100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne

    Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne

    Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.

    • 4 min
    Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”

    Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”

    • 1 min
    25 APRILI 2024

    25 APRILI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) anaeleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki. 
    Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo mwaka huu inahamasisha kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huu ili kuwa na ulimwengu wenye usawa zaidi kwani imebainika kuwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ndio wanaoathirika zaidi.Leo pia ni siku ya kimataifa ya wasichana katika tehama na mwaka huu inasherehekea uongozi ikisisitiza hitaji muhimu la kuwa na mifano thabiti ya wanawake viongozi katika taaluma ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati -STEM kwani hali ilivyo sasa kuna wanawake viongozi wachache katika maeneo hayo.  Na tukisalia na masuala ya wasichana katika tehama Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa ripoti inayoonya kuwa pamoja na faida za kufundisha na kujifunza kidigitali maendeleo hayo ya kidigitali yanaweza kuwaathiri wasichana kwa kuingilia faragha zao, kuvuruga masomo yao na unyanyasaji mtandaoni.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 10 min
    Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania

    Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania

    Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto. Prisca na wenzake kutokana na kupenda kazi yao wanafanya kila njia iwe ni kutumia usafiri wa bodaboda au hata kuvuka mito na mabonde kwa miguu kuhakikisha chanjo zinafika. Kufahamu kwa kina ungana na Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Tanzania.

    • 3 min
    Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili 

    Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili 

    Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.
    (Taarifa ya Anold Kayanda)
    Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.
    Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi  na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.
    WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.
    Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani.
    WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo.
    Tags: Siku za UN, WHO, Chanjo, EPI, Wiki ya Chanjo Duniani

    • 1 min
    Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO

    Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO

    Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023. 
    (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
    Asante Leah. Kwa hakika ripoti hiyo ya “Mgogoro wa kimataifa wa chakula” GRFC inasema kiwango cha watu wenye njaa duniani kiliongezeka kwa watu milioni 24 kutoka mwaka 2022 hadi 2023 na ni asilimia 21.5 ya watu waliofanyiwa tahimini  na hicho ni kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19 limesema shirika la FAO likiongeza kuwa idadi ya walio na njaa duniani inaendelea kuongezeka.
    Ripoti imetaja sababu kuu tatu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa janga la njaa duniani ambazo ni mosi migogoro na vita ambapo inasema inaathiri katika nchi 20 zilizo na jumla ya watu milioni 135 wanaokabiliwa na njaa zikiwemo Sudan, Yemen na Palestina katika Ukanda wa Gaza.
    Pili ni matukio mabaya ya hali ya hewa yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa chanzo cha njaa katika nchi 18 na kuathiri kwa njaa zaidi ya watu milioni 77.
    Na tatu mdororo wa kiuchumi uliokuwa chachu ya njaa katika nchi 21 na kuathiri jumlaya watu milioni 75.
    FAO imesema kwa miaka minne mfululizo takriban asilimia 22 ya watu waliofanyiwa tathimini duniani wamekuwa wakikabiliwa na kutakuwa na uhakika wa chakula. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Mgogoro huu unahitaji hatua za haraka. Kutumia takwimu zilizoainishwa katika ripoti hii ili kufanyia marekebisho mifumo ya chakula na kushughulikia mizizi ya kutakuwa na uhakika wa chakula itakuwa muhimu sana”
    Kwa mujibu wa ripoti waathirika wakubwa ni watoto, wanawake na watu wenye ulemavu.Mtandao wa kimataifa dhidi ya mgogoro wa chakula imetoa wito wa haraka wa kubadili mtazamo ili ujumuishe amani, hatua za kuzuia na za maendeleo sambaba na juhudi za dharura kuvunja mzunguko wa janga la njaa ambalo linasalia katika viwango vya juu
     

    • 2 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Serial
Serial Productions & The New York Times
Up First
NPR
The Tucker Carlson Podcast
Tucker Carlson Network
Prosecuting Donald Trump
MSNBC
The Megyn Kelly Show
SiriusXM

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
UNcomplicated
United Nations
Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Interviews
United Nations