100 episodes

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu United Nations

    • News
    • 5.0 • 4 Ratings

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain

    Uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain

    Jukwaa la 5 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 linaanza kesho kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama ukileta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo wajasiriamali kutoka pembe zote za dunia. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na na maudhui ni kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuendeleza uvumbuzi na ukuaji wa kiuchumi. Jukwaa hili linalenga basi kupatia majawabu changamoto za dunia ikiwemo umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi, amani, haki kwa muktadha wa SDGs. 
    Dkt. Hashim Hussein, ni mtaalamu wa kuendeleza uwekezaji katika shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO anaeleza ni nini hasa wanatarajia kutoka jukwaa hili alipopata fursa kuzungumza na Assumpta ambaye tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.

    • 4 min
    Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini

    Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini

    Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. 
    Kwa mujibu wa Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, “Shambulio hilo limeharibu paa la hospitali katika kituo cha huduma za dharura kwenye Hospitali ya Sourthen katika mji wa El Fasher ambayo ndio hospitali pekee inayofanyakazi kwas asa katika jimbo la Darfur Kaskazini na ambako vifaa vya matibabu na dawa sasa karibu vinakwisha.” 
    Amesema takriban watu 800,000 wanaishi katika mji wa El Fasher na maelfu ya maisha yao yako hatarini huku taifa zima la Sudan likiwa katika hali mbaya.
    Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema makumi ya raia waliuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano mapya  makubwa yaliyozuka Ijumaa kati ya vikosi vya serikali ya Sudan SAF na vikosi vya msaada wa haraka RSF katika eneo la Darfur Kaskazini ambalo ndilo lililosalia chini ya udhibiti wa serikali.
    Shirika hilo linasema hivi sasa karibu watu milioni 25 nchini Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu na watu milioni 17.7 miongoni mwao wanakabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula na kuna hofu kubwa ya kurejea kwa baa la njaa Darfur.
    Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la luhudumia wakimbizi UNHCR na la uhamiaji IOM yamesema takriban watu 570,000 wametawanywa katika jimbo la Darfur Kaskazini katika miezi 13 iliyopita, wengine milioni 6.7 nchini Sudan ni wakimbizi wa ndani huku milioni 1.8 wamekimbilia katika nchi za jirani.

    • 1 min
    13 MEI 2024

    13 MEI 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makali yanayoendelea nchini Sudan, na huduma za afya uzazi Kalobeyei nchini Kenya.  Makala inatupeleka Bahrain ambako Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza Manama hapo kesho Jumanne, na mashinani tunasikiliza simulizi ya mkimbizi wa ndani nchini DRC.
    Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto.Makala inatupeleka Bahrain huko Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza kesho Jumanne Kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Manama likiwaleta pamoja washirika mbalimbali wakiwemo viongozi katika sekta ya biashara duniani na wajasiriamali. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na mwenzetu Assumpta tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    • 11 min
    Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

    Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

    Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. 
    Anasema anaitwa Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei.  
    “Katika hospitali hii tunafanya kazi na jamii za wenyeji na wakimbizi, wanapokuja najitambulisha na kuwaeleza kazi yangu katika idara hii na pia nawaelezea kile ninachokuelezea ni kile ambacho hata mimi nilipitia.”
    Wakati ulimwengu ulisherehekea siku ya wauguzi hapo na siku ya wakina mama hapo jana Mei 12, Rose anaeleza kile kinachompa furaha zaidi katika kazi yake hii ya ukunga.
    “Ni furaha yangu ninapomuona mjamzito anapokuja kwa ajili ya kujifungua na mwisho wa siku anajifungua mtoto mwenye afya njema. Huduma hapa hutolewa bure ukitoa hata sumni bado itakurudia mwenyewe. Ni kama ninapotoa huduma kwa hawa wakina mama vyema najua zawadi yangu ipo pale.”

    • 1 min
    Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’

    Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.

    • 3 min
    Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya

    Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya

    Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.
    Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.

    • 1 min

Customer Reviews

5.0 out of 5
4 Ratings

4 Ratings

Top Podcasts In News

The Daily
The New York Times
Up First
NPR
Serial
Serial Productions & The New York Times
The Ben Shapiro Show
The Daily Wire
The Megyn Kelly Show
SiriusXM
The Dan Bongino Show
Cumulus Podcast Network | Dan Bongino

More by United Nations

UN News - Global perspective Human stories
United Nations
Noticias ONU - Mirada global Historias humanas
United Nations
Interviews
United Nations
联合国新闻 - 全球视野, 常人故事
United Nations
The Lid is On
United Nations
أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية
United Nations