Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

  1. 5 HR AGO

    27 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya na lishe katika nchi zinazokumbana na ukame. Makala tunakwenda Ureno na mashinani nchini Sudan, kulikoni? Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, amesema amestushwa na kusikitishwa na kifo cha aliyetarajiwa kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Engelbert Ndungulile kutoka nchini Tanzania.Awamu ya pili ya mradi wa kuboresha lishe, SUN II nchini Zambia umewezesha wakulima kupanda mazao yanayohimili ukame na vile vile kukabiliana na viwavi jeshi kwa kutumia mbinu za asili, mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja la kuhudumia watoto, UNICEF ili wakulima wasikumbwe na njaa wakati huu ambapo ukame umetikisa nchi za kusini mwa Afrika.Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika jukwaa lao wakiwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+.Na mashinani fursa ni yake Shaza Ahmed, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la wanawake Nada El Azha linalotoa msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudana akitoa wito kwa viongozi wa kimataifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!

    10 min

About

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More From United Nations

To listen to explicit episodes, sign in.

Stay up to date with this show

Sign in or sign up to follow shows, save episodes and get the latest updates.

Select a country or region

Africa, Middle East, and India

Asia Pacific

Europe

Latin America and the Caribbean

The United States and Canada