwani bila kukusudia. Waliomwokoa walimchanganya na mili minane bila kukusudia tayari kupeleka katika hifadhi ya maiti lakini kwa bahati nzuri aliokolewa. Ilikuwa aje?
    Martin Ndiema amefanya mezungumzo na Kibet katika Podcast hii.

    • 12 min
    Kijiji Cha Walemavu, Bungoma | Kisa Changu Podcast

    Kijiji Cha Walemavu, Bungoma | Kisa Changu Podcast

    Kijijini Namawanga, kilichoko eneo la Busunu Kaunti ya Bungoma kuna takriban familia 27 hivi. Kisicho cha kawaida ni kwamba katika kila familia kuna angalau mtoto mmoja mwenye ulemavu. Wapo waliozaliwa wakiwa na matatizo kuona, kuna wengine waliozaliwa bila viungo vya mwili kama vile miguu na mikono na wengine wanaugua ugonjwa wa seli-mundu yaani sickle cell.
    Duncan Waswa amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na baadhi ya wakazi. Haya hapa masimulizi yao ya kuhuzunisha.
    Duncan Waswa amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na baadhi ya wanakijiji. Haya hapa masimulizi yao ya kuvunja moyo.

    • 12 min
    Pesa za HELB ziliishia kampeni | Kisa Changu Podcast

    Pesa za HELB ziliishia kampeni | Kisa Changu Podcast

    Stephen Kwisis, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Laikipia ana machungu baada ya kukosa kufaulu katika azma yake ya kuwa mbunge wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka 2022. Kwisis mwenye umri wa miaka 24 anasema alitumia fedha za mkopo wa kufadhili elimu ya chuo kikuu, HELB kufanyia kampeni.
    Mwanasiasa huyo mchanga aliyekuwa akikabiliana na washindani 13 alipata kura 156 pekee. Amezungumza na Duncan Waswa kuhusu masaibu yanayomkumba katika masimulizi yafuatayo.

    • 6 min
    Kisa Changu Podcast: Mahangaiko ya wanasiasa wanawake wenye ulemavu; Sehemu ya 1

    Kisa Changu Podcast: Mahangaiko ya wanasiasa wanawake wenye ulemavu; Sehemu ya 1

    Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Machakos Rose Museo ana ulemavu. Museo aliyepata ulamavu huo ulemavu kufuatia ajali mwaka 2007 anasema changamoto hiyo haikumzuia kufanikisha ndoto yake ya kuwa kiongozi. Rose Mukonyo amezungumza naye anafafanua zaidi huku akiwashauri wanawake wengine wenye ulemavu kwamba wanaweza.

    • 24 min

Top Podcasts In Society & Culture

I Said What I Said
Carousel Network
The HonestBunch Podcast
Glitch Africa
So Nigerian
Dami Aros
Menisms
Madeaux Podcasts
To My Sisters
Courtney Daniella Boateng & Renée Kapuku
Life Uncut
Brittany Hockley and Laura Byrne