34 episodes

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Salama Na YahStoneTown

  • Entertainment News
  • 4.5 • 289 Ratings

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  Ep. 34 - Salama Na DOGO JANJA | YENTE

  Ep. 34 - Salama Na DOGO JANJA | YENTE

  Nakumbuka mara ya kwanza kukutana na Dongo Janja enzi hizo akiwa mtoto kabisa na hata kwenye viduara vyetu alikua anakaa mbali maana havikua vinamhusu. Kukua kwake kwenye macho yetu wakati mwengine inatufanya tuwe tunadhani kama tunamfahamu sana au tuna haki sana ya kujua kila kitu kwenye maisha yake na kumhukumu kwa maamuzi mengine ambayo sisi kama sisi hatujayapenda, tunasahau kama hayo ni maisha yake na ana haki ya kujifunza kwa kukosea na kukaa sawa kama ambavyo yuko sasa.

  Jina la serikali ni Abdulaziz Abubakar Chende aka JANJARO, sio DOGO JANJA tena, sasa ana miaka 25. Unakumbuka mara ya kwanza kumuona au kusikia kuhusu yeye? Basi toka siku hiyo mambo yamebadilika sana sana. Ya ki maendeleo na ya ki binafsi kama binadamu. Kwasababu mimi ni Dada yake ilibidi turudi nyuma kidogo maana sijamuona siku nyingi so nilitaka ku catch up wazungu wanasema. Kwanza nimeona kwa ukaribu kama hana tena ile sura ya ki toto na confidence yako ni ya mtu aliyepitia kadhaa na akajifunza juu yake.

  Khadithi kuhusu siku ya kwanza alipofika hapa jijini Dar es Salaam, alifikaje? Alikuja kufanya nini? Je yeye kujulikana akiwa na umri mdogo anadhani kumemtegenezea maisha yake au kumemzigua? Mahusiano yake na Rais wa Manzese, TIp Top Connection na pia kuhusu elimu ambayo kwa kipaji chake ni kama alikua akiipata kwa bei nafuu tu. Ilikuaje mpaka akashindwa kabisa kumaliza? Miaka si mingi pia alimpoteza Baba yake mzazi ambaye kwa mujibu wa Abdul walikua ni watu wa karibu sana na kifo chake kilimgusa ki vyengine sana.

  Kuna suala la ndoa ambayo wengi wetu tulidhani ilikua kama geresha ivi au Kiki kama wasemavyo watoto wa mjini. Kumbe ilikua na ukweli kabisa na wawili hao walikua wameshibana mpaka wakaona waoane tu. So nini kilitokea hapo mpaka sasa hawako pamoja? Kwanini anadhani ilikua habari kubwa ambayo ilikua Ina nenda rudi nyingi? Je ana majuto yoyote kuhusu suala hili kwa ujumla yeye kama yeye? Na vipi kuhusu maisha yake ya sasa? Ana furaha? Aliye naye anadhani ndo wa kweli kwake? Pia kuna suala la muziki na umaarufu na suala la Mama yake na mahusiano yao kama Mama na mtoto wake.

  Janjaro kakua na nimeliona hilo kwa jinsi tu anavyojibeba na anavyojielewa, hana papara katika kujibu maswali na kutafakari vitu, na kwa asilimia 100 naamini limetokana na kukaa na Madee karibu kwasababu nimeambiwa katika watu wenye busara na maamuzi ya kuto kukurupuka kwenye vitu basi Rais wa Manzese naye yumo. Napenda kumpogeza kwa kukuza na kuendelea kumsuka kijana awe kati ya binadamu bora. Nakutakia utazamaji mwema kwenye kipindi hiki na yangu matumaini utajifunza jambo na uta enjoy pia.

  Love,
  Salama.


  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 48 min
  Ep. 33 - Salama Na SPESHOZ | BOBBIN

  Ep. 33 - Salama Na SPESHOZ | BOBBIN

  Jeffrey Jessey Mmbungu ni kijana wa ki Tanzania ambaye aliangaliaaa wapi pa kupata rizki ili mambo yake yamuendee kama anavyopenda na akafanikiwa kwa asilimia nyingi sana huku akipata pointi nyingi za kujiamini na kuthubutu kutoka kwangu. Ni rafiki yangu kwa miaka zaidi ya minne sasa, tunagombana tunapatana, kisha tunagombana tena alafu tunapatana, kisha tunagombana kwasababu ya Manchester United alafu tunapatana tena kabla hatujagombana tena kwasababu ya suit yangu kutotobolewa mashimo ya vifungo vya pembeni ya suruali yangu, au pengine kwasababu nlikua nataka kumpiga kirungu akachomoa, au pengine simu yake haipatikani kiiiila wakati wakati yeye ni mtu ambaye hatakiwi simu yake iwe na mizinguo hiyo, ilimradi ni vita tu kati yetu. Najua hili lakini, kwamba wagombanao ndo wapendanao, kiasi cha heshima na kumuamini na kumu admire ni cha hali ya juu sana.

