Binti Utalii

community voices in focus
Binti Utalii Podcast

To advocate on gender base violence, Women empowerment and Sexual reporductive health and Right .

Episodes

  1. 17/12/2020

    Karibu Binti Utalii

    BINTI UTALIINi progam inayowalenga Mabinti wa umri wa miaka 18-35 yenye lengo la kuwaleta Pamoja na kusimama katika kukuza utalii na utamaduni kupitia Sanaa na mitindo mbalimbali. Vilevile program hii imelenga kupitia utalii na tamaduni kuweza kutokomeza changamoto mbali mbali zinazo mkabili mtoto wa kike kama vile ukeketaji,ubakaji,mimba na ndoa za utotoni, na matendo yote ya ukatili wa kijinsia. Program hii imelenga kuwainua Mabinti (Women empowerment) kuweza kujitegemea na kujisimamia katika maeneo yafuatayo.1.Kijamii- hapa Mabinti watajishughulisha na Kazi mbali mbali za kijamii kwa lengo la kujenga ustawi bora kuwa jamii unayo wazunguka na wao Binafsi.2. Kiuchumi- kuwawezesha Mabinti Kujifunza na kutekeleza miradi mbali mbali ya kiuchumi ili kuweza kujiletea maendeleo.3 . Kiutamaduni - hapa Mabinti wanajifunza namna ya kuenzi na kutunza tamaduni zetu na kuzitumia kuweza kujiletea kipato tamaduni hizo ni kama ngoma za asili vyakula vya asili mavazi na nyinginezo.4. Utalii Ujasiriamali hapa Mabinti watajifunza namna ya kutumia Utalii Kama njia ya kujipatia kipato na kuweza kuleta maendeleo binafsi na ya taifa kea ujumla Mabinti watatembelea maeneo tofauti tofauti ya kitalii.SIFA ZA KUWA SEHEMU YA BINTI UTALII.1. Uwe tayari kujitoa kwa jamii inayokuzunguka na kujituma katika kutekeleza majukumu utakayopewa.2. Utapaswa kulipa ada ya kiingilio kiasi cha shilingi 10000/= ambayo ulipwa mara moja tu.3. Uwe tayari kujiheshimu na kuheshimu wengine muda wote wa Maisha ya Pamoja na mabinti wenzako.4. Uwe mbunifu na mwenye kujituma katika kuleta mafanikio chanya5. Uwe mwenye kutaka kujifunza na kuwafunza wengine.Mwisho kwa upekee kabisa tunapenda kuwakaribisha wote kuweza kuwa sehemu ya binti utalii na kuhakikisha tunafikia malengo kwa Pamoja.

    2 min

About

To advocate on gender base violence, Women empowerment and Sexual reporductive health and Right .

To listen to explicit episodes, sign in.

Stay up to date with this show

Sign in or sign up to follow shows, save episodes and get the latest updates.

Select a country or region

Africa, Middle East, and India

Asia Pacific

Europe

Latin America and the Caribbean

The United States and Canada