43 episodes

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Siasa na Gumzo Standard Media

    • History

Mijadala, uchambuzi na gumzo la kusisimua kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

    Hasla Akosa Usingizi Kufuatia Gharama ya Maisha | Siasa na Gumzo Podcast

    Hasla Akosa Usingizi Kufuatia Gharama ya Maisha | Siasa na Gumzo Podcast

    Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu?
    Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha kutoka Marekani kupiga jeki Hazina ya Hustler Fund. Umesaidika na fedha hizo? Kiwango ulichoomba kimeongezeka?
    Pia kuna masaibu ya Cherera4. Unasemaje kuwahusu? Tribunal iendelee kuwachunguza au unasema leave them alone jinsi anavyotaka Baba?
    Wanahabari wetu Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki gumzo na wananchi.

    • 11 min
    Uteuzi wa Makatibu Wazua Tumbojoto, Raila akitaka Waluke Kuachiliwa | Siasa na Gumzo Podcast

    Uteuzi wa Makatibu Wazua Tumbojoto, Raila akitaka Waluke Kuachiliwa | Siasa na Gumzo Podcast

    Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela.
    Riggy G naye hataki harufu ya Tinga Kenya Kwanza, Tinga naye anasema wewe kijana wacha kuniota kila saa mimi si rika lako. Unamshauri vipi Riggy G? Vilevile Baba anataka Waluke kuachiliwa huru. Eti kesi dhidi yake itupiliwe mbali kama za wengine. Unasemaje?
    Kuhusu njaa, unadhani serikali imeweka juhudi za kutosha kukabili makali ya njaa? Alhamisi serikali ya Kenya ilituma msaada wa chakula Somalia ilhali hapa Kenya watu, mifugo wanaangamia.
    Kwa mengi wanahabari wetu Collins Chungani akiwa Nyeri, Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wameshiriki Gumzo na Wakenya.

    • 11 min
    Gumzo la GMO; Azimio yamkosoa Hasla | Gumzo la Wiki Podcast

    Gumzo la GMO; Azimio yamkosoa Hasla | Gumzo la Wiki Podcast

    GMO imezua gumzo, Azimio wakipinga. Kalonzo naye anasema Rais Ruto analenga kuangamiza kilimo cha mimea ya kiasili. Mbali na hayo, unadhani kwamba Kalonzo anatoshea viatu vya Odinga katika upinzani?

    Baba naye angali anamlaumu Chebukati na mataifa ya kigeni, kwamba yaliingilia uchaguzi wa Kenya! Unasemaje? Si hayo tu, Azimio inasema Ruto amekuwa kiguu na njia, bila kwanza kutimiza ahadi kwa Wakenya. Nawe unatathmini vipi utendakazi wa Ruto ndani ya siku 30 tangu kuapishwa?

    Wanahabari wetu William Omasire wa Nyamira, Edwin Mbugua wa Nyeri, Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanasema na wananchi.

    • 15 min
    Gumzo na Siasa Podcast; Manifesto za Ruto na Wajackoyah

    Gumzo na Siasa Podcast; Manifesto za Ruto na Wajackoyah

    Mgombea urais wa UDA, William Ruto amezindua manifesto yake akiangazia nguzo sita; kupunguza gharama ya maisha, kumaliza uhaba wa walimu, matibabu bila malipo, kujenga nyumba elfu 250 kila mwaka, kukuza biashara na kuimarisha kilimo. Ahadi hizi zinatekeleka?
    Upande mwingine Wajackoyah ameweka wazi manifesto yake akijumuisha mambo ya kiajabu. Mara atahamisha jiji la Nairobi hadi Isiolo, sijui kufuga nyoka, kuvunja sekta ya bodaboda na kuwaajiri wahudumu hao katika mashamba ya bangi na mengine mengi ya kushangaza.
    Ni manifesto gani ni nzuri?
    Halafu Kenya Kwanza inasema bandari ya Mombasa imeuzwa huku serikali ikikana.
    Kadhalika Baba ameanza vita dhidi ya Chebukati. Anasema manual register sharti itumike sambamba na electronic. Chebukati anasema la hasha. Kwa nini Baba anasisitiza ni lazima manual itumike?
    Haya yanajiri huku suala la zoning likitikisa nyumba ya Baba. Wagombea wasio maarufu wanaambiwa wajiondoe kuwapisha wenye nguvu. Benard Lusigi wa Kakamega, Edwin Mbugua wa Nyeri na Martin Ndiema akiwa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.

    • 12 min
    Siasa na Gumzo; Kabogo/Kuria walia, Sakaja atetea digrii

    Siasa na Gumzo; Kabogo/Kuria walia, Sakaja atetea digrii

    Nyumba ya Kenya Kwanza imeanza kuwaka moto. Kuria na Kabogo wataka mkutano wa dharura wakimshtumu Gachagua kufuatia madai ya udikteta. Aidha, wanadai wana-UDA wanapendelewa katika kampeni za Kenya Kwanza. Kunani? Gachagua amekuwa mzigo Kenya Kwanza? Anavutia kura au anafukuza?
    Sakata ya Sakaja kuhusu digrii nayo yamfikia Tinga na Hustler. Kelele zimechacha kuhusu kisomo cha Tinga na PHD ya Hustler. Baba awataje classmates wake.
    Bei za mafuta zimeendelea kupanda. Tuwalaumu nani? Wanahabari wetu Clinton Ambujo wa Kisumu na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia sehemu hii.

    • 9 min
    Gumzo la Wiki; Wabunge wa tumbokrasia; si demokrasia wala uwajibikaji

    Gumzo la Wiki; Wabunge wa tumbokrasia; si demokrasia wala uwajibikaji

    Bunge la 12 limevunjwa rasmi baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano. Je, limetimiza matarajio ya Wakenya ama limekuwa bunge la demokrasia ama utumbokrasia kwa kujali tu donge nono kupitia marupurupu?
    Kura za maoni nazo zinaendelea kutolewa kuelekea uchaguzi mkuu. Je, ni za kuaminika ama zinatoa taswira ya kila mwamba ngoma kuvutia kwake?
    Raila Odinga naye ametangaza manifesto ambayo imeibua gumzo kuu hasa kwa kuzitaja nguo za mitumba kuwa za wafu yaani marehemu.
    Je, alieleweka visivyo? Wanahabari wetu, Martin Ndiema wa Trans Nzoia, Clintone Ambujo wa Kisumu na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wanatupambia gumzo la wiki hii tukianza na Kiraese.

    • 16 min

Top Podcasts In History

History's Secret Heroes
BBC Radio 4
The Rest Is History
Goalhanger Podcasts
American Scandal
Wondery
Throughline
NPR
American History Tellers
Wondery
An Old Timey Podcast
An Old Timey Podcast