100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"

    Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."

    02 MEI 2024

    02 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.
    Nchini Kenya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameathiri maelfu ya watu yakisababisha vifo na kuwaacha wengi bila makazi. Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirikaRipoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi ESCWA inasema vita inayoendelea Gaza imesababisha athari mbaya za kiuchumi na maendeleo ya binadamu katika eneo zima la Palestina.Niger mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 na ongezeko hili na wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno ELEKEZA NA ELEZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 11 min
    Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne

    Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne

    Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi. Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO). 
     

    • 2 min
    UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano

    UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano

    Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana. 
    Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP ambapo kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana” 
    Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi,  na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "
    Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia mashambulizi yanayoendelea likisema“kumekuwa na zaidi ya mashambulizi 360 kwenye vituo vyake tangu kuanza kwa vita. Mbali na makumi ya maelfu ya waathiriwa, miundombinu muhimu imeathiriwa pia, pamoja na kisima cha maji cha shirika hilo kilichoko katika jiji la Khan Younis.”
    Na ili kukarabati chanzo hicho cha maji UNRWA inasema kunahitajika kuondoa tani za uchafu ikiwemo vilipuzi na vifaa vingie vya mabaki ya virta kama vilivyobainiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada wa kutegua mabomu UNMAS nav yote vinahitaji kuondolewa kwa usalama kipande kwa kipande,."
    Na wizara ya afya ya Gaza imeonya kwamba endapo hakutopatikana usitishwaji mapigano basi Maisha ya watu yataendelea kukatiliwa zaidi na hali itakuwa janga kubwa la kibinadamu kwani hadi sasa takriban watu 34,568 wameuawa na 77,765 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7 mwaka jana.

    • 1 min
    01 MEI 2024

    01 MEI 2024

    Hii leo jaridani inaangazia hali ya kibinadamu Rafah ambapo wakimbizi wa ndani Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano. Pia inamulika udhibiti wa taka za plastiki kambini Kakuma. Makala inaangazia jamii ya watu wa asili na mashinani inatupeleka nchini DRC, kulikoni?
    Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, ambapo mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Makala inaangazia changamoto za mabadiliko ya tabianchi zilizowalazimisha wanawake wa jamii ya Kimaasai nchini Kenya kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na athari hizo ili kujikimu kimaisha.Na katika mashinani inayotupeleka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Goma Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo vurugu za kutumia silaha zinaendelea kusababisha raia kupoteza maisha yao. Katika video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi DRC, wanawake wanaomba amani irejee.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    • 9 min
    UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka

    UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka

    Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.
    Ninapoona plastiki naona fursa za ajira! Ni kauli hiyo ya Raphael Bassemi, mkimbizi kutoka DRC akiwa hapa kambini Kakuma akizungumza huku wanawake na wanaume waliovalia maovaroli na glovu na barakoa wakiokota taka. Anasema anafurahi anapoona jamii inashiriki na zaidi ya yote wanawake wasiokuwa na ajira sasa wameajiriwa, "Nilipoanza nilijikita tu kwenye plastiki, lakini ilibainika kuwa kuna takangumu nyingi za kudhibitiwa. Sasa  ninajishughulisha na aina zote za taka.”
    Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaonesha taka mbalimbali zikiwemo mifupa ya mafuvu ya ng’ombe, vyuma, seng’eng’e na kadhalika. Sasa amesharejeleza tani zipatazo 100 za takangumu.
    "Tunatengeneza rula kwa ajili  ya wanafunzi, vibanio vya kuanikia nguo, sahani za kulia chakula na vikombe vya chai na kahawa. »
    Raphael na wenzake wakiwa kwenye kiwanda hiki alichoanzisha wanapata ugeni ukiongozwa na Dominique Hyde kutoka UNCHR. Baada ya ziara, Bi. Hyde anasema, "Kilichotuvutia ni jinsi wanaweka mawazo yao kwenye hii biashara ili istawi, na pia kushirikisha jamii ipate ajira na hatimaye kipato walipie elimu na umeme. Kama sisi sote tunahitaji kazi, wao wanahitaji kazi, na wao wameanzisha hii ajira wenyewe. »
    Sasa Raphael anasema jamii ina furaha naye ana furaha na zaidi  ya yote.
    "Ninapoona wanawake  ninaofanya nao kazi wana furaha, nami nina furaha na ninatamani kuchukua hatua zaidi."

    • 1 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Serial
Serial Productions & The New York Times
Up First
NPR
Pod Save America
Crooked Media
The Rest Is Politics: US
Goalhanger
The Tucker Carlson Podcast
Tucker Carlson Network

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations