Tangu mwaka 2015, mauaji na vifo vya wananchi vinavyotea katika vituo vya Polisi katika mkoa wa Geita vimeendela kuongezeka, vipo vinavyofanywa na watu wasiojulikana, na vingine vinafanywa na jeshi la Polisi.
Serikali na vyombo vya dola vinadai hakuna askari aliyehusika na kama yupo ni katika kujihami na kulinda usalama wao na kituo.
Storm fm, kupitia makala ya tafakari pevu imekuwa ikifuatilia kifo cha Enos Misalaba (34) Mkazi wa kata ya mganza wilayani chato mkoani Geita, mtuhumiwa aliyefariki mikononi mwa polisi.
Wananchi wenye hasira walichoma kituo cha polisi mganza, wilaya ya chato mkoani geita wakipinga uonevu unaofanywa na askari polisi wa kituo hicho, kufuatia kumkamata mtuhumiwa na kumpiga, kitendo kinachodaiwa kusababisha kifo chake.
Jumla ya timu 4 za uchunguzi ziliundwa, mbili za IGP zikiongozwa na DCI makao makuu, moja ya jopo la madaktari kwaajili ya kufanya (PM), na moja ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Lakini miezi 10 tangu kuundwa kwa kamati hizo hakuna ripoti hata moja iliyowekwa wazi, hivyo, mkala hii inajibu maswali matatu makuu…askari hawa ni akina nani? …kwanini wanapiga au kuua watuhumiwa vituo vya polisi na kwanini ripoti za uchunguzi haziwekwi wazi au kupelekwa kwa waathirika?
Information
- Show
- Published9 May 2024 at 18:50 UTC
- Length18 min
- RatingClean