100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

    Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 anajibu swali aliloulizwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwamba Je, Lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu linalohamasisha usawa wa kijinsia litafikiwa huko Zanzibar kufikia mwaka 2030?

    • 3 min
    Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

    Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

    Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao. 
    Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa takwimu hizo likinukuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, huku ikisema kuwa idadi inazidi kuongezeka kila uchao.
    IOM kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na Nairobi, Kenya inasema mvua hizo za masika zimesababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya udongo na kuharibu miundombinu muihmu kama vile barabara, madaraja na mabwawa ya maji.
    Mkurugenzi wa IOM Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika Rana Jaber anasema mafuriko hayo ya kipekee na yaliyosababisha uharibifu yameibua ukweli mchungu wa mabadiliko ya tabianchi, kwa kusababisha vifo na kufurusha watu makwao, watu ambao sasa wanakabiliwa na kazi kubwa ya kujijenga upya huku hali zao zikizidi kuwa taabani.
    Ni kwa mantiki hiyo anaesema katika nyakati hizi muhimu, wito wa IOM unasalia kuchukuliwa kwa hatua endelevu na za dharura za kutatua ukimbizi wa binadamu unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi.
    Pamoja na kushirikiana na serikali na wadau kusambaza misaada ya hali na mali ya kuokoa maisha ikiwemo fedha taslimu kwa walioathiriwa huko Burundi, Kenya, Somalia, Ethiopia na Tanzania, IOM inasema mjadala ujao huko Ujerumani kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC ni dhahiri shairi kuwa mazungumzo kuhusu tabianchi lazima yazingatie ukimbizi utokanao na janga hilo.
    Afrika inaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi licha ya kuchangia asilimia 4 pekee ya hewa chafuzi duniani.

    • 1 min
    08 MEI 2024

    08 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, na wakimbizi wanaorejea nchini Sudan Kusini kutoka Sudan. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?
    Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.Katika makala Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, alipata nafasi kuzungungumza na Anold Kayanda.Na mashinani inatupeleka katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri wa Kidemkrasia ya Congo DRC, ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku kadhaa sasa zimesababisha maafa, ikiwemo maelfu ya familia kuathirika. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 10 min
    Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM

    Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao. 
    Waswahili husema “Mkataa kwao mtumwa” na hili ndio hasa alilowaza Bi. Lydia John Wol Mabior ambaye alikuwa ukimbizini nchini Sudan lakini huko nako vita ilipoanza akakumbuka usemi “Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani” kwani ilikuwa si hali. Anasema, “Nilipokuwa Khartoum sikulala usiku wala mchana, niliona ni bora nije kuteseka Sudan Kusini. Na leo nina furaha sana kwasababu nimefika nchini kwangu”
    Lidya ya familia yake miaka kadhaa iliyopita aliikimbia nchini yake ya Sudan Kusini pale vita vilipozuka. Na shukran ziliendee shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo limefanikisha kumrejesha nchini mwake.
    “Niliambiwa kuna shirikia lakutusaidia kufika Sudan Kusini, na tangu tumefika hapa eneo la Renk, tumepewa msaada wa kifedha tunamshukuru Mungu. Baada ya kusafiri kwa boti kutokea Malakal tulipewa msaada na IOM na sasa tunachotaka ni kusaidiwa Kwenda nyumbani kwetu huko Wau kwa msaada wa IOM.”
    Lydia ametoa shukran zake za dhati kwa shirika la IOM na wadau wake kwa msaada wote waliowapatia katika kusaidia kuwaunganisha tena na familia zao.

    • 1 min
    07 MEI 2024

    07 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako Umoja wa mataifa uko mstari wa mbele kuwapa msaada wakenya wanaotatizika kutokana na mafuriko. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza, Uhamiaji na misitu. Mashinani inatupeleka nchi Haiti, kulikoni? 
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea kusisitiza wito wake wa kusitishwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka wote na kuepusha zahma kubwa ya kibinadamu kwa watu wa Gaza. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani amesema “Tuko katika wakati maamuzi kwa ajili ya watu wa Palestina na Israeli na kwa hatima ya Ukanda mzima.Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limezindua Ripoti ya Dunia ya Uhamiaji 2024, ambayo inaonyesha mabadiliko makubwa katika mifumo ya uhamiaji duniani, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao na pia ongezeko la fedha zinazotumwa kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope amezindua rasmi ripoti hiyo nchini Bangladesh, nchi ambayo iko mstari wa mbele katika changamoto za uhamiaji na kusema "Ripoti ya Uhamiaji Duniani ya 2024 inasaidia kuondoa utata wa uhamaji wa binadamu kupitia takwimu na uchambuzi unaozingatia ushahidi." Kati ya mwaka 2,000 na 2022 ongezeko la utumaji fedha nyumbani kimataifa kwa mujibu wa Ripoti lilikuwa ni zaidi ya asilimia  650 na kufikia dola bilioni 831 bilioni.Na jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu kikao cha 19 kinaendelea hapa kwenye makao makuu wa Umoja wa Mayita New York Marekani kikimulika mada mbalimbali ikiwemo jukumu la sheria katika afya ya misitu. Akizungumzia hilo Patricia Kameri-Mbote mkurugenzi wa idara ya sheria katika shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP amesema “Misitiu ni muhimu sana katika kushughulikia majanga matatu makubwa yanayoikabili Dunia ambayo ni uchafuzi wa hewa, opotevu wa bayoanuwai na mabadiliko ya tabianchi.” Na kwamba afya ya misitu ni nguzo ya kuhakikisha afya ya sayari dunia na kwa mantiki hivyo sheria za kulindwa kwa misitu zina wajibu muhimu sana na sio chaguo bali ni lazima.Na mashinani huku kukiwa na ghasia zinazoendelea nchini Haiti, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limepanua kwa haraka msaada wake wa chakula, na kufikia zaidi ya watu nusu milioni tangu kuanza kwa mzozo, ikiwa ni pamoja na watoto wa shule, Evenie Joseph, mama mjasiriamali anasema mpango wa mlo shuleni umeleta manufaa kwa watoto wanaokimbia ghasia hizo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

    • 12 min
    UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

    UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inaanzia Bujumbura Burundi kisha inakupeleka Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kama inavyosimuliwa na Evarist Mapesa.

    • 3 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Serial
Serial Productions & The New York Times
Up First
NPR
The Ben Shapiro Show
The Daily Wire
Pod Save America
Crooked Media
The Megyn Kelly Show
SiriusXM

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
Interviews
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations
ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas
United Nations