  Kuna habari zilienea kipindi flani kuhusu maamuzi yake ya kuacha kazi benki ya dunia na kuamua kujiajiri, na kwamba ni mtoto wa kishua ila anajitia umaskini ili apate huruma kutoka kwa watu na yake yamuendee. Shutuma nzito haswa kwa upande wake. Kwenye kipindi hiki nadhani hatukuacha kitu, yote yalipewa ufafanuzi na pia tukapewa elimu ya yale tusoyajua ambayo ki ukweli tulikua tunajifanya tunayajua sana. Kuanzia hilo suala la kazi mpaka alivyokutana na Cecilia Mosha aka Ceci kama ambayo Jeff humuita. Wana watoto wawili wa kiume ambao wote wamepewa majina ya wachezaji wa zamani wa Manchester United, na ndoto yake ni kuwa vijana wake hao waje kuwa wachezaji wa mpira, niko hapa kuzidisha maombi hayo ili dua za Baba zitimie nami kama shangazi niweze kwenda kukaa kwenye ‘private box’ za Wembley au OT kuangalia vijana wetu wakilisakata gozi

  So biashara wake aliingiaje huko? Na kweli alijiona akitoa ajira kwa watu zaidi ya hamsini ambao wako chini yake? Mitihani gani haswa hupata? Yeye kama yeye ana thamani ya kiasi gani? Pesa ngapi huwa anatengeneza kwenye kazi yake hii? Kuna changamoto? Nani mteja wake mkuu? Mahusiano yake na Diamond Platnumz? Walikutana wapi? Huwa Platnumz analipia nguo zake zinazotoka kwa Jeff? Ana biashara nyengine anazofanya? Na elimu yake je? Wapi alienda skuli? Alisomea nini? Kusema za ukweli maswali ni mengi ila tuli pata wa kumuuliza maana alinyoosha vizuri na nilicheka sana na ku enjoy haswa. Yangu matumaini nawe pia utafanya hivyo. Kuna ya kujifunza mengi hapa, ya kukupa muangazo pia yanapatikana humu kwa wingi.

  Tafadhali enjoy.

  Love,

  Salama.


  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 1 hr 23 min
  Ep. 32 - Salama Na Riyama | UTAKWENDA UTARUDI

  Ep. 32 - Salama Na Riyama | UTAKWENDA UTARUDI

  Riyama Seleman Ally, malkia wa kazi aifanyayo na kila alitilialo msisitizo hulifanya kwa asilimia 100, hata kama akichelewa kama pengine alivyochelewa kupata heshima yake na malipo yake anayostahili, kama ambavyo anapata sasa au ambayo anapata maana safari bado ni ndefu. Na kwa mazungumzo haya nilofanya naye huo ndo muelekeo na ndo nia na madhumuni. Sote tunajua PENYE NIA PANA NJIA, so kazi ni kwetu.

  Mzaliwa wa Unguja Tanzania, kakua katika familia ya kidini na malezi bora ila kwa mujibu wa maongezi yetu haya yeye alipenda zaidi kuwa muimbaji, kitu ambacho Mwenyezi Mungu mtoa vipaji hakumjaalia kipaji hicho na uzuri ni kwamba aligundua mapema na akafanya ustaarabu wa kutafuta kitu chengine cha kusogeza maisha yake.

  Ule usemi wa Mungu anakupa unachostahili na sio unachotaka hapa umetulia mahala pake. Imagine kutoka kutaka kulazimisha kuwa Khadija Kopa (ndo muimbaji anayempenda zaidi) na kuwa mmoja wa wasanii wa filamu hodaaari kabisa hapa kwetu na kama SI NDIO MUIGIJAZI BORA WA KIKE WA FILAMU hapa Tanzania.

  Heshima zangu za dhati zinaenda kwake kwa kukubali kuja kuongea nami na kunielezea kinaga ubaga juu ya ukuaji wake, maamuzi fulani fulani ambayo ashawahi kufanya maishani mwake. Elimu yake, alisoma? Shule ipi? Alikua mwanafunzi wa aina gani? Kuhusu familia? Ana mtoto? Na pia tulizungumzia filamu na maisha yake kama kioo cha jamii. Majibu yalikua mazuri na marefu na kwa hilo namshkuru sana yeye kwa kuweza kuja na kuongea nami huku mume wake mpendwa akiwa anamgojea kwenye parking lot.
  Yangu matumaini uta enjoy maongezi haya kama nami nilivyo enjoy kuongea naye.

