19 avsnitt

Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.

Meza Huru Meza Huru

    • Musik

Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.

    Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18

    Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18

    Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo. 
    nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)? 
    Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo?
    Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare 😁
    Meza Huru imekaa nao na kupata simulizi ya maisha yao ya muziki na amini kwamba, inavutia sana. 
    Jumuika nasi mezani kuwasililiza 😊, Karibu 
    #MezaniNaMandojoNaDomokaya 
    #MezaHuru

    • 2 tim. 30 min
    Mezani na KIBACHA Part II

    Mezani na KIBACHA Part II

    Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha

    Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.

    Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. 

    Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.

    Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.

    Mwamba huyu hapa 😊

    #MezaniNaKBC 

    #MezaHuru 

    • 1 tim. 41 min
    Mezani na KIBACHA Part I

    Mezani na KIBACHA Part I

    Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha

    Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.

    Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa. 

    Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.

    Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.

    Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa 😊

    #MezaniNaKBC 

    #MezaHuru 

    • 1 tim. 39 min
    Mezani na DOLO #15

    Mezani na DOLO #15

    Anaitwa DOLOMOI FRANCIS, kwa jina maarufu anafahamika kama DOLO. Ni moja ya waasisi wa kundi la Wachuja Nafaka na Wanaume TMK. 
    Kutoka maeneo ya TEMEKE. 
    Tumepata bahati ya kukaa naye mezani na ametupitisha kwenye safari yake ya muziki. Kuanzia akiwa hajawa Dolo, 
    mpaka hivi sasa akiwa bado anapeperusha vyema bendera ya TMK.
    #MezaniNaDolo 
    #MezaHuru

    • 2 tim. 9 min
    Mezani na KR MULLAH #14

    Mezani na KR MULLAH #14

    KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family

    Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi

    Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk.

    Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo

    Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba.

    #MezaniNaKakaRashidi 

    #MezaHuru

    • 1 tim. 30 min
    Mezani na RAS INNO #13

    Mezani na RAS INNO #13

    Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania. 

    Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo.

    Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae

    Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia,

    Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu.

    #MezaniNaRasInno 

    #MezaHuru 

    Anchor - https://anchor.fm/meza-huru

    Google podcast -  https://podcasts.google.com/feed/aHR0... 

    Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683

    Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r... 

    Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797

    Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2... 

    Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087

    Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru... 

    YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...   



    Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10... 

    Twitter - https://twitter.com/MezaHuru

    • 2 tim. 6 min

Mest populära poddar inom Musik

P3 Musikdokumentär
Sveriges Radio
Hemma hos Strage
Lejon Media
Inget Här Är Byggt För Oss
Rasmus Arvidsson
SkivSnack
Stefan Sundberg
100 Best Albums Radio
Apple Music
Mästerverken i P2
Sveriges Radio