HATUA 6 ZA SAFARI KUELEKEA KATIKA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE

Azhar Juma
HATUA 6 ZA SAFARI KUELEKEA KATIKA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE Podcast

Hatua 6 za Safari kuelekea kwenye biashara inayojiendesha

Episodes

  1. HATUA 6 ZA SAFARI KUELEKEA KATIKA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE

    19/01/2020

    HATUA 6 ZA SAFARI KUELEKEA KATIKA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE

    *HATUA 6 KUELEKEA SAFARI YA BIASHARA INAYOJIENDESHA* *Aina ya Kwanza:* Aina hii inamhusu mtu ambaye hana aina yeyote ya shughuli ambayo inamuingizia kipato. Mtu huyu anaishi kwa kutegemea misaada kutoka kwa ndugu, marafiki,na jamaa. *Aina ya Pili* : Aina hii inamhusu mtu ambaye anabiashara ila kipato chako ni kidogo. Kipato hichi cha biashara hakimtoshelezi kukidhi mahitaji ya maisha yake ya kila siku kiasi cha chini kabisa. Pia biashara yake, haionyeshi dalili yeyote ya kukua. Kwa sababu kipato hakitoshi mara nyingi naye anakuwa wakati mwingine anategemea ndugu na jamaa kufidia pengo la kipato. *Aina ya Tatu* : Huyu ni mtu ambaye kipato chake ni kidogo, lakini kutokana na juhudi zake, kipato chake kinaongezeka siku hadi siku. Changamoto ni kuwa, kila kipato kinapoongezeka, pia matumizi yanaongezeka. Kwa hiyo matumizi yake huwa ni makubwa kuliko mapato siku zote. *Aina ya Nne:* Huyu ni mtu biashara yake inafanya vizuri, na kipato chake ni kizuri. Uzuri wa mtu huyu ni kwamba kipato anachopata, ni sawa na matumizi. Kwa maana nyingine kila faida anayopata, anaitumia yote katika matumizi yasiyohusu biashara. Mara nyingi mtu huyu na nafasi kubwa ya kwenda juu zaidi, pia ananafasi kubwa zaidi ya kwenda chini kama biashara itayumba au matumizi yakaongezeka ghafla. *Aina ya Tano:* Huyu ni mtu biashara yake inafanya vizuri, na kipato chake ni kikubwa kuliko matumizi. Kila inapofika mwisho wa mwezi, anauwezo wa kuigwa faida. Kiasi cha faida anatumia katika matumizi yasiyokuwa ya kibiashara, na baadhi ya pesa anaweza kuweka akiba kwa lengo la kukuza biashara baadae. *Aina ya Sita:* Huyu ni mtu biashara yake inafanya vizuri sana. Inatengeneza faida kubwa, na anauwezo wa kuweka akiba kwa lengo la kukuza biashara. Kizuri zaidi ya yote, mtu huyu ametengeneza mfumo wa biashara. Badala ya mwanzilishi wa biashara kuiendesha yeye mwenyewe kila kitu, MFUMO ndo unaendesha biashara hii. Mtu huyu ana uwezo wa kusafiri kwa muda mrefu kwenye biashara yake bila kuadhiri utendaji wa biashara.

    7 min

About

Hatua 6 za Safari kuelekea kwenye biashara inayojiendesha

To listen to explicit episodes, sign in.

Stay up to date with this show

Sign in or sign up to follow shows, save episodes and get the latest updates.

Select a country or region

Africa, Middle East, and India

Asia Pacific

Europe

Latin America and the Caribbean

The United States and Canada