Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

  1. 12h ago

    08 OKTOBER 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Umoja wa Mataifa unaonya kwamba pengo la kidijitali linaweza kubadilika kuwa pengo la Akili Mnemba (AI), na hatimaye kuwa pengo la maendeleo, usalama na mamlaka ya nchi. Shrika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP linatoa takwimu likisema barani Afrika kwa mfano, ni chini ya asilimia mbili ya uwezo wa vituo vya kuhifadhi na kuchakata data duniani ndi upo barani umo, huku ni asilimia tano tu ya wabunifu wa AI barani humo ndio wana uwezo wa kupata nguvu za kompyuta wanazohitaji. Hali hiyo ndio msingi wa mazungumzo yafuatayo kati ya Anold Kayanda wa Idhaa hii, na Gloria Anderson, Mkurugezi wa shirika la TEDI Tanzania. Gloria Anderson alikuwa New York Marekani kuhududhuria mikutano mbalimbali wakati wa UNGA81. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo. • Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo wamezindua mpango mpya wa kimataifa wa kukabiliana na matatizo ya shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito ambayo huathiri mamilioni ya wanawake duniani kote kila mwaka. Shinikizo la damu huweza kusababisha kudhurika kwa viungo vya mwili hasa figo ambapo mpango husika utaleta pamoja utafiti, dawa, mwongozo wa kitabibu, mifumo ya afya na hatua za kisiasa ili kuhakikisha nafasi ya mwanamke kuishi salama wakati wa ujauzito na kujifungua mtoto haiamuliwi na mahali anapoishi. • Nasalia na afya ambapo leo ikiwa ni siku ya uoni duniani, WHO inakumbusha apu yake ya kuchunguza macho ambapo mtu anaweza kutumia simu janja kujifanyia uchunguzi wa awali kabla ya kwenda kwa mtaalamu wa macho ili kubaini iwapo macho yake yako salama au la, na kisha kuwahi hospitali. Apu hiyo inaitwa WHOeyes, na ni bure huko App Store au Google Store. WHO inasema uchunguzi wa mapema huepusha uharibifu mkubwa zaidi wa macho. • Na hatimaye huko kwenye maeneo ya ndani zaidi huko Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS unasaidia vijana kuachana na magenge ya uhalifu ili waweze kujenga upya maisha yao kupitia mipango mipya. Cephus Diggs ambaye Afisa wa UNMISS akihusika na ulinzi anasema, “tuliweza kuwaleta pamoja viongozi wa makundi mbalimbali ya magenge, wakiwemo wasichana waliokuwa kwenye magenge. Kwa sasa, tunajihusisha na shughuli za ukaushaji wa samaki kwa kutumia moshi ili waweze kunufaika na shughuli hizo na kufikiria upya namna ya kushiriki katika shughuli zenye manufaa, badala ya kukaa tu au kuzurura kambini na kuwashambulia watu.” Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

  2. 3d ago

    05 OKTOBA 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Wiki iliyopita katika Ofisi ya Kenya ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo, KALRO iliyoko jijini Nairobi nchini Kenya, FAO nchini Kenya kwa kushirikiana na serikali walizindua mradi wa SoilFer. Mradi huu unahusisha kuwa na ramani ya aina za udongo za taifa hilo la Afrika Mashariki ili kusaidia wakulima kuongeza tija kwenye kilimo. Je ina maana gani? Na kwa nini hasa? Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS- Kenya alizungumza na Barack Okoba, Afisa Programu FAO, Kenya anayeanza kwa kufafanua kilichofanyika siku hiyo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili. • Leo ni siku ya kimataifa ya makazi duniani na mwaka huu kauli mbiu ni Makazi bora kwa wote, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi, UN-Habitat Anacláudia Rossbach, amesema makazi yanapaswa kuchukuliwa kama kipaumbele cha umma sambamba na ardhi na huduma za msingi, huku uwekezaji zaidi ukielekezwa katika jamii na ushirikiano ukiimarishwa katika ngazi mbalimbali za serikali, sekta binafsi na mashirika ya kiraia. Rossbach amesisitiza kuwa takwimu pekee zinaweza zisielezee kwa kina janga la makazi kwani..“familia inaweza kuwa na nyumba, lakini bado wanatumia fedha nyingi kwa pango na wakabakia na fedha kidogo sana kwa ajili ya chakula, elimu na afya. Nyumba inaweza kuwa bei nafuu lakini iko mbali na mahala pa kazi, shule au usafiri.” • Leo pia ni Siku ya Walimu Duniani, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa wito wa kuimarisha hadhi na mazingira ya kazi kwa walimu milioni 107 duniani. UNESCO inasema takwimu mpya zinaonesha kuwa katika nchi mbili kati ya kila tano zilizochambuliwa, walimu wanalipwa mishahara midogo kuliko wataalamu wengine wenye sifa zinazolingana, hali inayofanya iwe vigumu kuvutia walimu wapya na kuwaendeleza waliopo katika taaluma hiyo. • Na tukimalizia na masuala ya ulinzi na usalama wa dunia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres usiku wa kuamkia leo amesafiri kutoka Marekani kwenda nchini Pakistan. Pamoja na mambo mengine atakayo fanya nchini humo ziara hii, Guterres atazungumza na viongozi wa Pakistan ambao ni kiungo muhimu cha mazungumzo ya kidiplomasia baina ya Iran na Marekani nchi ambazo zipo kwenye mzozo ambao umeathiri mustakabali wa ulimwengu hususan kwenye kupanda kwa gharama za vitu mbalimbali sababu ya vita baina ya nchi hizo. • Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili huko Zanzibar, BAKIZA anafafanua maana ya neno, MAFAMBA. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Ratings & Reviews

5
out of 5
5 Ratings

About

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More From United Nations