SE6EP11 - Salama Na Dula Makabila | MZEE WA NDERE…MO Salama Na

    • Entertainment News

Listen on Apple Podcasts
Requires subscription and macOS 11.4 or higher

Abdallah (sijui jina lake la katikati ambalo amekataa kutuambia mimi na wewe just in case tutataka kumroga) Mzee aka Dulla Makabila ni kiumbe special sana. Na nasema haya kwasababu binafsi nilishawahi kupata wasaa wa kukaa naye kwa zaidi ya mara mbili kabla ya hiki kikao chetu hiki.

Kutoka kwenye familia za kimaskini na ki dini, anakumbuka jinsi Marehemu Mzee wake alivyokua anawakumbusha wajibu wao na kuzingatia dini, yeye pia anaamini kama bado Mzee wake angekuwepo basi yeye kufanya mziki ingekua ndoto tu. Ila Mama yake hana neno na support ambayo anampatia ni ya asilimia 100. Maisha waliyokua wakiishi zamani si ambayo wanaishi sasa na kama Mzazi hana budi kujivunia mahangaiko na nguvu ambazo Dulla amewekeza kwenye usanii wake.

Anakumbuka sana maisha ya zamani na jinsi ambavyo alianza, yeye anasema pengine ilikua kama ajali tu, ajali ambayo ilipangwa na Mwenyezi Mungu, na ilipotiki basi ilitiki mazima. Ki mtaa kwa mtaa tu Dulla alikua akifanya mziki na anasema pia wakati mwengine alikua anaambiwa hawezi ila hayo maneno hayakuwahi kumkatisha tamaa hata siku moja. Mtoko wake wa kwanza ilikua nyimbo ya kuisifia klabu yake ya Yanga (ya wakati huo, maana hivi karibuni alirudi kutengeneza wimbo wa klabu yake ya sasa ya Simba 😄.) Pengine kuachwa kwa verse yake kwenye tungo hiyo ndo ilifanya awe na maamuzi hayo ila Mimi nilivyokutana naye kwa mara ya kwanza, aliniambia yeye ni SHABIKI wa Simba mzuri sana na siku moja angependa dunia ilijue hilo.

Kwa mashabiki wa mziki wa Singeli ambao sasa unazidi kuwa mkubwa hapa kwetu na In Shaa Allah dunia nzima utautambua Dulla ni Kinara na hodari kabisa, anaandika, ana ghani vizuri na anajielewa kwa kiasi chake, Dulla anaweza kuwa ni moja ya sura kuu zinazobeba mziki huu kwa sasa. Mtata, haswa linapokuja suala la mahusioano na heshima binafsi, mambo yake mengi yako hadharani ikiwa pamoja na imani yake ya mambo ya kishirikina.

Hapa karibuni kilikua na story yake juu ya mahusioano yake na WCB ambao kwa maisha ya mwanzo ya Dulla tuliona ndo kama walikua rafiki zake wa karibu lakini siku za karibuni mambo kama yamekua na mkorogo kidogo.

Kikao hiki kiliongelea heshima, mitihani, mwanzo wa kazi, mapenzi na imani na matumaini yangu uta enjoy pia.

Love,
Salama.