Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA
Nchini Tanzania wanufaika wa mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.
Information
- Show
- Channel
- FrequencyUpdated daily
- Published25 November 2024 at 15:16 UTC
- Length4 min
- RatingClean