  Love,
  Salama.  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 1 hr 15 min
  Ep. 31 - Salama Na GOODLUCK | WASTAHILI SIFA

  Ep. 31 - Salama Na GOODLUCK | WASTAHILI SIFA

  Sifa za Bwana inabidi zisemwe kwa zawadi hii alotupa sisi wanadamu, tunamshkuru sana kwa kipaji cha Goodluck Gosbert na tunamshkuru pia kwa kumfanya ni wa kwetu, kutoka nchini kwetu, kwamba ni mwenzetu. Kwa kweli binafsi nimependa sana na najivunia yeye.

  Utamu wa sauti yake nadhani cha kwanza wengi tulikipenda sana, baada ya kumsikia tu, kama ilivyokua mara ya kwanza anataka kujifunza kupiga gitaa akaenda kanisani, na akaskika akiimba na wana kwaya wa kanisa hilo na wakampenda toka siku hiyo mpaka leo, ndo ilivyokua kwetu pia naamini. Kipaji chake cha pili ni utajiri wa mashairi, kipaji kikubwa cha kuandika na wakati naongea nae alitaja baadhi ya nyimbo kubwa alizowahi kuandika ambazo ni za ‘kidunia’ na pia kama zilimtia matatani kiasi maana imekua ikileta tafsiri nyengine kwa baadhi ya watu ambao wao wanamuona kwenye njia nyengine. Lakini hutunga nyimbo zake mwenyewe na pia anawaandikia wengine na katika hizo zinajumuisha kazi zake za nzuri tu alizowahi kufanya ambazo zilitufanya mimi na wewe tumkubali.

  Kutoka kuwa mtoto pekee wa kiume nyumbani, na pia kukuzwa na Mama tu ambaye kwa mujibu wa Goodluck alikua muhangaikaji haswa, alifanya kila aliloweza kwa kujituma kuhakikisha watoto wake wanapata elimu ili ije kuwasaidia baadae lakini pia kukua kwenye maadili yaliyo bora kwa kumpenda na kumtanguliza Mungu. Mama yake hakuamini siku ya kwanza alipojua mtoto wake ni amejiunga na kwaya ya kanisani kwake. Na yaliyofuata baada ya hapo ni historia tu. Ungana nami kumskiliza Goodluck hapa na kama ilivyo kawaida, natumai utapata mawili matatu ya kukusogeza katika maisha yako. Tafadhali enjoy.

  Love,

  Salama.  Follow:

  Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

  Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

  Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown


  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 1 hr 4 min
  Ep. 30 - Salama Na SEVEN | ROCKSTAR

  Ep. 30 - Salama Na SEVEN | ROCKSTAR

  Mtaani huwa wanasema ‘hizo kazi za wanaume’, maana mambo ya kukesha na watoto wa kiume na kuhangaika nao usiku na mchana kwa mwanamke inakua ngumu, na pengine inaweza ikaleta mambo yasiyohusu au ikasababisha vitu nyengine visiende kwasababu tu anayefanya hiyo kazi ni MWANAMKE. Ila kwa Christine ‘Seven’ Mosha nadhani hayo maneno yalikua ndo mafuta kwenye utambi wake na aliyatumia hayo kuweza kutoa mwanga maridhawa ulioset standard ya kuvutia. Kuna kipindi na mpaka sasa, ukiwataja ma meneja wa wasanii walio hodari hapa kwetu basi la Seven litakua la kwanza kwa mujibu wangu Mimi, maana kwa kuwa mfano kwenye tasnia aliweza haswa!

  So swali ni alifikaje huko? Kabla hatujafika huko niseme ambavyo mimi namfahamu yeye rafiki yangu huyu. Kwanza hatupishani umri kabisa na pili nimekua fan wake wa muda mrefu. Napenda jinsi anavyojibeba. Napenda anavyojiweka, anavyofanya mambo yake, anavyokua bora kila miaka inavyozidi kwenda lakini kikubwa zaidi ni jinsi anavyojua mziki wetu na anavyopambana kuweka kipaji chake na cha wale anaowasisamia vizuri sana, na haswa ukimuacha akuongoze kwa mfano. Nayasema haya kwasababu nna idea ya jinsi anavyowaona watu na vipaji vyao na anavyotaka kuwanyooshea yao kwa moyo mmoja ili yao na yake yaende vizuri sana. Kwenye tasnia ambayo imejaa wanaume yeye ameweza kukaa miaka yote hiyo na huku akihakikisha heshima na maendeleo yake na anayewaongoza yakiongea yenyewe.

  Kwenye kikao hiki nilitaka kumfahamu kwa undani haswa kwa faida yetu sote lakini kama kawaida, alikua mgumu kuongelea maisha yake binafsi, na unaweza kumuelewa maana si kila mtu anapenda kuyaanika maisha yake na ya awapemdao hadharani, so tuligusia tu kwa uchache lakini tuliongelea sana mambo ya biashara, muziki, Ali, Lady JD, Ommy Dimpoz, Rockstar yake na jinsi alivyoanza na mpaka hapa alipo. Pia tuliongelea mahusiano yake na Marehemu Ruge Mutahaba na enzi hizo alivyoanza kama mtangazaji wa radio na kufikia level ya kusimamia talanta za watu wengine. Seven alianza na TID wakati huo hata usimamizi wa vipaji halikua jambo muhimu.

