99 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN United Nations

  • News
  • 5.0 • 5 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

  Changamoto moja kubwa ya kutimiza SDGs ni vijana hawana taarifa za kutosha – Paul Siniga

  Changamoto moja kubwa ya kutimiza SDGs ni vijana hawana taarifa za kutosha – Paul Siniga

  Changamoto moja kubwa ya kutimiza SDGs ni vijana hawana taarifa za kutosha – Paul Siniga 

  Mkutano wa 26 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya madola, CHOGM, unaendelea katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali ambapo leo ni siku ya kwanza ya mkutano wa ngazi za juu. Kandoni mwa mkutano huu, imefanyika mikutano mingine ikijadili mambo kadha yakiwemo Malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs. Kijana Paul Peter Siniga yeye akiwa ni Balozi wa SDGs kupitia Umoja wa Mataifa Tanzania, amehudhuria mkutano wa vijana wa jumuiya ya madola ikiwa ni sehemu ya kupeleka ujumbe kwa viongozi hao. Paul anaanza kwa kueleza changamoto ya utimizaji wa malengo haya kwa kundi la vijana. 

   

  • 3 min
  Mradi wa maji uliofadhiliwa na IFAD waleta nuru nchini Mauritania

  Mradi wa maji uliofadhiliwa na IFAD waleta nuru nchini Mauritania

  Mabadiliko ya tabianchi yanaleta madhara kila kona ya dunia ikiwemo kupungua kwa viwango vya mvua na hivyo kuleta usumbufu mkubwa wa wakulima, mathalan nchini Mauritani kiwango cha mvua kilichokuwa kikinyesha miaka 30 iliyopita sasa wanapata robo tu ya kiwango hicho hali iliyowatesa wakulima na wafugaji lakini mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD umewanusuru kwa kuwahakikishia maji mwaka mzima. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Anold Kayanda.

  (Taarifa ya Anold Kayanda)

  Mauritania, nchi inayotambulika kuwa na majangwa na ukame kwa muda wa miaka mitatu mfululizo imeshuhudia upungufu mkubwa wa mvua kutokana na ukame wa mara kwa mara.

  Hali hii imesababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kilimo kwa kuwa wakulima wengi wanategemea mvua kwa ajili ya kilimo ambacho hatimaye huwapatia chakula na cha ziada wanauza kwa ajili ya kipato.

  Mratibu wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD nchini humo Ahmed Ould Amar anasema “mbali na changamoto hiyo lakini wakazi wa Ukanda wa Kusini wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kilimo kwa kuwa eneo hilo ni la mteremko na mvua na mafuriko vimemomonyoa udongo, huku ukosefu wa maji na uhaba wa chakula vikileta migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambao mifugo yao ilikuwa ikiingia katika mashamba ya wakulima na kula mazao.”

  Ili kutatua changamoto hizo IFAD kwa kushirikiana na serikali ya Mauritania wamefadhili mradi wa maji unaowezesha wakulima kuendesha shughuli zao mwaka mzima bila wasiwasi kama anavyoeleza Zeinebaou Binti Mohamed mkulima kutoka mkoa wa Ghidimakha

  “Mradi huu unatusaidia kutupatia mashine za umwagiliaji, pampu za maji na matangi ya kuhifadhi maji, mbegu za mazao na uzio ili mifugo isiiingie katika mashamba yetu. Pia wametupatia mabomba makubwa ya maji na haya yanatusaidia katika kilimo na tunawashukuru kwa hilo.”

  Wakati wananchi wa Mauritania wakifurahia mradi huu Umoja wa Mataifa umesema ni muhimu kila eneo la dunia kuhakikisha wanasaidia kupata suluhu za kudumu za changamoto za maji kama nchini Mauritania kwa kuwa watu bilioni 2.3 duniani kote wanakabiliwa na upungufu wa maji hali inayosababisha njaa na shida kubwa.

