Nukta the Podcast

Nukta Habari

Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.

  1. 9h ago

    Ifahamu Halloween, sherehe za kale zilizohusishwa na ulimwengu wa wafu

    Kila ifikapo Oktoba 31, watu katika maeneo mbalimbali duniani, hususan Marekani huonekana wakiwa katika mavazi na vipodozi vya kutisha wakiadhimisha sherehe maarufu zinazojulikana kama Halloween. Lakini ushawahi kujiuliza, sherehe hii ilianzia wapi, maana yake nini na kwa nini mavazi ya kutisha yamekuwa sehemu muhimu ya maadhimisho yake? Kwa mujibu wa Maktaba ya Congress ya Marekani, historia ya Sherehe za Halloween ilianzia katika karne ya pili kabla ya Kristu, katika sherehe za kale za watu wa zamani waliokuwa wanajulikana kama Waselti. Katika kipindi hiko ambacho ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita sherehe hizo zilikuwa zikijulikana kama (Sow-in) na zilikuwa zikihusishwa na mwisho wa msimu wa mavuno.  Waselti ni makabila na jamii za kale za Ulaya zilizokuwa na lugha, mila na tamaduni zinazofanana, zilizoishi katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, yakiwemo Ireland, Scotland, Wales, Uingereza na Ufaransa ya sasa. Katika sherehe za Sow In Waselti waliamini kuwa mpaka kati ya ulimwengu wa walio hai na waliokufa ulikuwa mwembamba sana hivyo waliamini kwamba roho za marehemu zingeweza kurejea kuwatembelea walio hai.  Waselti waliweka utamaduni wa kusheherekea sherehe hizo kwa kuvalia ngozi za wanyama,na vinyago vya kutisha ili wafanane na wafu wakiamini kwamba kwa kufanya hivyo wangeweza kujikinga dhidi ya roho zilizodhaniwa kuzunguka duniani usiku huo. Na hii ndio sababu mavazi ya kutisha yameendelea kuwa sehemu maarufu ya maadhimisho ya Halloween. Hata hivyo, historia ya Halloween iliendelea kubadilika baada ya kuenea kwa Ukristo. Katika karne ya nane, Kanisa Katoliki liliweka Novemba 1 kuwa Siku ya Watakatifu Wote, na Novemba 2 kuwakumbuka waumini waliokufa. Mabadiliko hayo yaliifanya sherehe ya Sow in kuingiliana na kalenda ya maadhimisho ya Kikristo. Na usiku wa kuamkia Novemba 1, yaani Oktoba 31 ulianza kujulikana kama All Hallows’ Eve, maana yake ‘Usiku wa Kuamkia Siku ya Watakatifu Wote’ jina ambalo baadaye lilifupishwa na kuwa Halloween.  Baadaye, wahamiaji kutoka Ulaya, hasa Ireland, walichangia kueneza Halloween nchini Marekani katika karne ya 19. Kadiri muda ulivyopita, sherehe hiyo ilibadilika na kuwa sehemu ya burudani na utamaduni maarufu, ikihusisha mavazi ya wahusika wa kutisha, mapambo ya maboga yaliyochongwa, sherehe na watoto kuomba pipi. Ingawa Halloween ya sasa inaonekana zaidi kama burudani, historia yake inahusishwa na mila za kale na mabadiliko ya kidini na kitamaduni yaliyotokea kwa karne nyingi.  Mavazi ya kutisha ni sehemu ya urithi huo wa kihistoria, ingawa maana yake kwa washiriki wa leo inaweza kuwa burudani tu, bila kuhusisha imani za kale kuhusu roho za wafu.

    Ifahamu Halloween, sherehe za kale zilizohusishwa na ulimwengu wa wafu
  2. Jul 18

    FIFA kuuza kipande cha nyasi uwanja wa fainali za kombe la dunia kwa Sh1 milioni

    Mbio za fainali za Kombe la Dunia zinaendelea kuchanja mbuga huku mashabiki wa nyota wa soka Lionel Messi wakiendelea kutembea kifua mbele mara baada ya timu wa taifa ya Argentina kufanikiwa kumng’oa mwingereza kwa bao moja kwa mbili kwenye hatua ya nusu fainali. Hata hivyo kivumbi na jasho kinatarajiwa kuonekana siku ya Jumapili Julai 19, 2026 ambapo kidume wa mashindano haya makubwa zaidi ya michezo duniani atakwenda kuonekana baada ya dakika 90 za mtanange kati ya Argentina na Hispania kutamatika katika dimba la New York New Jersey nchini Marekani. Mchezo huu wa fainali hauendi tu kuwa mchezo wa kawaida bali kwa kila timu inakwenda kuandika historia mpya itakaponyakua taji hilo lenye thamani zaidi kuliko mataji yote katika ulimwengu wa soka. Kwa Argentina iwapo atashinda anakwenda kuweka historia ya kuchukua kombe hilo mara mbili mfululizo tangu atwae taji hilo mwaka 2022 pale nchini Qatar kitu ambacho ni nadra sana kufanyika katika historia ya soka. Kadhalika kwa Hispania iwapo atashinda atakwenda kumaliza ukame wa miaka 16 tangu kutwaa taji hilo mwaka 2010 pale Afrika Kusini chini ya kizazi cha kina Xavi na Iniesta. Lakini kwa mwaka huu kuna jambo la kushangaza kidogo kwani Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) halijataka historia ya mtanange huo kubakia katika picha na video tu na badala yake imetangaza kuuza vipande vya nyasi za uwanja utakapochezeka mchezo huo ambao kuushudia live itakulazimu kununua tiketi kwa zaidi ya Sh15 milioni kwa daraja la kawaida. Kwa mujibu wa FIFA vipande hivyo vya nyasi vinakwenda kuuzwa kama bidhaa maalum ya ukumbusho, huku bei zikianzia dola 450 za Marekani, ambayo kibongo bongo ni zaidi ya Sh1 milioni kwa kipande kimoja. Kwa mashabiki wanaotaka kumbukumbu ya kiwango cha juu zaidi, kuna vifurushi vinavyofikia hadi dola 3,000 ambayo ni takriban Sh8 milioni.  Ikiwa FIFA itafanikiwa kuuza idadi yote ya vipande maalum vilivyowekwa, taasisi hiyo inatarajia kuingiza kiasi cha Dola za Marekani milioni 11 zaidi ya Sh29 bilioni. Je, uko tayari kununua kipande cha nyasi kwa Sh1 milioni?

    FIFA kuuza kipande cha nyasi uwanja wa fainali za kombe la dunia kwa Sh1 milioni

About

Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.