1 min

Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili‪ ‬ Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    • Daily News

Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.
(Taarifa ya Anold Kayanda)
Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.
Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi  na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.
WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.
Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani.
WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo.
Tags: Siku za UN, WHO, Chanjo, EPI, Wiki ya Chanjo Duniani

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
Interviews
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
UNcomplicated
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations