Salama Na

Salama Na
Salama Na

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

  1. SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE

    02/03/2023

    SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE

    Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea shurba kutoka kwake. Mfaume ni kama wengi wetu ambao tumetokea katika familia za kawaida tu ambayo malengo ya wazazi wetu kwetu ni kuhakikisha unasoma ili uweze kupata kazi nzuri na uje uwasaidie wao na Ndugu zako utakapokua mkubwa, vile vile mambo ya michezo ni kawaida maana kama mtoto unapokua unakua shuleni na mtaani ni lazima kunakua na kucheza, chochote ambacho kiko mbele lakini zaidi huwa ni mpira wa miguu kwa Kaka zetu ingawa sasa dunia imebadilika kiasi, siku hizi hata watoto wa kike kucheza soka ni jambo la kawaida tu na kwa hilo napenda sana. So kwa Mfaume ni kama kwetu wengine tu, alianza kwa kucheza mpira lakini baadae interest yake ikatoka kutoka kwenye mpira na kuhamia kwenye ngumi, kwa wazazi wake huo ulikua mitihani hasa. Kwa mzazi kukuona mtoto wake akichezea vitasa mara kwa mara haliwezi kuwa jambo la kupokelewa kwa mikono miwili ndani ya nyumba, mtoto anarudi nyumbani kutoka kujifua nae anakua kafuliwa kwelikweli au akijua kwamba una pambano na mwamba flani aliye shindikana ndo hofu inapanda mpaka juu ya dari na inaeleweka kwanini inakua hivyo na kama mpaka sasa hujaelewa au hujaipatia picha basi mwenzetu huna moyo lol. Alinipa story moja kwenye maogezi yetu haya kuhusu Mama yake, ananiambia kuna wakati alikua na mechi na bondia ambaye alikua anaongea sana, anajisifia na kumtishia sana maisha yake, kwamba atamchakaza vibaya sana tena mbele ya Mama yake, na aliyasema hayo akijua fika Mfaume huwa anaenda na Bi Mkubwa wake kwenye fight zake zote za ndani, ananiambia Mama yake aliogopa sana, alimsihi sana lakini kwa jitihada zake na maguvu ya Allah aliweza kumaliza mchezo wake huo vizuri tu. Mabondia ni watu ambao wana roho za kipekee sana, unaweza ukamkuta mtu akiwa uliongoni anatoa dozi nzito kwa mpinzani wake ukadhani ni mtu mwenye roho mbaya sana, lakini ukimkuta nje ya ulingo na kwa watu wake utajua ni mtu wa aina nyengine kabisa. Kwa bahati nzuri nna marafiki ambao wanacheza mchezo huu wa boxing ikiwa pamoja na Mfaume mwenyewe, huwa ni watu wakarimu sana na wana mapenzi ya kweli lakini akiwa uliongoni anakua mtu mwengine kabisa, nadhani hiyo ndo tofauti ya masumbwi na michezo mengine. Yangu matumaini uta enjoy session yetu hii ya mwisho ya msimu huu na mwana huyo humble kutoka kitaa, na pia kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusogeza sehemu. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    1 h
  2. SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE

    23/02/2023

    SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE

    Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan Abdullah Turky aka Mr White ambaye na yeye akiacha ukweli kwamba alikua tajiri na mfanya biashara nzuri huko visiwani ila yeye pia alikua kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mpendae ambapo sasa Toufiq ndo anaye liongoza jimbo hilo baada ya Mzee wake kutangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu Amrehemu. Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chetu kikukuu Taufiq anakumbuka wakati wa msiba wa Mzee wake bado wa moto kabisa watu walikua wanakuja nyumbani kwao na kumshauri yeye agombee ubunge wa jimbo hilo ambalo Mzee wake alikua akiliongoza. Ikumbukwe Mzee wake Mr White alifariki kipindi ambacho wananchi walikua wanajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge wawakilishi na Rais, ananiambia kwanza aliwafukuza watu hao, wakarudi tena baada ya maziko bado Toufiq akawakatalia, baadae baada ya mambo kutulizana na kuombeleza kupungua watu ambao anawaheshimu walimfuata tena na kumueleza umuhimu wa yeye kugombea jimbo hilo. Wakamuelezea umuhimu wa Marehemu Mzee wake kwa watu wa Mpendae na kwamba kama hatofanya hivyo basi haitakua jambo zuri kwa wakazi wa eneo hilo. Ndugu Turky ilibidi akubaliane na ombi hilo na kutimiza matakwa ya wana Mpendae ambao walimpa kura nyingi za ndio. Yeye mawazo yake yalikua kwenye kuendeleza biashara zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa Mzee wake alikua alimshirikisha nayo toka akiwa mdogo. Kuweza kufanya yote hayo kwa kijana mdogo kama yeye pengine ingekua mambo mengi sana so kwa heshima wakati mambo mengine yanaenda Toufiq ilibidi aachie majukumu mengine kwa Mdogo wake wa Kiume Ndugu Abdallah Salim na Dada yake Bi Khaytham Salim Turky, ingawa bado yeye ndo Mwenyekiti wa makampuni hayo ambayo yamejikita katika biashara mbali mbali ambazo zimestawi visiwani Zanzibar na nchi nyengine. Toufiq alikuja kwenye maongezi haya akiwa na mambo yake mengine ya ki majukumu kwenye meza yake na ki ukweli hatukupata wasaa teeele wa kuweza kuyachambua mengi kama ambavyo tungependa lakini pia hatukukosa lolote jambo la lolote jambo hilo ndo tumaini letu litasaidia kwenye kukusogeza kwenye sehemu fulani katika uelewa na uchambuzi wako wa mambo. Tafadhali enjoy hiki kidogo ambacho tuliweza kukukusanyia kwenye muda mchache. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    36 min
  3. SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

    16/02/2023

    SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

    Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika. Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday 😄). So wakati ananiambia nami tayari nilikua nishamuona, basi mengine yakaendelea kwenye meza yetu adhimu. Story ya maisha yake Ndugu yetu huyu ni ya mateso mengi sana, ila kwa sasa na hata pengine mwanzo kwa adha zote hizo tunamshukuru Allah kwa hayo yote maana hayo ndo yameleta hasira za yeye kutaka zaidi, kuomba zaidi na kufanyia kazi zaidi yote ambayo anayo leo. Ally anakumbuka jinsi alivyofika Dar es Salaam mara ya kwanza na pia amenihadithia adha ya kutokua na sehemu ya kukaa hasa unapokua umekuja mjini mara ya kwanza. Alinifanya nijiulize maswali mengi sana mimi kama binadamu wa kawaida kabisa, au ambaye Mwenyezi kanibariki kwa mengi zaidi ya wengine, nini nafanya kuwasaidia ambao nawaona barabarani? Au ambao hawana uwezo wa kunifikia lakini wana uhitaji? Kanifundisha kuhusu kutochukulia maisha au nafasi ambazo tunazo kwenye maisha yetu kwamba ni kawaida tu. Ki ukweli kila ambacho tunacho kwenye maisha yetu TUNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU AMBAYE AMETUPA. Ila pia inabidi mara moja moja tujipigie makofi kwa mbali ambapo tumetoka na ambapo tumefika lakini zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu azidi kutuimarisha na kutufungulia milango ya Kheri, ZAIDI. Niamini mimi nikikuambia kuhusu kutoa, kwamba kutoa ni raha zaidi kuliko kupokea ingawa wengi wetu tunapenda zaidi kupokea, ukitaka kujua hilo jaribu kwa kuanza kumpa hata mtu zawadi ndogo tu, hata pipi ambayo alikua hategemei kama utampa au utakumbuka, sura yake itakueleza mengi hata kama yeye ataamua asikuambie kwasababu zake zozote tu. Ally alisaidiwa na mtu ambaye hata walikua hawafahamiani na kuamua kumpa hifadhi katika sehemu ambayo yeye alikua anakaa. Pengine yeye alipofanya wala hakujua kama Ndugu Ally atakuja kuwa mmoja wa ma DJ HODARI na Hyper Man bora ambae nchi hii imewahi kuona. Leo ningependa tujifunze kuhusu hilo, kuhusu kuwa kind, kuhusu kuwapa watu nafasi kwenye maisha yetu na kutosubiri malipo kutoka kwao maana pengine yanaweza yasije lakini wewe tayari unakua ushamaliza kazi yako. Yangu matumaini story ya DJ Ally Bee itakua na impact kwenye maisha yako kama ambavyo imekua kwenye maisha yangu. Enjoy and stay BLESSED. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    1 h 5 min
  4. SE7EP35 - SALAMA NA EVANS BUKUKU | STICK - TO- ITIVENESS

    09/02/2023

    SE7EP35 - SALAMA NA EVANS BUKUKU | STICK - TO- ITIVENESS

    Ulikua muda mwingi hasa umepita toka mara ya mwisho nilionana na Evans wa Bukuku na kukaa naye chini kisha tukaongea. Na ki ukweli hajawahi kuwa rafiki yangu wa karibu ila ni mtu ambaye tunafahamina na kuheshimiana. Hustle zake nazifahamu kwa ukaribu maana industry ambayo tunafanya kazi ndo hiyo hiyo kwahiyo nikama chakula, tusipokutana jikoni basi tutakutana kwenye sahani. Kama ilivyo kwa watu wengi nimekua nikimsikia kwenye radio mbali mbali katika safari yake kama mtangazaji wa vipindi mbalimbali lakini pia nimekua nikimuona kwenye majukwaa mbalimbali akifanya shughuli zake za ku host sherehe au matamasha kadhaa. Kwenye kitabu changu yeye ni mmoja wa hustlers timamu kabisa ambao Tanzania yetu inayo na mazungumzo yetu haya pia kwa kiasi kikubwa yamenipa picha nyengine ya aina ya mtu ambaye yeye ni, kwanza alikuja kwenye set na binti yake (ambaye tayari kashanizidi urefu) na inavyoonekana ni rafiki yake mkubwa maana huwa yuko naye benet mara nyingi, nadhani kwa experience yake ya kukutana na watu wengi kutoka sehemu tofauti kumemfanya naye pia ajifunze mambo flani kutoka kwao na hili ni jibu kati ya majibu ambayo niliyapata kutoka kwenye maongezi yetu. Watu wengi ambao amekua akikutana nao wanamfundisha mambo mengi na ukiachana pia kwamba na yeye amekua kwenye maisha ya ‘ki familia’ zaidi maana yeye na wazazi wake na Dada pamoja na Marehemu Kaka yake wako karibu sana. Moja ya mambo aliniambia ni jinsi ambavyo anaangalia anachokula na kujitunza yeye na mwili wake, anahakikisha anapata muda mzuri wa kupumzika na vilevile kufanya mazoezi. Anajua umuhimu wa haya yote na anayafanyia kazi. Binafsi kwanza nilitaka kujua kwanini amekua akimua kufanya vipindi vya radio vya asubuhi tu na sio wakati mwengine? Nini hasa maana ya hiyo? Majibu yake yatakufurahisha kama nawe utakua mtu wa kujifunza. Hatukuweza kuacha kumuongelea Marehemu Roy ambaye alikua ni Kaka yake, nami nilijua hiyo siku, muda wote nilikua nikidhania yeye ndo mkubwa. Roy ni mmoja wa wapishi wazuri wa Bongo Flava tamu ambayo tulianza kuipenda kwenye miaka ya mwanzo ya 2000, Roy ndo mpishi wa Mr Blue, kina Ally Kiba, kina ParkLane na wengine tele, heshima yake ni kubwa na binafsi nilitaka aliskie hilo kutoka kwangu. Na nilitaka kujua kitu ambacho kilisababisha kifo chake pia, haikua rahisi kuuliza maswali kama haya lakini pia hakukua na budi maana maua ya Kaka yake ilikua ni wajibu wake kuyapokea. Pia tulimuongelea Enika ambaye ni Dada yake pia, nilitaka kujua nini ambacho kimemfanya asifanye tena Bongo Flava, na nini ambacho anafanya sasa, na je ana furaha? Tuliongelea pia hustle yake nyengine ya comedy ambayo nayo amekua akiizingatia na kuisimamia kwa miaka sasa, hakuna comedian yoyote kwenye nchi hii ambaye kwa kiasi chochote kile hana mchango wake ndani yake, na si lazima awe amepita mikononi mwake, bali hata njia (nyingi) ambazo amewahi kuzitengeneza na ambazo anaendelea kuzisimamia. Evans mtu, tena wa watu na yangu matumaini utakubaliana nasi mara tu baada ya kuangalia au kuskiliza maongezi yetu haya. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    1 h 14 min
  5. SE7EP34 - SALAMA NA FETTY DENSA | KUTOKA UBAVUNI...

    02/02/2023

    SE7EP34 - SALAMA NA FETTY DENSA | KUTOKA UBAVUNI...

    Kwa ambao wanafuatilia mpira hapa nyumbani wanamjua mchezaji huyu mahiri wa Simba Queens lakini ambao wanafuatilla soka la wanawake hawa watakua wanaelewa uwezo binafsi na uhodari wake wa kucheza namba tofauti tofauti uwanjani ila ukimkuta kaikamata mbavu ya kulia aidha kwa Simba au timu ya Taifa ya Tanzania. Fatuma Issa ni mtu na nusu, hakuna mpenzi wa mpira au kocha yoyote wa mpira anaweza akamuacha kwenye benchi wakati team inatafuta matokeo au inataka kuwaonyesha walofika kuwaangalia vipaji ambavyo wanavyo kwenye kikosi chao. Kwa yoyote yule na kwa vyovyote vile, Fetty Densa, ni lazima AANZE. Ananikumbusha sana mimi na rafiki zangu wakati tunakua, tulikua chizi michezo hasa baada ya kufika shule ya Sekondari, ilikua kama lazima kila mmoja kuwa na uwezo wa kucheza zaidi ya mchezo mmoja ili tuwe na vikosi imara inapotokea kwenda kufanya uwakilishi wa shule, mkoa au nchi. Binafsi nilikua na uwezo wa kucheza Basketball na table tennis tu ila nina marafikia kama kina Kalova na Mboni Mntambo ambao wao walikua wanacheza Basketball, Netball, Volleyball na chochote kitakajokuja mbele ambacho kinatumia mpira kucheza lol, na tena VIZURI, sio kujazia namba tu uwanjani. Naye Fetty ni kama wanangu hao kutokana na maongezi yetu. Ananiambia hata shuleni mwalimu na wanafunzi wote katika shule yao walikua wakifahamu na kujivunia yeye sana. Akiwa anakua huko Morogoro Fetty ni ‘mtoto wa Bibi’ zaidi, yeye ndo alomlea na kumtunzia siri zake zote, na ndo alomfundisha kupika na kumkumbusha kwamba yeye ni mtoto wa kike kwahiyo alihakikisha pia mjukuu wake kwenye masuala ya kupika na usafi wake na wa nyumba pia haachi kujifunza. Bibi pia ndo alipewa ahadi ya kwamba kuna siku mjukuu atakuja kuwa mchezaji hodari kuwahi kutokea hapa nyumbani na so far, so good. Babu yake nae hakua nyuma kwenye kumsifia mjukuu wake pale anapofanya vizuri jikoni kwasababu pengine kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili ampe moyo mjukuu wake. Fatuma anatuambia humu kwenye maongezi yetu jinsi ambavyo alihangaika mkoani Morogoro kupata team ya kucheza na jinsi ambavyo alijutuma toka siku ya kwanza kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Ukimsikiliza kwa makini utagundua kama ni mtu mwenye mawazo ya mbele kuliko hata umri wake, hiyo inamsaidia pia inapofika wakati wa kufanya maamuzi anapokua ndani na nje ya uwanja. Unaweza ukajiuliza kwa kipaji chake na ujuzi wake kwanini hachezi nje ya nchi? Kwanini amekua Simba huu msimu wake wa nne na amekua akicheza kwa kiwango cha juu sana? Densa anatupa majibu ya swali hilo ambalo nina uhakika wengi wao wamekua wakijiuliza. Mahusioano yake na Mama yake ambaye alikua mmoja kati ya wanenguaji wazuri miaka iliyopita na ndo alimfanya pia mwanae naye atake kuwa Densa (ndo jina la Fetty Densa lilikotokea). Wana mahusiono ya aina gani? Mama alilichukuliaje suala la Binti yake kuchagua soka? Na Mzee wake nae yuko wapi? Nafasi yake kwenye team yake? Team ya Taifa je? Experience ambayo waliipata Morocco wakati Simba ilipoenda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Africa? Vipi kuhusu mpira wa miguu wa wanawake hapa nyumbani? Pesa ipo? Muelekeo je? Haya maongezi ni moja ya maongezi bora ambayo nimeshawahi kufanya na natumai yatafungua milango kwa watoto wa kike na wazazi wao wengi kuelewa na kuipambania fursa hii ambayo Dunia nzima imeanza kuielewa. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    1 h 12 min
  6. SE7EP33 - SALAMA NA MR BLUE | KHERI

    26/01/2023

    SE7EP33 - SALAMA NA MR BLUE | KHERI

    Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV. Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo. Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa. Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu. Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII. Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya. Maongezi haya yalikua yafanyike mapema tu lakini u busy wa Lil Sama na kupishana kwa ratiba ze

    57 min
  7. SE7EP32 - SALAMA NA MRISHO NGASSA | MACHACHARI…

    19/01/2023

    SE7EP32 - SALAMA NA MRISHO NGASSA | MACHACHARI…

    Mrisho Halfani Ngassa alikua top top top footballer na kwa bahati nzuri nishawahi kumshuhudia akiwa kazini kwake, tena ukimkuta kaamka vizuri basi uhakika wa burudani ni UHAKIKA . Na kipindi ambacho alikua kwenye peak yake pia kulikua na vitasa imara na magolkipa wazuri tu lakini nna uhakika kila mmoja kati yao ana la kusema kuhusu winga na forward hii machachari ambayo nchi yetu ishawahi kuona. Hakuna kitasa ambacho hakijawahi kukataa kufungua mlango muda ambao Mrisho Ngassa alikua anakuja kupiga hodi. Uzuri wake alianza kucheza mapema sana na kwasababu alikua machachari basi hata utulivu kidogo wakati anakua ulikua sio mzuri sana maana alikua na haraka. Ananiambia kwenye session hii vile ambavyo ali sign Yanga pasi na kumskiliza kocha wake kutoka Mwanza ambaye alikua anaamini kama dogo bado hajaiva, Pengine miaka miwili au mitatu ya kuendelea kujijenga ingemfanya awe bora zaidi na zaidi lakini kwenye kichwa na fikra za kijana huyu ambaye alikua na uchu wa mafanikio na kutaka kufika mjini maongezi hayo ya kusubiri yalikua ni kama kumuona sisimizi kwenye sukari alafu unamuambia asile leo badala yake ataila asubuhi, isingewezekana. Hivyo kocha akaona basi si mbaya, aende akayaone na kujifunza akiwa kazini. Yanga ndo Yanga, kwa wachezaji wote wanao chipukia au ambao ndo wanatafuta maisha kuichezea klabu kama ya wananchi ni heshima kubwa sana na zaidi kama wao ndo wametaka iwe hivyo. Kwa kijana mdogo ambaye alikua na spidi na uchu mkubwa wa kuzitia nyavuni basi klabuni pale ndo ilikua steji muafaka ya kuonyesha kipaji chake. Mrisho anakumbuka aina ya ‘vifaa’ ambavyo vilikua vinapatikana mitaa ya Jangwani. Majina makubwa na kazi ilotukuka ambayo walikua wakiifanya ilikua inajielezea. Kwa kijana kutoka mkoani kuweza kupata namba haikua kazi rahisi, ila pia haikua kazi ngumu maana ulichokisia ndo ambacho unakiona, kuanzia mazoezini mpaka anapopatiwa nafasi wakati wa mechi. Kwenye episode hii tunazungumzia aina ya mitihani na maamuzi ambayo ilikua inabidi yafanyike. Kwenye wasifu wake Mrisho amewahi kucheza kwenye team zote tatu kubwa hapa nyumbani kwetu. Kashawahi kuwa muajiriwa wa Yanga, Azam na Simba ambapo alienda kwa mkopo kutoka Azam FC, lakini pia ashawahi kupatiwa majaribio katika team kadhaa nje ya nchi yetu na wakubwa wanasema kama Ndugu yetu angekua katuliza akili na angefahamu aina ya nafasi ambayo alikua nayo kipindi kile basi yeye ndo angekua mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi pendwa ya Uingereza. Trials kwenye klabu kama Westham alipata na ofa kwenye vilabu kadhaa kutoka hapa hapa barani Afrika nazo zilikua hazikati. Sasa, nini haswa kilitokea? Wapi hasa alienda mrama? Ni kweli alikosea? Au malengo yake si malengo yetu? Au tulipokua tunamuona sisi yeye alikua hapaoni huko? Vikwazo vilikua nini? Mambo yepi hasa ndo ambayo yanaweza yakawa ndo chachu ya hayo yote kutotokea? Kama Mrisho angekua anawez kufunguka zaidi nami kwenye episode hii naamini tungeweza kupata funzo lilonyooka kwa wenetu na ukichukulia sasa mambo ndo yameanza kufunguka. Naamini angekua mwalimu mzuri kwa wake wote ambao wangetaka kusoma somo ambalo lina uhitaji mkubwa. Yangu matumaini utaweza kuelewa na kupata chochote kitu kutoka kwenye maongezi haya. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    1 h 21 min
  8. SE7EP31 - SALAMA NA KUSAH | NG’WANA AZAIZA!!

    12/01/2023

    SE7EP31 - SALAMA NA KUSAH | NG’WANA AZAIZA!!

    Kutoka zake Lushoto huku mkoani Tanga ni kijana mtanashati ambaye anajua kama amekuja town au jijini Dar es Salaam kwasababu ya kusaka pesa ili abadilishe maisha yake na ya wale ambao wamemzunguka. Na kila alikumbuka ambapo ametoka basi spidi ya kuhakikisha kalamu yake haivuji na inaandika kwa muandiko mzuri ili kila ambaye atabahatika kusoma kile ambacho yeye kakiwaza na kukiandika basi azame kwenye dimbwi lake na endelee kumsikiliza mpaka pale yeye mambo yake yatakapoenda, na kwa story ambazo amenipa basi ukinasa kwenye kitabu chake itakuia vigumu kutoka kwasababu amepanga kuwepo kwa muda mrefu sana, nia na madhumuni yake ni kuhakikisha yupo yupo sana. Kusah ananihadithia aina ya kazi ambazo ilibidi afanye wakati anakua, ilikua inabidi aende shuleni ila pia amsaidie Bi Mkubwa wake ambaye alikua anafanya kazi nyingi kuhakikisha watoto wanakula na kusoma, ikiwa pamoja na kuuza pombe za kienyeji ambazo ni haramu. Uvunjaji huo wa sheria ulikua unaifanya familia iingie matatani na anakumbuka kipindi ambacho ilikua inabidi amsaidie Mama kuficha vitendea kazi na vithibiti pale msako wa ghafla unapotokea. Kama mtoto wa kiume kwa utashi wake tu toka akiwa na umri mdogo aliona huo ulikua ni wajibu wake kuhakikisha Mama yake yuko Salama. Tukizungumzia suala zima la kazi ambayo ameichagua kufanya sasa yeye ni fundi, moja ya mafundi hodari ambao ameshaanza kujijengea na fan base yake nzuri tu, show za ndani na nje anafanya na anaelewa jinsi ya kuji brand na nini cha kufanya wakati gani na kitamfaaje. Mambo ambayo anayafanya na kuyafanikisha ni ambayo yawewachukua baadhi ya watu muda kuweza kuyakamilisha lakini yeye kwa kipindi kifupi ameweza kupiga hatua kubwa na pengine ingekua kubwa zaidi kama kusingekua na kuchelewa flani hivi ambako kulitokea baada kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Ruby ambao kwa taarifa tulizokua tunazisikia na nyengine kuzisoma mtandaoni mahusiono yao hayakua mazuri kwa afya ya kila mmoja wao. Kusah anazungumza nasi kuhusu hilo, kuhusu Mama yake, kuhusu Lushoto na plan ya maisha yake. Ameongea na sisi kuhusu kazi alizowahi kufanya maishani mwake, jinsi alivyoweza kutoka kwenye ‘toxic’ relationship ambayo ilikua ikimuumiza yeye na aliyekua partner wake. Pia anatuhadithia suala la yeye kuwa Baba kwa mara ya kwanza na mara ya pili. Tumeongelea pia mahusiano yake na Aunt Ezekiel na plan zake za huko mbele akiwa kama mwanamuziki ambaye amejikita zaidi. Yangu matumaini uta enjoy kila sekunde ya maongezi yetu haya na mawili matatu utayapata ya kukufunza jambo. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

    51 min

À propos

‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society. Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

Vous aimeriez peut‑être aussi

Pour écouter des épisodes au contenu explicite, connectez‑vous.

Recevez les dernières actualités sur cette émission

Connectez‑vous ou inscrivez‑vous pour suivre des émissions, enregistrer des épisodes et recevoir les dernières actualités.

Choisissez un pays ou une région

Afrique, Moyen‑Orient et Inde

Asie‑Pacifique

Europe

Amérique latine et Caraïbes

États‑Unis et Canada