Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa hiyo kazi yenyewe.
Kazi ya Zuchu ilianza kabla hajaipata hiyo kazi yenyewe na ilikua kazi haswa kuipata na Mama yake Bi Khadija Kopa ndo alikua kinara kwenye hiyo connection ambayo Binti yake alikua anaitaka ili aweze kuwa msanii wa Diamond, na hayo ndo yalikua maneno yake hasa, toka alivyorudi kutoka Nigeria kwenye mashindano ya kusaka vipaji na alikua hajielewi elewi kwa kiasi flani ni kitu gani alikua anataka kufanya na kama basi kutakua na la kufanya inabidi liwe kutoka WCB na sio sehemu nyengine yoyote na agulia nini kilitokea? WCB aliipata na kilichokua kinatakiwa baada ya hapo ni UVUMILIVU wa HALI YA JUU.
Kwenye vitabu vyangu vyote Bi Zuhura Othman Soud ndo muandishi wangu BORA wa KIKE kuwahi kutokea katika kizazi chetu hiki cha Bongo Flava, na naweza sema hivyo wakati wowote iwe usiku au mchana, kipaji hicho ndicho kilichonifanya mimi nistaajabu sana na kutaka kuongea nae na kumuuliza yote yale ambayo nilikua nataka kumuuliza, ingawa humo humo nilikua nishajijibu kutoka kwenye historia ya familia atokayo ingawa hiyo haikutakiwa ndo iwe lazima, lazima mtoto wa Khadija Kopa na Othman Soud awe muandishi mzuri maana wazazi wake wamejaa vipaji tena na Baba yake ndo muandishi mkubwa wa nyimbo nyingi za Mama yake zilizowahi kuvuma.
Kwa umri wake wakati mwengine hujiuliza kajuaje haya maneno yote, anajua maana yake hii? Kasikia wapi hili neno au pengine je huwa anamfikiria Mama yake (ambaye ndo kipenzi chake na ndo amemlea) wakati anaandika hii? Anaona aibu? Je huwa wanaongelea hayo mashairi wanapokua wawili tu? Mazungumzo huendaje?
Sasa turudi kwenye kazi hiyo ya kuanza kuifanya baada ya kuipata sasa WCB, ukiachana na msoto mrefu alopitia, WCB wenyewe walikua waangalifu sana kwenye mipango ambayo ilikua ikiandaliwa kwaajili yake, yeye ndo msanii wa KWANZA wa KIKE kuwahi kutokea kwenye label kwahiyo ukichana na kipaji pia uwekezaji wa hali ya juu ulitakiwa ufanyike and boy they did that. Toka single yake ya kwanza mpaka wakati naandika hii Zuchu hakuwahi kuwa na kazi chafu, album yake ya kwanza alotoka nayo ya I am Zuchu ilikua na nyimbo 7 ambazo zote zilienda kufanya vizuri, na mpaka leo kila wimbo ambao anaachia ni wa moto, tukisema namba moja nadhani namba zake pia zinasema hivyo za kila sehemu, hakuna chumvi yoyote ndani yake.
Vipi sasa anaweza ku maintain hii schedule yake ilojaa mambo kuanzia asubuhi mpaka usiku? Kutoka Jumatatu mpaka Jumapili? Je ana muda kwaajili yake? Ana mpenzi? Mipango yake je? Endelevu? Vipi hizi title ambazo tunampa anazichukuliaje? Kuna pressure yoyote? Na kuhusu familia je? Kuna pressure yoyote kwenye baadhi ya mambo na maamuzi? Na kwenye label nako? Watu na furaha na kazi yake?
Kwa kuanzia msimu wetu wa TANO nadhani introduction ya Ms Zuchu inatufaa sana na yangu matumaini uta enjoy pia.
Asante kwa support ya toka siku ya kwanza ulipoanza kutupa macho na masikio yako.
You’re the best, nakukumbusha tu kwamba mengi yajayo yatakufurahisha In Shaa Allah maana kazi ndo kwaanza imeanza.
Love,
Salama
--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
Information
- Show
- FrequencyUpdated weekly
- Published16 June 2022 at 18:00 UTC
- Length56 min
- Season7
- Episode1
- RatingClean