  Pia Seven si mtu wa kutopenda kuwa mbele mbele kama mfuko wa shati, na kwa uelewa wangu anapenda mnoo kuona watu wanakua na wanafaidika na vipaji vyao walivyopewa na Mwenyezi Mungu. Je game imekua kiasi gani? Muelekeo wetu je, tunaelekea kuzuri? Tunakua? Nini tufanye ili watu wafaidike zaidi? Kuna hayo na mwengine ya kumwaga katika maongezi yetu haya, na yangu matumaini utamfahamu zaidi Christine na kumpa heshima yake anayostahili. Tafadhali enjoy.

  Love,

  Salama.  Follow:

  Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

  Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

  Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown


  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 1 hr 7 min
  Ep. 29 - Salama Na CPWAA | KILA CHOMBO CHA WIMBILE

  Ep. 29 - Salama Na CPWAA | KILA CHOMBO CHA WIMBILE

  Wakati Parklane iko juu sana wengi wetu tulikua tunamfahamu zaidi Sumalee na ilikua haswa Sumalee na yule mwengine mwenye sauti nzito ambaye alikua anatupia tu vichombezo vya hapa na pale, hata kwenye posters za show na mambo mengine Ismail Sadiq aka Sumalee ndo alikua kila kitu mpaka pale kundi lilipovunjika na kila mmoja akaenda upande wake, hapo ndio tulipoanza kufaidi kipaji cha huyu mwanachama mwengine wa hiyo duo, jina la serikali ni Ilunga Khalifa aka Cpwaa alianza kung’ara zaidi na kupata mpaka show za kimataifa.   Yuko na swagg, anaweza kuongea kiswahili na kizungu kwa ufasaha na vile vile yeye ndo mfalme wa crank music hapa nyumbani Tanzania. Nani ambaye hakuzimia style ile ambayo Cpwaa alikuja nayo? Nani ambaye hakushangaa alipoona kipaji chake kama solo artist kipindi kile? Maana ki ukweli yeye alikua wa juu kwa juu tu kwenye kundi na zaidi mwenzake ndo alikua anafahamika zaidi? Alitushangaza sote na pia tulimpoke kwa mikono miwili.  Kama mwanafunzi Ilunga alikua ni mtu wa kupasi kwa maksi za juu haswa na nna uhakika kama insengekua mziki kipindi kile (sijaribu kusema kwamba mziki ni kitu kibaya) ila anagezingatia masomo kwa asilimia mia moja basi naamini anagekua mbaaali kuliko alipo sasa (na si kwamba alipo sasa ni pabaya). Akiwa anazunguka kwenye tour yeye na mwanaye Ismail kipindi hicho, Ilunga alikua anakosa sana masomo mpaka kuna kipindi ilikua inabidi atungiwe mtihani mwengine na aufanye peke yake maana wenzake wanakua washafanya mitihani yao wakati yeye alikua nje ya Dar es Salaam kuendeleza kipaji chake na kutoa burudani.  Sasa, nini haswa kilotokea kati yake yeye na Ismail? Kwanza haswa walikutana lini? Wapi? Ilikuaje siku ya kwanza? Na kama kundi walikua wanaishi vipi? Waliwezaje ku handle umaarufu kipindi hicho? Walikua wanatengeneza pesa? Je wazazi wake walikua wanamruhusu kukosa shule na kufanya mziki? Nani alimfanya yeye avutiwe na mziki? Ana majuto yoyote katika maisha yake? Na je Baba na Mama yake ni watu wa aina gani? Ameoa? Mtoto? Kazi gani anafanya? Pia alikua rafiki mzuri wa Marehemu Mangwair, kifo chake kimemuathiri vipi? Na industry ya sasa je anaweza kutoboa? Wallahi kulikua na maswali mengi Ila na majibu nayo hayakua nyuma, yangu matumaini na hii pia itakufunza jambo, tafadhali enjoy.  Love,

  Salama.  Follow:

  Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown

  Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown

  Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown


  ---

  Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

  • 1 hr 4 min

Customer Reviews

4.5 out of 5
289 Ratings

289 Ratings

vintotztattoo ,

BIG 5

Endelea kuwafundisha hawa watangazaji wa siku hizi kwamba ukiwa radio personality au tv personality unatakiwa uwe...
You are my role model salama.

lordreaper__ ,

unbelievable

This show is on point, I need more

iajar ,

Bravo

Dada Maria sarangi should be the next .

Listeners Also Subscribed To