  Umoja wa Mataifa pia umetahadharisha kuwa ifikapo mwaka 2050 robo tatu ya watu wote duniani wanaweza kuathiriwa na ukame.

  • 2 min
  Sanaa yatumika kuhamashisha amani DRC

  Sanaa yatumika kuhamashisha amani DRC

  Huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wasanii vijana wanatumia sanaa ya upakaji kuta rangi kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii kuachana na ghasia sambamba na kueneza kauli za chuki. Taarifa hii iliyoandaliwa na Esther Nsapu wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko DRC inasomwa studio na Assumpta Massoi.

  (Taarifa ya Assumpta Massoi)

  Nats..

  Mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini, kuta za baadhi ya maeneo zimechorwa picha zenye ujumbe tofauti tofauti ! Mathalani Tusitupe mawe na tusichome matairi kwenye barabara ! Tunatakataa Ujeuri ! Tulinde na Tukinge mazingira. !

  Ujumbe katika kuta hizi ni sehemu ya mradi wa Vijana Pamoja Jenga Nchi, au VIPAJI uliozinduliwa mwezi uliopita na Taasisi ya Sanaa ya Kivu, AKA, taasisi ambayo ni kituo cha tafiti za kitamaduni na ujasiriamali na makao yake ni Goma.

  Sanaa inaendelea ya uchorani ambapo AKA imekaribisha vijana wapendao sanaa hii kutoka mji wa Bukavu, jimboni Kivu Kusini, halikadhalika vijana kutoka mikoa jirani ya Rwanda kama vile Gisenyi.

  Mradi lengo lake ni kusongesha amani, kuondokana na ghasia, elimu ya uraia na kulinda mazingira.

  Thierry Vahwere Croki, mwenye umri wa miaka 37 ni miongoni mwa waanzilishi wa mradi huu na amekuweko kwenye sanaa hii kwa miaka 17 sasa anafurahi kufanya kazi na vijana kwa sababu vijana wanajipatia kipato na kwamba,

  (Sauti ya Thierry Croki)

  “Hawana muda wa kwenda kuombaomba au kubeba silaha kwa sababu wana kazi na wana kitu cha kufanya.”

  Na zaidi ya yote mradi ni muhimu kwa mji wa Goma wenye wakazi takribani milioni 2 kwa kuwa,

  (Sauti ya Thierry Croki)

  “Tunauvisha Goma vazi jipya! Michoro hii inapendezesha na siku hizo na teknolojia vijana wengi wana simu janja wakipita wanasoma ujumbe, wanapiga picha na kusambaza pia ujumbe kwa familia, ndugu na jamaa, shuleni na hivyo tunachora picha na kujisogeza karibu na jamii, vijana na wakati huo huo kuvunja fikra potofu.”

  24 Juni 2022

  24 Juni 2022

  Hii leo jaridani, Leah Mushi anamulika:

  1.    Chuo cha sanaa Kivu, AKA huko Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na harakati za kutumia uchoraji wa kuta ili kuepusha vijana na ghasia sambamba na kulinda mazingira.

  2.    Nchini Mauritania IFAD imeleta nuru kwa wakulima waliokosa mvua

  3.    Makala tunakwenda Kigali, Rwanda kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Madola ambako kijana Paul Siniga kutoka Tanzania amewakilisha vijana.

  4.    Mashinani, tunakwenda Kilifi nchini Kenya kumulika harakati za kulinda baharí, Karibu!

   

  • 11 min
  Jifunze Kiswahil: Methali- Ukipewa shubiri, usichukue pima

  Jifunze Kiswahil: Methali- Ukipewa shubiri, usichukue pima

  • 51 sec
  23 Juni 2022

  23 Juni 2022

  • 12 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
5 Ratings

5 Ratings

Top Podcasts In News

The New York Times
The Daily Wire
NPR
The Daily Wire
Crooked Media
New York Times Opinion

More by United Nations

United Nations
United Nations
United Nations
United Nations
United Nations
United Nations