100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

    Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

    Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira. 

    • 3 min
    Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

    Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

    Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.
    Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Matal Amin iliyoko Baidoa nchini Somalia zaidi ya wananchi 1500 wanahaha huku na kule kurekebisha maturubai yao ambayo hasa ndio makazi yao ikiwa ni maandalizi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza muda wowote. 
    Hali ni hivyo hivyo pia katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rama cade kama anavyotueleza Kiongozi wa kambi hiyo Abdulkadir Adinur Aden anasema “Tunajiandaa na msimu wa mvua ili kupunguza athari za mafuriko, tunatumia maturubai ya plastiki kufunika makazi yetu na pia tunatumia viroba vilivyojazwa michanga ili kuzuia mnomonyoko mafuriko yatakapo tukumba.”
    Wadau mbalimbali wa misaada ya kibinadamu ikiwemo OCHA wamepeleka katika kambi hizo misaada kama vile chakula na lishe, viroba vilivyojazwa michanga, maji safi na salama pamoja na dawa mbalimbali ikiwemo za kipindupindu hata hivyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa OCHA nchini Somalia Erich Ogoso anasema mengi ya makazi hayataweza kuhimili mvua kubwa na hivyo yataharibiwa.
    “Wananchi wanaoishi katika kambi hii ya Matal Amin walifika hapa mwaka 2017 wakitokea katika mkoa wa Bay ambako walikimbia ukame, mzozo, na mambo mengine. Wamekuwa wakiishi hapa tangu kipindi hicho, mafuriko yanapokuja wamekuwa wakiondoka eneo hili na kukikauka wanarejea na sasa wanajiandaa tena na mafuriko na kuna uwezekano wakutakiwa kuondoka eneo hili.” 
    OCHA wanasema taarifa walizopokea kutoka kwa wadau wao walioko mashinani mpaka kufikia tarehe 28 mwezi Aprili mwaka huu, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Somalia zimewaathiri zaidi ya watu 124,155 na kuwaacha zaidi ya 5,130 bila makazi huku vifo vya watoto saba vikiripotiwa. 

    • 2 min
    03 MEI 2024

    03 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira. Pia tunakupeleka nchini Somalia na Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo, kulikoni? 
    Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika makala tukisalia na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, namkaribisha Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.Na mashinani tutaeleke nchini Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo kufuatili jinsi ambavyo mashirika wanavyohaha kusaidia waathirika wa miozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu

    • 11 min
    UNESCO: Waandishi wa habari 44 waliuawa wakichunguza masuala ya mazingira

    UNESCO: Waandishi wa habari 44 waliuawa wakichunguza masuala ya mazingira

    Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.
    Masuala hayo ni pamoja na jinsi sekta ya madini inavyochafua mazingira, migogoro ya ardhi hasa kwenye maeneo yenye maliasili na bila kusahau ukimbizi utokanao na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Kipindi hicho cha miaka 15 ni kuanzia mwaka 2009 hadi 2023.
    Guilherme Canela, Mkuu wa Kitengo cha Uhuru wa Vyombo vya Habari na Usalama wa Waandishi wa Habari, UNESCO akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema, tumebaini kuwa waandishi wa habari 44 waliuawa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kwa sababu walikuwa wanaandika habari kuhusu mazingira.
    Akinukuu ripoti hiyo mpya itokanayo na utafiti utafiti uliohusisha waandishi wa habari 905 kutoka nchi 129 zikiwemo za bara la Afrika, Bwana Canela anasema katika hao 44 waliouawa, ni kesi tano tu ndio wahusika walipatikana na hatia na kuhukumiwa.
    Asilimia 70 ya waandishi wa habari waliohojiwa walikumbwa na ghasia wakichunguza masuala ya mazingira kama vile uchafuzi utokanao na uchimbaji madini na migogoro ya ardhi. Asilimia 41 kati yao hao walipata mashambulio ya mwilini wengi wao wakiwa wanaume, ilhali asilimia 60 walishambuliwa mtandaoni, walengwa wengi wakiwa ni wanawake. Bara la Afrika lilibeba theluthi mbili ya matukio ya mashambulizi ya mwilini.
    Kama hiyo haitoshi, asilimia 25 walikabiliwa na kesi za madai kwa lengo la kuwanyamazisha. Bwana Canela akisema “tuligundua pia matukio 749 katika nchi 89 ya mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari au vyombo vya habari kwa sababu tu ya kuripoti masuala ya mazingira. Na kwa bahati mbayá, watekelezaji wakuu wa vitendo hivi vya mashambulizi walikuwa ni watu wa serikali. Polisi, wanasiasa au watu wenye uhusiano na serikali kwa njia moja au nyingine.”
    Hata wakati wa maandamano waandishi wa habari walilengwa kwani ripoti hiyo ya kurasa 18 inasema katika kipindi hicho cha miaka 15 kuanzia mwaka 2019  hadi 2023, waandishi wa habari 194 walishambuliwa na matukio mengi ni barani Ulaya, Amerika Kaskazini, Amerika ya Kusini na Karibea.
    Hivyo afisa huyu wa UNESCO akatoa wito wa shirika hilo ya kwamba “katika siku hii ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu wa 2024 tunahitaji kusisitiza umuhimu wa ulinzi kwa waandishi wa habari wanaoripoti kuhusu masuala haya, kwa sababu kama si hivyo, tutabakiwa kuwa na maeneo ya ukimya, ambako huko wanajamii hawafahamu au hawajapatiwa taarifa kwa njia isiyoegemea upande wowote juu ya kile kinachoendelea kuhusiana na aina hizi za mivutano.”

    • 2 min
    Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"

    Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."

    02 MEI 2024

    02 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.
    Nchini Kenya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameathiri maelfu ya watu yakisababisha vifo na kuwaacha wengi bila makazi. Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirikaRipoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi ESCWA inasema vita inayoendelea Gaza imesababisha athari mbaya za kiuchumi na maendeleo ya binadamu katika eneo zima la Palestina.Niger mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 na ongezeko hili na wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno ELEKEZA NA ELEZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 11 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Serial
Serial Productions & The New York Times
Up First
NPR
Pod Save America
Crooked Media
The Charlie Kirk Show
Charlie Kirk
The Ben Shapiro Show
The Daily Wire

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Interviews
United Nations
UNcomplicated
United Nations
संयुक्त राष्ट्र समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य
United Nations